Mohamed Dewji kuinunua Simba

Mohamed Dewji kuinunua Simba

washabiki wenyewe ndio kuwaza hivi kila siku bora niendelee kuishabikia arsenal yangu tu
timu haiwezi kupangwa na wanywa kahawa na kucheza bao siku nzima halafu ikapata kombe la afrika

Mpira wa bongo umenishinda

Kila la heri na Arsenal yako.. Tuachie timu yetu.
 
Simba na Yanga haziendelei kwa sababu ya kumilikiwa na wanachama

Wanaamini uchawi kuliko kucheza mpira..
Imagine Simba inamilikiwa na Mo, Yanga na Manji, Azam na Azam mwenyewe, hapo lazima tambo ziwe nyingi na timu hizi zitafika mbali sana maana wote matajiri, hata wadhamini itawabidi waongeze hela maana kila timu itakuwa na uwanja wake....
Fan base itaongezeka zaidi...
Napenda hizi timu ziwe binafsi kumilikiwa na mashabiki ndio maana hata Arsenal haijafika mbali
 
weka mfumo wa hisa, asilimia 51 mmpe mfanyabiashara mkubwa anayeweza kuendesha timu kibiashara na wanachama wachukue 49 waachane na mfumo wa kizamani.

hata wao wenyewe wanachama wanaweza kuangalia kama wanaweza kuiendesha wenyewe kwa kuchanga kuwekeza na kuanza kutegemea kupata faida za kiburudani na kifedha sio lazima wauze. the way forward ni kuendesha timu kibiashara.
 
ile timu yake ya singida ilimshinda nini??

Umenikumbusha kuna striker wake alikuwa anaitwa Kipanya Malapa. Simba na Yanga zina advantage ya kuwa na fanbase kubwa lakini viongozi wake wameshindwa kabisa kutumia hiyo opportunity
 
Ni wazo zuri.. But tunatakiwa kulipitia kwa kina mana tusije tukawa tunampa mbu kazi ya kutibu malaria.

Mpeni tu maana wanasema mchawi mpe mwao amlee. Siyo huyo aliwahi kununua Mbagala Market ikamshinda? Mwenzie Azam kayakimbia hayo hayo!
 
Simba na Yanga sio kampuni. Ni vilabu. Wajuzi wa biashara mnijuze. Anaununua Simba kwa nani? Aveva sio mmiliki ni mali ya wanachama wote wa Simba.

Nadhani hatua ya kwanza ni kuifanya iwe kampuni kwanza. Hapo ndiyo kwenye "issue" yenyewe. Wanachama watakubali? Wale makomandoo ambao Yanga na Simba ndiyo zinawaweka mjini watakubali?
 
Wanaamini uchawi kuliko kucheza mpira..
Imagine Simba inamilikiwa na Mo, Yanga na Manji, Azam na Azam mwenyewe, hapo lazima tambo ziwe nyingi na timu hizi zitafika mbali sana maana wote matajiri, hata wadhamini itawabidi waongeze hela maana kila timu itakuwa na uwanja wake....
Fan base itaongezeka zaidi...
Napenda hizi timu ziwe binafsi kumilikiwa na mashabiki ndio maana hata Arsenal haijafika mbali

Hatua hiyo itafikiwa tu ikiwa club hizo zitakuwa kampuni kwanza. Mtihani uko hapo. Ziwe kampuni ili wamiliki hisa wajulikane.
 
Wanaamini uchawi kuliko kucheza mpira..
Imagine Simba inamilikiwa na Mo, Yanga na Manji, Azam na Azam mwenyewe, hapo lazima tambo ziwe nyingi na timu hizi zitafika mbali sana maana wote matajiri, hata wadhamini itawabidi waongeze hela maana kila timu itakuwa na uwanja wake....
Fan base itaongezeka zaidi...
Napenda hizi timu ziwe binafsi kumilikiwa na mashabiki ndio maana hata Arsenal haijafika mbali

Sio lazima zinunuliwe na watu binafsi, wakipatikana viongozi ambao wakatoa elimu na mikakati mizuri kwa wanachama kuhusu uendeshaji wa kisasa.Kwa idadi ya watanzania naamini Simba/Yanga haziwezi kosa wapenzi milioni 5 kila timu
 
kama mo anataka kuendeleza mpira si lazima anunue simba amwige bakhresa kwani ingawa ni mnazi mkubwa wa simba lakini kaanzisha timu yake sio aichukue simba
 
Mkuu Simba na Yanga ni kama ilivyo CCM vile au dini/imani...

