Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Namnukuu Matola

"Ina maana wewe hujui mtekaji ni nani? Pole
sana.
Hivi kwa akili yako baada ya IGP kutoa picha ya
Toyota surf unaweza kusubutu kwenda na
Toyota surf karibu na ikulu?
Mo ametekwa prime area na amerudishwa
prime area, hata kama wewe ni mfia chama
jaribu kuvaa ubinadamu ingawa maccm yote ni
bora hata ukutane na chui aliyeshiba."
Kwaiyo Toyota surf zilizuiwa kutembea mjini? Au zote zilikuwa zinakaguliwa kila wakati zinapotembea? Watekaji walikuwa naakili Sana. Kwa kumrudisha MO na gari ileile wamepoteza ushahidi mwingine muhimu.
 
Hivi kulikuwa na ugumu gani kumwambia, uje unahitajika kwa mahojiano, badala ya kumchukua kwa mbinu za utekaji?

Au walidhamiria kumfanyia jbo baya zaidi lakini mazingira yamewalazimisha kumwachia?
Ndugu wanabodi,
Ukiiangalia press ya IGP kisha ukaangalia majigambo ya Mambosasa akinesha gari iliyotajwa na IGP kuwa imepatikana na MO akiwa salama kabisa lazima utagundua kuwa kuna picha imechezwa hapa
Lakini yote kwa yote tumshukuru Mungu MO kapatikana salama
Aksante.
 
Kuna Press leo saa 8 mchana ya Sirro i think tutasikia mengine tusiyoyajua.
 
Hapana hujaelewa vizuri mkuu. Gari limevuka mpaka mara 3. Yaani kwa kuingia, kwa kutoka likiwa na Mo, na kuingia tena likiwa na Mo. Yaani hatutapa watekaji wenye huruma kama hawa. Walivuka na Gari hadi Msumbiji ah! Sijui Kenya halafu wamemrudisha Mo na Gari wakatuachia. Fantastic.

Haha hii kali aisee na bado wakaenda kumuacha gymkhana! Huu mfumo huu!
 
Kauli ya kumshukuru tu mheshimiwa rais mm ndo inanipa shida sana aisee,

Kwann amshukuru rais? Wakati watekaji walimchukua na wamemwachia bila nguvu yeyote kutumika

Shukrani kwa raisi ni za nn hasa?
Labda rais alichangia kwenye 1bil.ransom, si unajua tena mzee baba kwa kuchangia. Au aliwaelekeza wasiojulikana washushe dau maana naskia walikuwa wanahitaji utirioni
 
Habarini wana jamvi,Hivi karibuni kabla ya kutekwa MO,kulikuwa na sekeseke la watu kuandamana kwasababu ya huduma duni ya mabasi ya mwendokasi(BRT)

Wakati maandamano hayo yakishikakasi ghafla likaingia sakata la kutekwa MO" watu wakasahau shida za mwendokasi wakawa bize na MO,

Sasa inasemekana "MO"amepatikana tunashukuru kwa kampeni zenu za kumtafuta

Rudini na muendelee kuandamana na kushinikiza kutatua changamoto zilizopo kwenye mwendokasi

Kilichofanyika pengine ni kujaribu kuwatoa kifkra ili kuzima kelele za mwendokasii.

Nawasilisha kwa hisani ya kichwa maji.
 
Hivi aliyetekwa anaptikaneje bila kuwapata wahalifu! Kwa tafakuri hii naunga mkono hoja ya hizo 1b wapewe vijana wetu.
 
Vipi kuhusu aliyetekwa na kupelekwa mozambiki alafu akarudishwA?
Kamati kuu ya Chadema ili wahoji Watekaji then ikawapa Karipio

Muulize YericKo atakutajia Wabunge wa Chadema wenye tabia Za kuteka wenzao
 
Kutekwatekwa kunaanza kuwa ustaarabu wa awamu hii, si ajabu hata wewe muda wowote wakikutaka unapotea.
Wenye mapesa wananafasi ya kutoa ma-bi yao na kuachiwa wengine tindikali inawasubiri au tukuone unaelea koko beach. Hatari sana kuliko hata Rwanda
 
Tulia unaonekana unachemka sana.
Vile Vishindo tu vya Jeshi letu la Polisi, vimewafanya watekaji washindwe cha kufanya zaidi ya kusalenda.
Walikuwa wamezingirwa pande zote na hawana cha kufanya, hata kudai pesa walishindwa. Watadai kwa njia gani ?
Watalipwaje ?
Hawakuwa na namna zaidi ya kumwachia
Wangi mmeuangalia huu utekaji kirahisi sana.
Haikuwa rahisi hivyo.
Nimekuelewa. Kwa kuwa walishazingirwa, maana yake walishajulikana walipo. Tusubiri vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikiwapafikisha katika Mahakama ya Kisutu.
Vinginevyo, viwaombe radhi Watanzania, na hususan Mo na familia yake ama kwa kushindwa kuwatia nguvuni Watesi wa Mo huku wakiwajua, au kwa kushindwa kuwajua Watesi hao kutokana na uduni na udhaifu wa taaluma ya upelelezi huku wakikataa msaada toka nje!
 
Hebu subir hapo hapo alipiga simu! Kwa hiyo walimpa na simu apige au alipata simu kwa msamaria mwema? Sasa huyo aliyempa simu ndo ana claim hiyo Billion au? Pia hilo gari lilimtokea walisema lishavuka mpaka! Tena leo tunaliona! Hawa wanatuona mazwazwa kabisa, haya tuleteeni hiyo cctv shootage maana jana mzee wa sisitiv alijaribu kuficha pic la gari lkn bado watu wakamzidi akili! Na ndo maana hawakusema rangi ya gari wala habari ya noah hawataki tusikie!

All in all nina furaha tajir karudi sasa kifuatacho ni kuwa zakaria tuu maana washa turuhusu kumiliki silaha.
Zakaria aliwashtukiza kitu cha moto.
 
Back
Top Bottom