jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Uzalendo kwa nchi yako uko katika nyanja tofauti na ninaweza kusema hata mtu anaesaidia kuinua michezo kuhakikisha nchi yake inafanikiwa ni Mzalendo. Sio kuingia vitani na kuipigania nchi yako ndio uzalendo pekee. Kuna vitu vingi vitakavyoweza kukufanya uonekane mzalendo kwenye nchi yako, kuna walimu wanaotumia taaluma yao kuinua kiwango cha elimu nchini wao pia ni wazalendo, kuna madaktari wanaotumia udaktari wao kuinua hali ya afya nchini wao pia ni wazalendo, kuna wachezaji soka wanaojitahidi kila siku ili wahahakikishe nchi yao inashinda wao pia ni wazalendo, kuna wachangiaji wa JF ambao wako hapa kila siku kuipigia kelele serikali ifuate mfumo wa haki na upigaji vita rushwa wao pia ni wazalendo, kuna wabunge wetu kina Dr. Slaa wanaotumia bunge kuwakilisha vilio vyetu wao pia ni wazalendo. Ndugu Mushi sielewi wewe kwako uzalendo ni upi lakini nataka nikukumbushe tu uzalendo uko kwenye njanya mbalimbali. Labda Mushi tupe maana yako ya uzalendo.
Kwangu mimi uzalendo ni kulipenda Taifa lako kwa moyo mmoja na bila kujali kama utanufaika ama la...Hapo kwangu huo ndio uzalendo wenyewe.
Usidhani kwamba hawajui hawa watu...Wangekuwa wazalendo kiukweli Taifa lingekuwa mbali sana kimaendeleo.
Kama ukienda mahali ukakuta kucheza bao ni dili basi ukausadia mchezo wa bao watakuona wewe ni mwenzao..Huo ndio uafrika,utamaduni ambao wageni waliutumia vibaya na certainly wanaendelea kufanya hivyo...Wasaidie maendeleo ya kweli na shughuli za kujenga Taifa na si mambo ya soka na mdundiko.
Nasema sitaki tena waafrika tuendelee kufanywa makatuni.