Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
You are quite right mkuu, this is one sided story. Na wala haipo hivyo kwa ninavyoelewa. Mchawi wa Mwameja kwenye hiyo deal alikua ni Kasim Dewji aliyetaka kumzunguuka Jomo Sono ambaye ndio angekua wakala wake. Kasim alimdanganya Mwameja waachane na connections za Sono na wakaenda wao wenyewe Readings ili Kassim apige pesa. Readings wakafanya mawasialiano na Jomo Sono ambaye alishangaa imekuaje huyo mchezaji kaenda huko bila kumtaarifu na akajiondoa kumdhaminiA classic one sided story. Na ni somo zito juu ya kutovunja madaraja ukishayavuka.
Kadhulumiwa dola 6,000/= , sawa kama ni kweli, katukanana nao.
Katafuta njia mbadala kaondoka. Kafika mbele kakuta anahitaji watu hao hao wamchongee vyeti ambavyo hana!
Leo analaumu wamemharibia maisha yake wakati yeye mwenyewe ndio alikuwa hana vyeti!
Wazungu ni watu wa kufata protocol hasa za reference. Jomo Sono alivojitoa nao wakaacha kumpa mkataba Mwameja na kupelekea yeye kukaa Uingereza akifanya shughuli zisizohusiana na soka.Ka simu Dewji akajirudia zake kimyakimya. Hivyo vikwazo anavyodai aliwekewa na Rage na Ndolanga ni kweli lakini lakini havikua sababu ya yeye kukwamishwa bali deal ilikua imeshaharibiwa na Kasim Dewji kwa ujuaji wake.
Pia Mwameja anaposema hatamsamehe Ndolanga anakosea sana. Mbona yeye wanachama, mashabiki wa Simba na Watanzania kwa ujumla walishamsamehe kwa dhambi yao ya kuuza mechi ya fainali ya Kombe la Washindi Barani Afrika kati yao na Stella Abidjan? Au anadhani tumesahau?