Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Anamshukuru "rais" mimi namuuliza "kwa lipi alilokufanyia hali ya kuwa alikuwa anagonga juice na wanandinga pale mjengoni?
Sikumsikia akitamka lolote kutekwa kwako!
Tafadhali sana MO tupe maelezo in a free style mode.
Ulitaka rais ndo atoke ikulu kwenda kumtafuta mo, mawazo mengine muwe mnapeleka facebook sio huku kwa great thinkers
 
Kina maria sarungi wame tweet mpaka baasi!
Wakipaaza sauti "BRING BACK MO" kina TL wameandika mpaka makala!
Zitto Rugaya amepambana mno!
G. Lema kawaita waandishi wa habari kutoa njia mbadala ya kumpata MO!

Mshana Jr akatoa ma conspiracy theory ya abc za utekaji na malengoye!
Pascal Mayalla alishusha nondo hatari! Hii yote ni katika kushinikiza MO apatikane.
IWEJE AMSHUKURU Rais ambaye hatuna ushahidi wa kuguswa kwake na tukio la utekaji?
Kati ya hao kuna hata mmoja aliyechukua hatua za kwenda kumtafuta mo, kama hakuna hizo sauti zilizopazwa sijui makala zimeandikwa hazina tofauti na kasuku anavyoiga sauti za vitu mbalimbali. Yaan hazina maana yyt
 
Haya na huyo Tundu Lissu?!tundu lissu kashabuliwa kwa nia ya kuuwawa alishawahi hata kwenda kumuangalia.
 
Mtu tangia lini anapatikana kwa ku tweet?
Rais ndi mkuu wa majeshi yote nchini na yeye ndio kila kitu yeye ndio ana saidia na kuwezesha vyombo vya ulinzi.
Rais alikuwa ana wasiliana na Familia ya Mo si mpaka atoe tamko kama ninyi
hahahaha Mmeumia Rais kushukuriwa hahahaha imewachomaaaa
Hata BBC news ime confirm kuwa katika nchi masikini tajiri aliyeajiri watu karibu 23,000 wakipaza sauti wote watekaji watapata pressure.
 
Mapolisi hawa watengwe kwa ajili ya uchaguzi aaj8ri wengine kwa ajili ya usalama na mali zao.
 
Mtu tangia lini anapatikana kwa ku tweet?
Rais ndi mkuu wa majeshi yote nchini na yeye ndio kila kitu yeye ndio ana saidia na kuwezesha vyombo vya ulinzi.
Rais alikuwa ana wasiliana na Familia ya Mo si mpaka atoe tamko kama ninyi
hahahaha Mmeumia Rais kushukuriwa hahahaha imewachomaaaa
ndugu, amka usingizini.

vyombo vya ulinzi vinawezeshwa na kodi zako, zangu na za wanakijiji wenzangu hapa Mporoto. siyo rais!
 
Wakati mwingine tuwe tunatumia akili kidogo, Mohamed Dewji kawashukuru waliomteka kwa kuamua kumuachia usiku wa manane wakati tuliokuwa tukisikitika, tuliokuwa tukiomba, tuliokuwa tukiliaa na tuliokuwa tukipiga makelele tumelala. Mohamed Dewji hana muda wa kuwashukuru binadamu wanyonge kama sisi tulioumbwa kwa udongo.

Sala zetu, vilio vyetu na makelele yetu hayakuweza kufanikisha kupatikana kwa Ben Saanane, Azory na ndugu zetu lukuki waliopotea...iweje kwa Mohamed Dewji? Maombi yetu, masikitiko yetu na vilio vyetu havikuwezesha kupatikana kwa waliommiminia risasi zisizo na hesabu Mbunge wa Singida Mh. Tundu Antiphas Lissu kwa nia ya kumuua.

Mohamed Dewji hana haja ya kutushukuru wala asithubutu kutushukuru, awashukuru watekaji wenye roho nzuri waliomuonea huruma hadi kapatikana mzima wa afya bila hata kuhitaji uchunguzi wa afya yake, nashauri familia yake iwape hao watekaji zile trilioni kama asante...Tanzania ni zaidi ya tunavyoijua, pole sana Mohamed Dewji!
 
Kwanza lazima amshukuru Raisi maana ndio Amiri jeshi mkuu na ndie mtoa order wa mwisho akisema Fatilieni jambo lazima mfatilie akisema msifatilie bas mnauchuna so kwa userious wa polisi Ni lazima Raisi alitoa maagizo ya kukubali ufatiliaji ufanyike tena kwa haraka iwezekanavyo.

So kumshukuru raisi kwa MO ni muhimu na LAZIMA sio OMBI.

Mtu alitekwa sidhan kama anaweza kuwa na ujasiri wakuanza ongea na kuonyesha uso kwa raha gani alokua anaipata?? hapo yenyewe kaongea BASI tuu kwasababu Serikali ilihakikisha inapambana kumpata so kwa ubinadamu wake akaona si vyema kwenda nyumban direct Acha aje ATOE hata shukurani tu so hapo pakusema eti alificha uso sababu alikua anaogopa kitu HAPANA.

Aliyemteka MO si polisi wala si nani ila anaemjua Alomteka mpk sasa ni yeye mwenyewe MO tuache kushuku shuku kwetu na kuropoka ropoka.

Gari mlilikataaa na kapatkana na gari lile lile sasa sijui ni watu gani nyie msio hata na aibu mkanyamaza kidogo maana kama kuumbuka mmeumbuka pakubwa,tuachie fani za watu wengine tubaki mashabiki tu.
 
Ulitaka MO amtaje Zitto au Lema wakati walikuwa wanajineemesha kisiasa?
Mpango wenu wa kuuza tisheti umebuma.
 
Kwani yule Roma Mkatoliki alipopatikana alisema chochote vile au?
 
Wakati mwingine tuwe tunatumia akili kidogo, Mohamed Dewji kawashukuru waliomteka kwa kuamua kumuachia usiku wa manane wakati tuliokuwa tukisikitika, tuliokuwa tukiomba, tuliokuwa tukiliaa na tuliokuwa tukipiga makelele tumelala. Mohamed Dewji hana muda wa kuwashukuru binadamu wanyonge kama sisi tulioumbwa kwa udongo.

Sala zetu, vilio vyetu na makelele yetu hayakuweza kufanikisha kupatikana kwa Ben Saanane, Azory na ndugu zetu lukuki waliopotea...iweje kwa Mohamed Dewji? Maombi yetu, masikitiko yetu na vilio vyetu havikuwezesha kupatikana kwa waliommiminia risasi zisizo na hesabu aliyekuwa Mbunge wa Singida Mh. Tundu Antiphas Lissu.

Mohamed Dewji hana haja ya kutushukuru wala asithubutu kutushukuru, awashukuru watekaji wenye roho nzuri waliomuonea huruma hadi kapatikana mzima wa afya bila hata kuhitaji uchunguzi wa afya yake, nashauri familia yake iwape hao watekaji zile trilioni kama asante...Tanzania ni zaidi ya tunavyoijua, pole sana Mohamed Dewji!
Mkuu Mag 3 hata
mimi pia naunga mkono hoja,
P
 
aliyekuwa Mbunge wa Singida Mh. Tundu Antiphas Lissu.

Mkuu Mag3.

Hilo neno hapo juu nililolipigia mstari, halifai kuwepo hapo maana TL bado ni Mbunge. Hilo neno linamaanisha kuwa aliwahi kuwa mbunge na sasa sio mbunge.

Litoe au weka neno lingine hapo
 
Asante sana Mwifwa, nitarekebisha.
 
Back
Top Bottom