Mohamed Dewji ametajwa kuwa miongoni mwa watu matajiri Duniani, ana utajiri wa USD 2.2 Bilioni

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Jarida la Forbes Mwaka 2025 limemtaja Mtanzania Mohamed Gullam Dewji “MO Dewji” katika orodha ya mabilionea wa Afrika, listi mpya iliyotolewa na Forbes, Machi 29, 2025, imeonesha MO anashika nafasi ya 12, akiwa na utajiri wenye thamani halisi ya mali ya Dola za Marekani Bilioni 2.2 akipanda kwa Dola za Marekani Milioni 400 ikilinganishwa na Dola za Marekani Bilioni 1.8 za Mwaka 2024.
Jarida la Forbes (2025) limemtaja Mfanyabiashara  wa Tanzania Mohamed Dewji, kuwa miongoni mwa...jpg
Mnigeria, Aliko Dangote ambaye ni Mmiliki wa Kampuni ya Dangote kutoka Nigeria anashika nafasi ya kwanza katika orodha hiyo ukiwa ni Mwaka wa 14 mfululizo akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia Dola za Marekani Bilioni 23.9, ikilinganishwa na Dola za Marekani Bilioni 13.9 Mwaka 2024.

Katika orodha hiyo, raia wa Afrika Kusini, Johann Rupert anakamata nafasi ya pili akiwa na utajiri wa Dola za Marekani Bilioni 14 sawa na ongezeko la 39%.

Anafuatiwa na mfanyabiashara wa Afrika Kusini, Nicky Oppenheimer na familia yake, wanaokamata nafasi ya tatu kwa Dola za Marekani Bilioni 10.4.

Orodha ya mabilionea wengine wa Afrika na thamani ya utajiri wao kwenye mabano ni:
Screenshot 2025-04-04 090450.jpg

Nassef Sawiris kutoka Misri ($9.6 bilioni)

Mike Adenuga kutoka Nigeria ($6.8 bilioni)

Abdulsamad Rabiu wa Nigeria ($5.1 bilioni)

Naguib Sawiris kutoka Misri ($5 bilioni)

Koos Bekker kutoka Afrika Kusini ($3.4 bilioni)

Mohamed Mansour kutoka Misri ($3.4 bilioni)

Patrice Motsepe wa Afrika Kusini na Rais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) ($3 bilioni)

Issaad Rebrab kutoka Algeria na familia yake ($3 bilioni)

Mohamed Dewji wa Tanzania ($2.2 bilioni)

Michael Le Roux wa Afrika Kusini ($2.2 bilioni)

Othman Benjelloun na familia yake kutoka Morocco ($1.6 bilioni).

Dewji, Mkurugenzi Mtendaji wa Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) amekuwa akitumia sehemu ya utajiri wake kuwawezesha Watanzania, hasa kupitia ajira anazozalisha.

METL, iliyoanzishwa na baba yake MO miaka ya 1970, ni moja ya makampuni makubwa Tanzania, na Dewji ameitumia kufanikisha dhamira yake ya kuboresha maisha ya wananchi wa kawaida.

Mtazamo wake mkubwa umekuwa kufanya mabadiliko katika sekta zisizopewa kipaumbele, hasa kilimo, ambapo ameelekeza nguvu zake katika kufufua mashamba ya mkonge yaliyotelekezwa na kuzalisha ajira na fursa nyingi za kiuchumi kwa wananchi.
F50O0rdXEAAK8bl.jpeg
Uanzishaji wa Mo Cola umewawezesha Watanzania kunaojihusisha na biashara ndogo ndogo kupata fursa za kiuchumi huku akichagiza mapambano ya kibiashara na makampuni makubwa ya vinywaji baridi duniani.

Katika sekta ya huduma za kijamii na misaada wa kibinadamu, Dewji kupitia Mohamed Dewji Foundation (MDF) imefanya mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa maji safi na salama nchini Tanzania.

Kwa kushirikiana na Wizara ya Maji, MDF imechimba visima katika vijiji mbalimbali, na kuboresha upatikanaji wa maji na salama kwa zaidi ya watu 11,350.

Mwaka 2023 pekee, taasisi hiyo ilichimba visima 18 na kukarabati mingine vinne, hivyo kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa jamii za vijijini unakuwa endelevu.

