Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Wamebana wameachia, Jiwe siyo Mtu!.

Namshauri Mo asepe atulie zake huko Brunei au Kisiwa chochote cha Pasifiki ale bata miaka saba ipite kisha arudi tujenge nchi!, yeye bado kijana, kupumzika miaka saba siyo ishu!
huyo hawajamuachia Bure bure kunakitu wamepanga sasa ajichunge.
 
Chadema wamechukizwa mno na kupatikana kwa Mo maana kiki yao imebuma.

Shida na Matatizo yanayoipata Tanzania ndiyo ufahari wa Chadema!
mkuu suala hili la kutekwa mo litaisha kama watekaji watapatikana na kubaini pia mahali mo alipofichwa nje ya hapo bado kiki iko juu mno...
 
Tangu kutekwa kwa Mo Dewji, ni wapinzani kwa kushirikiana na watanzania wengine ndio waliokuwa wamesimama mstari wa mbele kupaza sauti kutaka MO apatikane huku watu wa upande fulani karibu wote wakiwa kimya zaidi ya ku-tweeet tu kusikitishwa na tukio hilo.

Mnaoshabikia upinzani ufe tukio hili liwafumbue macho na mjiulize ingekuwaje kama wote tungekuwa wa chama kimoja kama mnavyotaka.

Waliobuni mfumo wa vyama vingi hawakuwa wajinga hivyo na nyinyi mnaotaka turudi katika huo mfumo muache kuwa wajinga.

Lengo ni kuua upinzani ili kuwatawala watu kirahisi na kufanya chochote bila kupigwa kelele na kukemewa

Only in black continent.
 
Kuna jamaa katika utawala huu ukiwachinja kwa dua wanalika tu bila wasiwasi maana hawana tafauti na kitoweo kingine chochote kama mbuzi na kondoo
 
Dah.. Aisee yani wewe kila kitu ni kufagilia upinzani! Unatia kinyaa..

Kama unafikiri selikali ndio inahusika na imewaogopa hao wapinzani, mbona Ben bado hajarudi na kila siku mnapiga makelele?
 
Serikali yao ndio ilikuwa inamtafuta..wao ndio walikuwa wakifanya mazungumzo na familia ya mo mara kwa mara..ulitaka nao walalamike kama wafanyavyo majirani?? Si mngewacheka
 
Mo maneno yake ya Kwanza baada ya kuombwa aongee kidogo alisema "namshukuru Mungu kwa kuwa niko salama, pia namshukuru mh rais......."

Anamshukuru mh rais kwa kipi? Nimejiuliza maswali yasiyokuwa na majibu
Hahahaha, anamshukuru Rais kwa lipi? Maana wakati Sirro anatoa taarifa ikulu walikuwa wanahost taifa stars..., kuna hidden message hapo, lazima kuna sababu ya kumshukuru
 
ukisikiliza Kwa makini mambo sasa utagundua anatumia nguvu kubwa kuaminisha watanzania kuwa Mo walitekwa Na watu wasio kuwa Na utaifa wa Tanzania .mwanzo walisema wazungu Ila sasa wanasema ni watu wa South Africa tena wanaongea mather language. wanakazana kusema tunamshukulu MH RAISI.

Zitto kabwe Na watanzania wengi wapo sahihi wakisema kuwa wausika walijulikana mapema


Hauko makini.
Kasema neno MASHAKA yetu. Neno mashaka bado ni doubts yaani uhakika haupo mpaka uchunguzi ukamilike.
Pia wazungu wa wazawa wa afrika kusini wanaongea lugha za asili za afrika kusini vizuri sana. Mfamo ni yule mchekeshaji aliyeact muvi za bushman yule mzungu. Akiongea bila kumuona utasema ni mtu mweusi hivyo point yako hapa haina mashiko kabisa zaidi ni umetanguliza hisia na mawazo yako ulikuwa nayo kabla hata hajapatikana kuwa akipatokana utasema hivi.
 
Wanabodi,
Hii ni thread ya swali, nikipendekeza kwa kuuliza, maana siku hizi, ukiuliza kitu,, watu hawaonagi alama za kuuliza, wakadhani nimetoa statement.

