Mohamed Kiluwa kashindwa kuendana na zama hizi

Mohamed Kiluwa kashindwa kuendana na zama hizi

MAFILILI

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,377
Reaction score
1,200
Siyo siri tena ujasiriamali wa Kiluwa kuweza kukusanya rasilimali pesa kwa wageni huku akitumia udhaifu wa mfuko wa Halmashauri zetu na Serikali ya mkoa wa Pwani umegota rasmi leo pale magogoni kutokana na Rais Magufuli kuungana na Lukuvi kupingana na aina ya fursa anazochangamkia Kiluwa.

Mfano kakusanya bilioni 5 kutoka kwa wawekezaji wenziwe huku yeye kafanikiwa kupata eneo la ekari 1,000 kwa bilioni 1

Hongera Rais Magufuli kwa kuwaumbua watanzania kama hawa waliozoea kutumbua zama zilizopita.
 
Mrudishieni bilioni 1 yake ndio mchukue hizo hekari 1000 mlizomuuzia!!!Yaani mtu kapiga sound,akauziwa kihalali na mamlaka za Serikali halafu ananyang'nywa bila kurejeshewa fedha yake,si sawa!
 
Mrudishieni bilioni 1 yake ndio mchukue hizo hekari 1000 mlizomuuzia!!!Yaani mtu kapiga sound,akauziwa kihalali na mamlaka za serikali halafu ananyang'nywa bila kurejeshewa fedha yake,si sawa!
Mwizi mwingine huyu
 
Leo kaumbuka mbele ya jpm mzee huwa anapasua palepale ukitaka unune yeye anakuwa ameshamaliza kulitoa lililomoyoni mwake! Kawambia ccm ya Sasa siyo ya Zama hizi
 
Siyo siri tena ujasiriamali wa Kiluwa kuweza kukusanya rasilimali pesa kwa wageni huku akitumia udhaifu wa mfuko wa Halmashauri zetu na Serikali ya mkoa wa Pwani umegota rasmi leo pale magogoni kutokana na Rais Magufuli kuungana na Lukuvi kupingana na aina ya fursa anazochangamkia Kiluwa.

Mfano kakusanya bilioni 5 kutoka kwa wawekezaji wenziwe huku yeye kafanikiwa kupata eneo la ekari 1,000 kwa bilioni 1

Hongera Rais Magufuli kwa kuwaumbua watanzania kama hawa waliozoea kutumbua zama zilizopita.

Kiluwa Mohammed alijiteua kuwa dalali! Bado mawazo yake yalikuwa kulekule kwa awamu ya tatu na nne! Hi ni dalili tosha kuwa kama chaguo la Rais wa awamu ya nne angalikuwa Rais nchi ingeuzwa na kwa miaka 200 watu wangaliweza kuirudisha kwa wa Tanzania. Pili kama Mhe Lowassa angalikuwa Rais na Maalim Seif kuwa Rais wa Zenj basi Muungano ungalivunjika automatically 2015 kwani Maalim alitaka Zanzibar iwe na balozi wake Umoja wa Mataifa, Balozi wake AU, Waziri wa mambo ya nje wa Zenj, Wabunge 9 kutoka Zenj kuwa Wabunge wa bunge la Africa Mashariki(EAC)!!! Incidentally, kule Zanzibar kwa sababu hamna mbuge(Muwakilishi) kutoka chama cha upinzani, ni rahisi sasa kupitisha sheria ndogondogoo kwenye katiba ya Zanzibar kuimarisha Zenj na kufanya chama tawala kuwa chama chenye kushika hatamu - kufuta nafasi ya makamu wa Rais na kuwa na Waziri kiongozi tu!
 
Back
Top Bottom