Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

"Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga. kama suala la kutekwa kwa Mohamed Dewji linaacha maswali. Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa"- Rais John Magufuli

Hahahahaha lol! MO alitekwa tangu October hukutia neno lolote kwa miezi mitano sasa ghafla tu unaibuka na kudai uchunguzi?????

Vipi uchunguzi kuhusu lissu, Saanane, Azory? Vipi uchunguzi kuhusu 2.4 trillions? Vipi miili iliyookotwa ufukweni?
 
Inafikirisha sana hii nchi!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ni miaka 5 sasa toka huyu mwamba atekwe na wala watekaji serikali haijawapata wala Mo mwenyewe hajawi wafahamu [emoji23] walio mteka.

Binafsi namuelewa Mo kuamua kupotezea ili focus yake iendelee kwenye biashara zake.

Ila ule ulikuwa uhuni katika historia yake na watu wa staarabu.
Pole sana Mo, tunashukuru kwa imani yako kuendelea kuwepo Tanzania. Wengine waliamua kusepa kabisa.
 
MFANYABIASHARA MAARUFU MOHAMMED DEWJI APATIKANA AKIWA HAI

Amepatikana akiwa ametelekezwa kwenye viwanja vya Gymkhana

Baada ya kutekwa, Gari la watekaji liliendeshwa kwa kasi sana na kwenda kuwekwa kwenye chumba akiwa amefunikwa uso

Inasemakana watekaji walikuwa wakiongea lugha inayoonekana kuwa ni ya Afrika Kusini'

Tanzania, Mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ aliyetekwa Oktoba 11 na kupatikana leo Jumamosi Oktoba 20, 2018 saa nane usiku baada ya waliomteka kumtupa katika Viwanja vya Gymkhana katikati yajijini la Dar es Salaam.

Habari zaidi soma=>Dar: Mfanyabiashara Mohammed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay - JamiiForums

=======

“Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama.” — Mohammed Dewji (Saa 9:15 alfajiri, Dar es Salaam)

“I thank Allah that I have returned home safely. I thank all my fellow Tanzanians, and everyone around the world for their prayers. I thank the authorities of Tanzania, including the Police Force for working for my safe return.”
— Mohammed Dewji (3:15AM, Dar es Salaam)

View attachment 904322
View attachment 904323

Wala haikuwahi kujulikana hao walioongea kingoni cha madiba walikuwa wanataka nini[emoji23][emoji23].

Tulipitia mengi sana kama taifa. Ilikuwa hakuna kupoa.
 
Wala haikuwahi kujulikana hao walioongea kingoni cha madiba walikuwa wanataka nini[emoji23][emoji23].

Tulipitia mengi sana kama taifa. Ilikuwa hakuna kupoa.
Ukiangalia hiyo staged press Mo aliyotengenezewa aishukuru serikali ya dikteta uchwara unaona kabisa body language yake inamsaliti anapopeana mikono na Muliro.

Unajua kabisa hapo waliomteka anawafahamu.
images - 2024-08-19T132010.103.jpeg
 
Wamemteka Billionaire!?! Wasiojulikana wamejichanga.

2019 kitawaka sana, watu wengi waliohusika na hii watadakwa. Hapo ndiyo tutaona nguvu ya pesa.

Mi ninachojua hawa watu wanajua haki zao na hawatokubali kuonewa, sisi wa hali ya chini tunajisikia raha tukionewa huku tukisema ni uzalendo. Ukiitwa mnyonge unajisikia raha
 
Back
Top Bottom