Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

walidokoa mboga jikoni (kwa wizi) wakalamba mchuzi.
walipoulizwa wakamaka......"no, no, hatukuiba nyama sisi!, tunamhisi jirani hapo nyumba ya pili".
jana sasa, wakajitokeza hadharani tena kusisitiza "hatukuiba sisi".
lakini walisahau kufuta mchuzi ulioganda kidevuni.
watu wakauliza "mbona kidevu kina mchuzi?".
wakajua wameumbuka.
leo wamerejesha nyama yote, waliaambulia kulamba mchuzi tu!!!

Mungu hataniwi!
 
Serikali hii inatumia vibaya yombo vya dola. Tuweke kumbukumbu ya ujinga huu na wakitoka madarakani tuwafunge tusitazame Katiba wanayoitumia vibaya . Kilichofanyika ni UHUNI wa kijinga . Hebu fikiria wananchi wangeingia barabarani ingekuwaje. Tuje tuwafunge kuanzia kiongozi MKUU hadi wasaidizi wake.
 
Ni upepo na pia aliyetekwa ni tofauti kabisa na kina ben saanane. No offense to them, na wao ni binadamu ila tuwe wakweli, Mo ni ligi nyingine. Mtekaji lazima uwe na hofu maana nchi nzima ilisimama na dunia pia ilimulika.
Hahaha aisee wayekaji wamevuna aibu ya karne kwenye hili maana tukio hili limewavua nguo kabisa na wameonesha wasivyo makin na mission zao za kipumbavu
 
Shukrani Polisi wetu kwa kazi nzuri.
Pongezi kwenu sana.
Tulimuhitaji MO na amepatikana basi.
Hamuwezi kuwafurahisha watu wote kwa wakati mmoja.
Mimi nimefurahi sana sana, maana nilihuzunika sana.
Watani Zetu wa Yanga mupooo, tunawashukuru sana kwa kutuunga mkono kwa huu mkasa wa Bosi wetu.
Kuanzia leo nitawaheshimu sana sana,
Siwacheki tena labda kama mkifungwa kwenye mechi zenu.
[emoji123] nguvu moja.
 
me naomba kujua jesh la polis alifanyi kaz ipasavyo.. jana igp sirro kaongea sana na gar lilohiska kumteka mo limeonesha mpka plate number na wamedai ni la nchi jiran hapo wamechunguza sna.. mpk hayo majibu tumepewa jana... haya ssa gari lilihusika kumbe sio ni gar la hapa hapa tz.. ndo tunatka kusema jeshi letu bdo sana kwenye uchunguz.. ila igp sirro aje tu tena aite waandsh wa habar ATUOMBE RADH WATANZANIA WOTE KWA KUTUDANGANYA NCHI NZIMA
 
Watanzania, ni makosa makubwa sana yalifanyika kuwapa nchi hawa MALIMBUKENI na WASHAMBA, hata mzee LUBUVA anajutia sana hilo kwa sasa.
Sina hakika kama mtaweza kuwatoa hawa kwa sanduku la kura pekee, maana watapita tu kwa MABAVU. Lakini historia itawahukumu.
 
Habarini za asubuhi wakuu..

Ni jambo la kumshukuru Mwebyezi MUNGU kwa kuwezesha ndugu vyetu kupatikana akiwa hai na salama..Lakini kwenye Hili saga kuna mambo machache nimejifunza/nimeyaona ambayo ningependa kushea na nyinyi..

1.Wananchi wengi hawana imani na Mfumo wa Usalama wa nchi.
Baada ya Mo kutekwa,sehemu kubwa ya wananchi(mfano humu JF) walikuwa wanadai kwamba SERIKALI inafahamu alipo(inahusika) kulingana na mlolongo wa matukio ya kupotea watu mbalimbali ktk awamu hii.

2.Baadhi ya viongozi ni wa Ajabu sana.
Watu wengi waliponda na kuwa disappointed kiongozi fulani aliposema eti watu wasizungumzie kupotea kwa MO maana wanawatia huzuni wanafamilia[emoji23][emoji23][emoji23]..it was funny(myb he had a strong point..but it sounded funny among most of people)

3.POLISI BWANA!!
Hapa sina cha kuongezea..maana hata mimi nilishangazwa na zile picha za "CCTV" zilizotolewa(unless niwe sikumwelewa kamanda)

Pili;Kamanda alitoa maelezo ya kujichanganya kuhusu watekaji..mara ni raia wa kigeni(wazungu)..mara ni wasouth africa walikuwa wanaongea kilugha..uts contradicting!! Ukijumlisha na picha zililizokuwa released jana zilipingwa kwa nguvu zote na watu wengi kwamba pale sio kwny ile hotel.
Pia kamanda aliogopa nini kusema hiyo gali ina namba za usajili za msumbiji!?? Kwanini aafichefiche eti ni "nchi jirani"???anaonesha kama anawaogopa hivi(conspiracy theory[emoji23])

Tatu watekaji walimtupa MO baada ya kumalizana nae so msijipe credits nyingi sanaaa mtaharibu.mmefanya kazi nzuri lakini.

