Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama


Hivi hapo umeandika nini haswaaa?
Naona wengi mmeumia kwa yeye kurudi mzima.
 
Serikali acheni usanii,MO kapatikana well and good, lakini mtueleze mlikomtoa.haiwezekani anarudishwa gimkana bila mapoliccm kukamata gari ilomrudisha tena saa kumi usiku, na simu alopiga kwa familia ni ya nani, na mapoliccm walitoka wapi saa kumi hyo na wasiweze kuwakamata walomleta.
Acheni usanii watanzania syo mabwege na mazuzu kihivyo
 

Matumaini yangu mimi ni kuwa awe amepatikana kwa sababu ya kazi za polisi na usalama na siyo ransom. Maana kama ni ransom itaacha maswali mengi zaidi na ya hatari zaidi. Lakini zaidi ni kuwa kama alitekwa na wahalifu na watu hao wakaweza kumuachia (kwa ransom au vinginevyo) na wakatoweka bila kukutana na mkono wa dola ni jambo baya zaidi na linaloacha maswali mengi zaidi. Hoja siyo tu kupatikana kwa Mo bali pia kuhakikisha waliofanya kitendo hiki hawabakii salama.

Nilichokiona hata kwenye video hii ndogo ni kuwa Mo was broken; aliteswa na sababu yake haijawa wazi. Akiambiwa avue shati lake sidhani kama watu watapenda watakachokiona.. my fifty cents.
 
Ukiliona gari hilo toa taarifa.
 
Hawa jamaa wamemfanya ni kijana wetu hadi anashindwa hata kumtizama siro usoni? Kumbe unaweza kuwa tajiri ukfanywa chochote!
 
hahaa tunashukuru Ubalozi wa Marekani kwa kuwakaalia kooni bila ya hivyo wasingemuachia kirahisi..eti ile gari alionyesha IGP Ziro ndio imetelekweza Gymkhana..Yaani watekaji wamerejesha gari na MO.
Narudia IQ za wanaopanga hizi sinema zipo chini sana
 
#BREAKING Kwa mujibu wa Waziri January Makamba, Mfanyabiashara Mohammed Dewji amepatikana, “Nimemuona na kuongea kwa kirefu na Mohammed Dewji, ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni, mnamo saa nane usiku Watekaji waliamua kumtupa kwenye maeneo ya viwanja vya Gymkana, naamini Polisi watatoa taarifa za ziada kuhusu kilichojiri” -
 
Naona ndio umeamka mkuu nenda kanawe kwanza uso upige na mswaki
 
Mambosasa: Taarifa siku ya tukio,waliomteka Mo ni wazungu wawili

IGP: waliomteka Mo walikuwa na gari la nchi jirani ila hakulitaja,ila wataalamu wa kufuatilia lile gari walisema ni la Msumbiji

Mo amepatikana Dar es salaam lakin si Msumbiji, wala Afrika Kusini


Baada ya kupatikana:Mambosasa: waliomteka Mo walikuwa wasouth Afrika ,walikuwa wanaongea kilugha

Unaweza ukajiuliza maswali hapa ,kichwa kikaota upara bila kupenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…