Baada ya Mo kupatikana, baada ya juhudi kubwa sana za jeshi letu la polisi, baada ya ile ahadi ya motivation iliyopelekea hadi IGP kufanya press conference ya jana, hii imethibitisha kuwa kumbe Jeshi letu la polisi, linaweza, wala hatuhitaji wachunguzi wa nje. Jeshi letu la polisi sasa ndio linauwezo, au kama lilikuwa nao siku zote, then, likiamua, linaweza, ukijumlisha na ile ahadi ya motivation ya familia, bali limeweza kwa sababu, sasa ndio limeonyesha uwezo huo kwa kufanikisha Mo kupatikana akiwa mzima, salama uu salmini na bukheri wa Afya.

Sasa kwa vile familia tayari iliishatenga shilingi billion moja kwa atayefanikisha kupatikana kwa Mo, na waliofanikisha ni IGP Kamanda Sirro, na vijana wake, kwa ile Press Conference muhimu ya jana. Mimi Napendekeza hizo pesa apewe Kamanda Sirro na vijana wake, ili zitumike kuboresha jeshi letu la polisi nchini kwa kulijengea uwezo kuzuia matukio ya utekaji, kwa kuwa motivate, siku zote, mtu yoyote akitekwa au kushambuliwa na wasiojulikana, juhudi kama hizi za kumsaka MO, ikiwemo kuitisha press conference, zifanyike. Tena laiti kama tungelijua kabla namna ya kuwa motivate polisi wetu watimize wajibu wao, usikute hata Ben Saanane alipotoweka, tungejichanga tukatangaza dau, angepatikana,
Aliposhambuliwa Lissu, tungejichanga tukatangaza dau, wasiojulikana wale, wangepatikana, na alipopotea Azori Gwanda, sisi media tungejichanga tukatangaza dau, angepatikana, huwezi jua!, Bilioni moja jameni sii mchezo!.

Zamani tulizoea ahadi za motivation ni kwenye kutafutia kura tuu, lakini sasa, hata katika kutimiza wajibu!, tena naombeni msinielewe vibaya kwa hii hoja ya motivation, kwa the difference between Mo, Ben Saanane na Azori Gwanda ni status tuu, Mo ana motivational status iliyopelekea kuhangaikiwa kulikopelekea kupatikana.

Mungu Mkubwa, Pesa ndio kila kitu!, Mkono Mtupu Haulambwi!. Masikini Ben Saanane, masikini Azori Gwanda
Jumamosi Njema
P.
 
Familia ya bilionea Mohammed Dewji, imesimulia namna ambavyo kijana wao alivyoachiwa na watekaji usiku wa kuamkia leo.

Msemaji wa familia hiyo, Azziz Dewji ameviambia vyombo vya habari kuwa watekaji hao walimuachia huru bilionea huyo kijana majira ya saa 8 usiku, Oktoba 20.
Alieleza kuwa baada ya kumuachia, Mo Dewji alimpigia simu baba yake na kisha kurejea rasmi nyumbani kwao.
“Yuko hapa nyumbani tunamshukuru Mungu. Walimuachia majira ya saa nane na nusu usiku halafu yeye akapiga simu kwa baba yake,” alisema Azziz.

Aliongeza kuwa afya ya bilionea huyo ni nzuri kwa asilimia 100 na kwamba kama kuna tatizo litakuwa tatizo la kisaikolojia kutokana na kutekwa.

Aidha, alimshukuru Rais John Magufuli, vyombo vya usalama pamoja na wananchi kwa juhudi za kupatikana kwa mwanaye.

Mo alitekwa saa 11 alfajiri ya Oktoba 11 mwaka huu, katika hotel ya Colosseum iliyoko Oysterbay jijini Dar es Salaam, alipokwenda kufanya mazoezi.

Source: Dar 24
 
Kwahiyo hili nali litasababisha chadema kuishinda ccm hapo 2020?
 
Et Kelele Za Wapinzani.
Mbona Wengine Ni Kama Hawajarudi Bado.
 
Hahahaha ushamba wa jiwe utamcost siku moja

Cover story hapa itakuwa ni nini ? Maana hata mtoto mdogo anajua Mo alichukuliwa na kina nani .

Halafu watu wa aina hii ndio wakakae meza Moja na kina Prof Thontorn wa Barrick tutegemee kulipwa na Accasia matrilioni ??

Tutakesha tukisiburia hilo
Tukilipwa ntajinyea
 
Back
Top Bottom