Nne; kelele za wanasiasa na wannchi zimesaidia kupatikana kwa mo..huo ndo ukweli.

4.MWISHO.
Je Watekaji walikuwa wanataka nini!? Je itasemwa hadharani au itabaki kuwa siri(kama kina ishu ya kina Roma!!?)


Conclusion!!

Hizi habari za kutekana si nzuri zinaharibu sifa ya nchi na tunaonekana ni watu wa ajabuajabu..Tanzania ni nchi ya amani..tuitunze na tusupport vyombo vyetu vya usalama kwny kazi zao ili mambo yawe smooth.
Nice weekend everyone.

Kama Tz ina wachambuzi Kama wewe basi Kazi ipo.
 
Hii inaonyesha familia wamelipa ransom!

Moja ya masharti ya ransom ni kutozungumza kuhusu tukio lote!

Kama atazungumza kuhusu yaliyomsibu mpaka akarudi basi hiyo itaonyesha kuwa hakulipa ransom na hakuna makubaliano.

Hoja iliyopo mbele yetu kwa sasa, Je, kama amelipa ransom, nini kwa sasa nafasi ya matajiri nchini kuhusiana na usalama wao kwa sababu kulipa ransom ni kufungua mlango wa biashara ya kidnapping and ransom nchini kwa matajiri.

Kosa la kulipa ransom baada ya kutekwa ambalo nchi za kusini mwa Afrika kama Afrika Kusini na Msumbiji walilianza kwa matajiri ndilo kwa sasa linazidi kuwatafuta kwa kasi zaidi.

Je, kuna uwezekano na Tanzania tukaelekea ambako nchi za kusini mwa Afrika ziliko kwenye biashara ya kidnapping and ransom?
Muulize DAB na babake
 
Sisi tunaoenenda katika roho tunaiona hekima ya Mungu katika ujumbe wake. Tulifundishwa ya kuwa maneno yetu yasiwe mengi na tuwe watu wa kushukuru!
 
Ameona tz itawaka moto ,kaamuru watu wasiojulikana wamurudise salami salimini, lakini namushauri hivyo hivyo ahame tz kabisa
Tz hii hii ingewaka moto!? Kuwa serious basi,nani angeuwasha huo moto!? Kwa siku hizo saba alizokaa bila ya wawashaji moto kuwa na matumaini yoyote ulijaribu hata kidogo kuwasha moto?
 
Yaani kelele za Lema ziwe msingi wa kupatikana Dewji lakini kelele hizo hizo zisiweze kumleta Ben Saanane? You must be joking!

Nani mwenye uhusiano wa karibu kikazi na kimaisha kati ya Lema na Ben Saanene au Dewji?

Kumbuka Ben Saanane alikuwa mfanyakazi wa CHADEMA

Ulichofanya ni kutoa shukrani ambazo hazina hata ukweli kifikra!
By necessary implication, jana SIRO alijichanganya sana kiasi hata kichaa angelijua kuwa Mo amefichwa na SIRO, for that matter serikali! conscious ya "aliyemtuma" --by the way anajulikana, imemsuta na wakaamua wamuachie!
Lema alitoa nyongo akiwa ameshaamua kuwa maiti any time! Ile press yake ilikuwa very focused, precise and touching with accurate prediction who is likely to be the kidnapper!
 
Ma
Hahahaha ushamba wa jiwe utamcost siku moja

Cover story hapa itakuwa ni nini ? Maana hata mtoto mdogo anajua Mo alichukuliwa na kina nani .

Halafu watu wa aina hii ndio wakakae meza Moja na kina Prof Thontorn wa Barrick tutegemee kulipwa na Accasia matrilioni ??

Tutakesha tukisiburia hilo
Mawazo ya kitumwa.
 
Kinachowalinda hawa watu ni kwasababu wameshika dola.
Anayekulinda wewe na mali yako hata ukaweza kila mara kuandika humu JF ni nani? Au anayewalinda hao Mabwana zako, ambao kila kukicha hukimbilia kwenye vyombo vya habari kuilaumu Serikali, kama hufanyavyo humu JF, wakiwa huru na salama, ni nani?
 
Yaani Tanzania kuna watu wanamitindio ya ubongo, alipopotea walilalamika na kutukana, amepatikana wanalalamika na kutukana.

Daah
 
Back
Top Bottom