Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Inaelekea kile chombo kilichoripotiwa na nyumbu kikizamia bahari ya Hindi kilipats pancha imebidi wamrudishe tu.Ila IGP sasa mjifunze , kutoa taarifa za upelelezi inasaidia, sasa lile gari halina mwenyewe nalo,litatelekezwa parking ya NSSF.
 
Mo akiitisha Press Conference itavamiwa bila ya taarifa na Mwakiyembe ambae ndie atakuwa msemaji mkuu kama alivyofanya kwa ROMAAA.... HAHAAAA. awamu hiiii
Ameshapangwa.
Hawezi kuitisha.
Ukweli utajulikana baada ya huyu msukuma na makonda wake kuondoka madarakani
 
Mambosasa: Taarifa siku ya tukio,waliomteka Mo ni wazungu wawili

IGP: waliomteka Mo walikuwa na gari la nchi jirani ila hakulitaja,ila wataalamu wa kufuatilia lile gari walisema ni la Msumbiji

Mo amepatikana Dar es salaam lakin si Msumbiji, wala Afrika Kusini


Baada ya kupatikana:Mambosasa: waliomteka Mo walikuwa wasouth Afrika ,walikuwa wanaongea kilugha

Unaweza ukajiuliza maswali hapa ,kichwa kikaota upara bila kupenda
Migambo wanaruka na kukanyagana hahahaha hata asiye na akili ashang'amua game lote lilikuweje, producer mshamba kweli na mkizidi kumfuata mtaaibika maana nyie ndo washika vipaza sauti kusafisha utumbo wote
 
Uzima ndio kila kitu mengine ya binadamu unamuachia alieumba mbingu na nchi.
 
kwa mujibu wa maelezo ya Geshi la Porisi jamaa alitekwa na wazungu wanaoongea kizulu/xhosa.
 
Ni upepo na pia aliyetekwa ni tofauti kabisa na kina ben saanane. No offense to them, na wao ni binadamu ila tuwe wakweli, Mo ni ligi nyingine. Mtekaji lazima uwe na hofu maana nchi nzima ilisimama na dunia pia ilimulika.
 
MFANYABIASHARA MAARUFU MOHAMMED DEWJI APATIKANA AKIWA HAI

Amepatikana akiwa ametupwa kwenye viwanja vya Gymkhana

Baada ya kutekwa, Gari la watekaji liliendeshwa kwa kasi sana na kwenda kuwekwa kwenye chumba akiwa amefunikwa uso

Inasemakana watekaji walikuwa wakiongea lugha inayoonekana kuwa ni ya Afrika Kusini

View attachment 904322
View attachment 904323





Cinema imamalizika. Nawaza tu kwa sauti kwamba huenda MO atakuwa ameachia sehemu kubwa sana ya ukwasi wake (fedha na assets) kwa watekaji. Na midomo yao imefungwa kwa bandeji ya chuma, hakuna kukohoa. Pole sana MO na familia yako kwa ujumla. Jambo jingine ambalo haliingii akilini ni hii staili ya familia ya kwenda kumchukua MO. Yaani kweli mtu ametekwa wiki nzima halafu unapigiwa simu kwamba amepatikana, then wewe unawasha gari moja kwa moja kwenda kumchukua kama vile unaenda kuchukua mzigo tu mzigo flani. Yaani unajiamini nini kwenda kumchukua mtu aliyekuwa ametekwa na majambazi bila kuongozana na ulinzi wowote?. Hapo kuna mawili ama alikuwa ameshahakikishiwa usalama ama walichanganyikiwa kusikia hizo habari na kusahau kila kitu, hahahaaa!. Maamuzi ya zimamoto ndio shida yake, hakuna muda wa kujipanga kuweka vizuri mazingira. Hahaaaa
 
Taarifa zilizotufikia asubui ya leo ni kupatikana kwa Mo Dewji. Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kupatikana kwake akiwa hai na salama salimini. Swali langu kwa wataalamu wa mambo. Je? jeshi la polisi litamchukua tena Mo kwa ajili ya uchunguzi zaidi au litamuacha apumzike na aendelee na shughuli zake za kawaida?

Sababu ya swali hili ni kutokana na maswali mengi yasiyokua na majibu yaliyo sababisha na taarifa ya vyombo vya dola katika tukio hili. Tukianza na Wazungu wawili, CCTV inayotembea kufuata gari, taarifa za kupatikana kisha kufutwa ghafla, gari la msumbuji na maswali mengine kedekede. Ambayo kwa namna fulani hayawezi kupingana na mawazo ya wengi juu ya uhusika wa serikali katika tukio hili.

Je tutegemee polisi kumtwaa tena Mo kwa siku kadhaa kwa uchunguzi zaidi? au tukio hili ni kubwa kidogo kwao hivyo watampotezea na maisha yaendelee tu?

Maoni binafsi:
Mo hata hasipotueleza nani walimteka fresh tu, maana hata wao watekaji wanajua tunawajua
Debriefing ni lazima.
 
tunamshukuru amepatikana. hawa watekaji ni walewale waliomteka Roma mkatoliki. staili ileile...
 
Walishazoe pepo za kuvuma kutoka kusini kwenda kaskazini n.k ila huu upepo ulikuwa haueleweki ukawachanganya.
 
Mpuuzi sana na uvivu wako wako, imbecile walahi
Gari iliyomteka MO imepita kituo cha salenda ikapita jengo la UWT ikakatiza Agakhan ikapita kituo cha polisi cha agakhan ikenda kumtupa gymkhana na wakaliacha gari hapo hapo na hao WAZUNGU wanaoongea KIZULU wanaotokea MSUMBIJI wakatokomea halafu mnasema nchi ina ulinzi wa kutosha na mpo vizuri.
 
Kama kweli jeshi la polisi limefanikisha upatikanaji wake basi wahalifu wafikishwe mahakamani au la tuaamini vyombo vya usalama vimeanza biashara ya utekaji na ransom.
Jesh halijafanikisha kupatikana kwake amerud mwenyewe kutoka huko alikokwenda kutafuta maisha ful stop[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mambosasa: Taarifa siku ya tukio,waliomteka Mo ni wazungu wawili

IGP: waliomteka Mo walikuwa na gari la nchi jirani ila hakulitaja,ila wataalamu wa kufuatilia lile gari walisema ni la Msumbiji

Mo amepatikana Dar es salaam lakin si Msumbiji, wala Afrika Kusini


Baada ya kupatikana:Mambosasa: waliomteka Mo walikuwa wasouth Afrika ,walikuwa wanaongea kilugha

Unaweza ukajiuliza maswali hapa ,kichwa kikaota upara bila kupenda
Kwa hiyo mtaalamu wa hayo masuala umeunganisha doti na kutoa kasoro! Unahitaji kuteuliwa kuwa Mkuu wa Chombo chochote cha Usalama nchini.

Masuala ya kipelelezi waachie wenyewe. Kuna kitu huitwa "disinformation" kumpoteza mtuhumiwa, au siyo.
 
Wanataka kutengeneza ajira za walinzi wa matajiri kwa vijana wetu waliomaliza JKT na hawajapata ajira
 
Back
Top Bottom