Kuna waswahili waswahili wamejaa kwenye hivi vilabu hawataki kusikia kabisa mabadiliko...

Mathalani kumbuka kilichotokea kwa Yanga wakati ule wa uongozi wa Abbas Tarimba na maono yake ya kuifanya Yanga kuwa taasisi...

Mi naona ifike wakati hizi timu Simba na Yanga zimilikiwe na mtu binafsi ili maamuzi ya haraka yafanyike...
Mambo ya kusikiliza kila tawi yashapita
 
Uchambuzi wa tajiri umeenda shule...hofu yangu ni kwa makomandoo
na wazee wa kamati ya ufundi wa simba tu kama wataafikiana na mnene huyo.
 
weka mfumo wa hisa, asilimia 51 mmpe mfanyabiashara mkubwa anayeweza kuendesha timu kibiashara na wanachama wachukue 49 waachane na mfumo wa kizamani.

hata wao wenyewe wanachama wanaweza kuangalia kama wanaweza kuiendesha wenyewe kwa kuchanga kuwekeza na kuanza kutegemea kupata faida za kiburudani na kifedha sio lazima wauze. the way forward ni kuendesha timu kibiashara.

bila ku adopt mfumo anaopendekeza mo Mpira wetu hautakaa uendelee
 
Huo ndo mfumo kwa sasa ambao hata vilabu vya ulaya vinaenenda nao tusitegemee ujenzi wa kiwanja cha kisasa cha mpira kama club iko chini ya wanachama,mashabiki wanachotaka ni burudani,vikombe na historia nzuri ya club hivi itasaidia nini kama bado iko chini ya wanachama na bado tunafungwa na hamna makombe kama atafaidika na sisi tunachukua makombe better anunue club,ila kwa jinsi watu wasivyopenda kubadilika tutakataa,ila huo ndo ukweli sisi mashabiki hatufaidiki chochote zaidi ya burudani na vikombe na historia nzuri ya club
 
unajua hata yeye anaangalia mambo mawili, anaangalia simba kama mtaji na anaangalia mpira kama biashara ya kumpatia faida.

simba ina wanachama ambao kama wanaona wanaweza kuchanga kiasi kikubwa cha fedha kwa kuthamanisha thamani ya simba kwa sasa na kuamua kuongeza thamani ya clabu yao kwa kutengeneza hisa na kuuza hisa. wanaweza kupata fedha nyingi zaidi pengine za mtaji kwa kuwa na wanachama wengi lakini hakuna mtu mmoja ambaye anamiriki timu na wakaunda bodi ya kuendesha timu yao kibiashara. tatizo kubwa ni watanzania ufisadi ndio njia kuu yetu ya uchumi na hivyo popote wanachama wanapochanga michango na kuwakabidhi watu ni mara chache michango hiyo kutumiwa kwa tija kwani sisi utamaduni wetu ni kula mbegu badala ya kupanda na kufaidi mazao.

pengine mtu mmoja kuwekeza na akawa na sauti ya kusimamia maslahi yake inaweza kuwa njia sahihi ya kunusuru timu.

bila ku adopt mfumo anaopendekeza mo Mpira wetu hautakaa uendelee
 
Kuna vile vizee vinasema vilibeba matofali kujenga yale majengo,havikubali kitu kwani vitakufa njaa.

Sijui vinataka wote tungezaliwa zamani ili tushauri mazuri
 
Kama simba watagoma timu isiuzwe basi wajianda kufa
 
Back
Top Bottom