MDF inatarajia kuchimba visima 50 zaidi na kukarabati vingine 50 na kunufaisha Watanzania 15,000 zaidi.

Kama Mbunge wa Singida kuanzia 2005 hadi 2015, MO aliboresha upatikanaji wa maji ambapo asilimia ya wakazi waliopata maji safi iliongezeka kutoka asilimia 27-28 hadi asilimia 86-88.
 
Jarida la Forbes (2025) limemtaja Mfanyabiashara wa Tanzania Mohamed Dewji, kuwa miongoni mwa watu matajiri duniani, akiwa na utajiri wa USD 2.2 bilioni sawa na Tsh 5.7 trillioni. Mo, anakuwa tajiri namba 12 Afrika na namba moja Afrika Mashariki kwa utajiri huo.

2. Orodha ya mwaka huu inaonyesha utajiri wa Mo Dewji umeongezeka na kufikia, dola bilioni 2.2 kutoka dola bilioni 1.8 mwaka jana.

3. Orodha ya Forbes ya matajiri wa Afrika kwa mwaka 2024 ilibainisha kuwa utajiri wa Mo Dewji umeongezeka kutoka dola bilioni 1.5 hadi bilioni 1.8.

4. Licha ya utajiri huo, MO Dewji kupitia kampuni ya Mohamed Entrprises Limited (MeTL) imezalisha ajira 40,000 kwa watanzania, kupitia biashara 126 zinazofanywa na kampuni hiyo.
5. Lengo la Mo Dewji ni kuongeza ajira hadi kufikia laki moja kwa watanzania na wana-Afrika Mashariki.

6. Mo Dewji kupitia MoDewji Foundation, imeshirikiana na serikali kupitia Wizara ya Maji, kuchimba visima, kukarabati na kutibu maji mkakati uliosaidia watu zaidi ya 15,000 kupata maji salama ya kunywa.

7. Utajiri wa Mo Dewji haikushia kwenye maji na afya pekee, umekwenda zaidi na kuwekeza katika tasnia ya michezo ambako ni sehemu ya mmiliki akiwekeza asilimia 49 kwenye klabu ya Simba. #MoDewjiNamba12 Africa.

Chanzo: Crown FM
Vp GSM???pamoja na kudhamini timu nane ligi ya NBC katoka kapa?
 
Ni vipi kuhusu kiwango cha mishahara anayolipa wafanyakazi wake na ongezeko la kodi anayolipa TRA baada ya utajiri wake kuongezeka, hao Forbes hawajagusia?
 
Jarida la Forbes (2025) limemtaja Mfanyabiashara wa Tanzania Mohamed Dewji, kuwa miongoni mwa watu matajiri duniani, akiwa na utajiri wa USD 2.2 bilioni sawa na Tsh 5.7 trillioni. Mo, anakuwa tajiri namba 12 Afrika na namba moja Afrika Mashariki kwa utajiri huo.

2. Orodha ya mwaka huu inaonyesha utajiri wa Mo Dewji umeongezeka na kufikia, dola bilioni 2.2 kutoka dola bilioni 1.8 mwaka jana.

3. Orodha ya Forbes ya matajiri wa Afrika kwa mwaka 2024 ilibainisha kuwa utajiri wa Mo Dewji umeongezeka kutoka dola bilioni 1.5 hadi bilioni 1.8.

4. Licha ya utajiri huo, MO Dewji kupitia kampuni ya Mohamed Entrprises Limited (MeTL) imezalisha ajira 40,000 kwa watanzania, kupitia biashara 126 zinazofanywa na kampuni hiyo.
5. Lengo la Mo Dewji ni kuongeza ajira hadi kufikia laki moja kwa watanzania na wana-Afrika Mashariki.

6. Mo Dewji kupitia MoDewji Foundation, imeshirikiana na serikali kupitia Wizara ya Maji, kuchimba visima, kukarabati na kutibu maji mkakati uliosaidia watu zaidi ya 15,000 kupata maji salama ya kunywa.

7. Utajiri wa Mo Dewji haikushia kwenye maji na afya pekee, umekwenda zaidi na kuwekeza katika tasnia ya michezo ambako ni sehemu ya mmiliki akiwekeza asilimia 49 kwenye klabu ya Simba. #MoDewjiNamba12 Africa.

Chanzo: Crown FM
Ubilionea wa upigaji na kufanya nchi iwe maskini siyo?
 
Back
Top Bottom