Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Wote waliowahi kutekwa na kupatikana wakiwa hai hakuna aliyethubutu kufunguka ukweli wa nn alichotendwa, alichoambiwa au sababu ya kutekwa…
Sasa leo MO kaja na hii ya LUGHA NA LAFUDHI YA SOUTH AFRICA….
je, tuamini kwamba watekaji ni walewale wamekuja na mbinu tofauti ili kulinda kauli ile ya WATEKAJI NI WAZUNGU?
Gari iliendeshwa kasi kwa dk 15 tu then akaingizwa kwenye chumba…!!!!???
Na gari ileile iliyomteka ndio ilomtupa uwanja wa Gymkhana…!!!???
Kwhiyo hiyo gari bado ipo ndani ya Dar na makachero wapo wanapambana kuitafuta… hahahahahaha

Hivi hapo umeandika nini haswaaa?
Naona wengi mmeumia kwa yeye kurudi mzima.
 
Serikali acheni usanii,MO kapatikana well and good, lakini mtueleze mlikomtoa.haiwezekani anarudishwa gimkana bila mapoliccm kukamata gari ilomrudisha tena saa kumi usiku, na simu alopiga kwa familia ni ya nani, na mapoliccm walitoka wapi saa kumi hyo na wasiweze kuwakamata walomleta.
Acheni usanii watanzania syo mabwege na mazuzu kihivyo
 
Hii inaonyesha familia wamelipa ransom!

Moja ya masharti ya ransom ni kutozungumza kuhusu tukio lote!

Kama atazungumza kuhusu yaliyomsibu mpaka akarudi basi hiyo itaonyesha kuwa hakulipa ransom na hakuna makubaliano.

Hoja iliyopo mbele yetu kwa sasa, Je, kama amelipa ransom, nini kwa sasa nafasi ya matajiri nchini kuhusiana na usalama wao kwa sababu kulipa ransom ni kufungua mlango wa biashara ya kidnapping and ransom nchini kwa matajiri.

Kosa la kulipa ransom baada ya kutekwa ambalo nchi za kusini mwa Afrika kama Afrika Kusini na Msumbiji walilianza kwa matajiri ndilo kwa sasa linazidi kuwatafuta kwa kasi zaidi.

Je, kuna uwezekano na Tanzania tukaelekea ambako nchi za kusini mwa Afrika ziliko kwenye biashara ya kidnapping and ransom?

Matumaini yangu mimi ni kuwa awe amepatikana kwa sababu ya kazi za polisi na usalama na siyo ransom. Maana kama ni ransom itaacha maswali mengi zaidi na ya hatari zaidi. Lakini zaidi ni kuwa kama alitekwa na wahalifu na watu hao wakaweza kumuachia (kwa ransom au vinginevyo) na wakatoweka bila kukutana na mkono wa dola ni jambo baya zaidi na linaloacha maswali mengi zaidi. Hoja siyo tu kupatikana kwa Mo bali pia kuhakikisha waliofanya kitendo hiki hawabakii salama.

Nilichokiona hata kwenye video hii ndogo ni kuwa Mo was broken; aliteswa na sababu yake haijawa wazi. Akiambiwa avue shati lake sidhani kama watu watapenda watakachokiona.. my fifty cents.
 
Wote waliowahi kutekwa na kupatikana wakiwa hai hakuna aliyethubutu kufunguka ukweli wa nn alichotendwa, alichoambiwa au sababu ya kutekwa…
Sasa leo MO kaja na hii ya LUGHA NA LAFUDHI YA SOUTH AFRICA….
je, tuamini kwamba watekaji ni walewale wamekuja na mbinu tofauti ili kulinda kauli ile ya WATEKAJI NI WAZUNGU?
Gari iliendeshwa kasi kwa dk 15 tu then akaingizwa kwenye chumba…!!!!???
Na gari ileile iliyomteka ndio ilomtupa uwanja wa Gymkhana…!!!???
Kwhiyo hiyo gari bado ipo ndani ya Dar na makachero wapo wanapambana kuitafuta… hahahahahaha
Ukiliona gari hilo toa taarifa.
 
MFANYABIASHARA MAARUFU MOHAMMED DEWJI APATIKANA AKIWA HAI

Amepatikana akiwa ametupwa kwenye viwanja vya Gymkhana

Baada ya kutekwa Gari ya watekaji iliendeshwa kwa kasi sana na kwenda kuwekwa kwenye chumba akiwa amefunikwa uso

Asema watekaji walikuwa wakiongea lugha inayoonekana kuwa ni ya Afrika Kusini

View attachment 904322
View attachment 904323

Hawa jamaa wamemfanya ni kijana wetu hadi anashindwa hata kumtizama siro usoni? Kumbe unaweza kuwa tajiri ukfanywa chochote!
 
hahaa tunashukuru Ubalozi wa Marekani kwa kuwakaalia kooni bila ya hivyo wasingemuachia kirahisi..eti ile gari alionyesha IGP Ziro ndio imetelekweza Gymkhana..Yaani watekaji wamerejesha gari na MO.
Narudia IQ za wanaopanga hizi sinema zipo chini sana
 
#BREAKING Kwa mujibu wa Waziri January Makamba, Mfanyabiashara Mohammed Dewji amepatikana, “Nimemuona na kuongea kwa kirefu na Mohammed Dewji, ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni, mnamo saa nane usiku Watekaji waliamua kumtupa kwenye maeneo ya viwanja vya Gymkana, naamini Polisi watatoa taarifa za ziada kuhusu kilichojiri” -
 
Naona ndio umeamka mkuu nenda kanawe kwanza uso upige na mswaki
 
Mambosasa: Taarifa siku ya tukio,waliomteka Mo ni wazungu wawili

IGP: waliomteka Mo walikuwa na gari la nchi jirani ila hakulitaja,ila wataalamu wa kufuatilia lile gari walisema ni la Msumbiji

Mo amepatikana Dar es salaam lakin si Msumbiji, wala Afrika Kusini

Baada ya kupatikana:Mambosasa: waliomteka Mo walikuwa wasouth Afrika ,walikuwa wanaongea kilugha

Unaweza ukajiuliza maswali hapa ,kichwa kikaota upara bila kupenda
 
Back
Top Bottom