Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Hapa nionacho, chadema na tawi lake la bavicha WAMEKASIRISHWA sana na kupatikana kwa Mo tena akiwa mzima wa afya maana watakosa tena tukio la kudandia.
 
Dah.. Aisee yani wewe kila kitu ni kufagilia upinzani! Unatia kinyaa..

Kama unafikiri selikali ndio inahusika na imewaogopa hao wapinzani, mbona Ben bado hajarudi na kila siku mnapiga makelele?
Mnatia kinyaa nyie mliokuwa mnabeza kelele wa watanzania waliokuwa wanapaza sauti MO arejee alafu leo mnataka mpongezwe!
 
Aliyemteka Mo Dewji either anajiamini sana au sio mwenye akili timamu. Yaani anamteka mtu karibu na kwa Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Headquarters za Usalama wa Taifa. Alafu ana mtupa karibu na Ikulu. BILA UOGA KABISA!!
Hahhha, mwenye macho haambiwi tazama
 
Hivi kuna kosa lolote mtu kuwashukuru police embu tuacheni siasa yaani chuki yako dhidi ya jeshi la police unataka kuwaambukiza wengine uwe na shukrani bwana, wewe usiku umelaka na familia yako police wanakesha kukulinda leo unaishia kuwadharau kisha sababu za kisiasa muogope Mungu mkuu.
Acha ukuda...Mungu ndiye Mlinzi wetu.
Polisi watekaji na watesi wa raia tuu
 
Hii inaonyesha familia wamelipa ransom!

Moja ya masharti ya ransom ni kutozungumza kuhusu tukio lote!

Kama atazungumza kuhusu yaliyomsibu mpaka akarudi basi hiyo itaonyesha kuwa hakulipa ransom na hakuna makubaliano.

Hoja iliyopo mbele yetu kwa sasa, Je, kama amelipa ransom, nini kwa sasa nafasi ya matajiri nchini kuhusiana na usalama wao kwa sababu kulipa ransom ni kufungua mlango wa biashara ya kidnapping and ransom nchini kwa matajiri.

Kosa la kulipa ransom baada ya kutekwa ambalo nchi za kusini mwa Afrika kama Afrika Kusini na Msumbiji walilianza kwa matajiri ndilo kwa sasa linazidi kuwatafuta kwa kasi zaidi.

Je, kuna uwezekano na Tanzania tukaelekea ambako nchi za kusini mwa Afrika ziliko kwenye biashara ya kidnapping and ransom?
Kwahiyo wewe ndo ulipokea ransom.. Watetea watekaji mnapata kizungumkuti sana huu utawala.. Kila jambo mnaumbuka
 
Yaani kelele za Lema ziwe msingi wa kupatikana Dewji lakini kelele hizo hizo zisiweze kumleta Ben Saanane? You must be joking!

Nani mwenye uhusiano wa karibu kikazi na kimaisha kati ya Lema na Ben Saanene au Dewji?

Kumbuka Ben Saanane alikuwa mfanyakazi wa CHADEMA

Ulichofanya ni kutoa shukrani ambazo hazina hata ukweli kifikra!
Inawezekana la ben saanane wanalijua wenyewe chadema..kumbuka mbowe alishasema lisiongelewe..wakati la mo wameliongelea
 
Mliwapa hiyo taarifa???????? Au mlikuwa mnakosoa tu eneo la picha ya gari
 
Sasa ulitaka alalamike ili wamrudie tena????Usiwe bwege hivyo unafikiri tu ndani ya box!Conspirqcy ziko za aina nyingi,nenda kasome mikasa iliyowahi tokea duniani ili upanue uwezo wako wa kufikiri!
Hivi unaposema katekwa na serikali ni kufikiri ''nje ya box'' ehe!!! Yaonyesha msemo unausikia tu lakini hta maana huijui. Kama alikuwa na matatizo na serikali ambayo yanamfanya hata aogope kuzungumza ukweli basi huyo ni mtu hatari sana na alistahili kupatwa na yaliyompata. Atakuwa na kosa gani mpake aogope kuuweka ukweli hadharani? Na kama anaogopa bado kuna alternative ya kuhamia nchi nyingine ili apate kuzungumza ukweli! Lisu alishambuliwa kwa risasi na bado hakuogopa kuweka feelings zake hadharani!
 
Gari iliyokuwa inatafutwa Tanzania nzima, ndio gari hiyo hiyo iliyomtupa Gym Khana😯..., sijui walijuaje kuwa gari iliyomtupa Gym Khana ndio gari ile ile iliyomteka mtekwaji?
 
Wa bongo wape kichwa cha habari story watatunga wenyewe

Mooooooooooooo
 
Back
Top Bottom