Mohamed Mwameja: Siwezi kumsamehe Muhidin Ndolanga

Hivi unazungumziaje suala la Moses Odhiambo kukosa kushindwa kusafiri na timu kwenda Nigeria wakati alikuwa mchezaji tegemezi wa Simba ?

Hii nayo haikuwa hujuma ya kina Wambura kweli ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hilila Moses Odhiambo sina hakika Mkuu ingawa kwa figisufigisu za kwenye soka zilivyokua miaka ya nyuma yote yanawezekana. Shaka yangu kwa jambo hilo ni kwamba Wambura ni Simba damu sijui kama angeweza kufanya hivyo kama jambo hilo halikua na maslahi ya moja kwa moja kwake.

Zaidi ya hivyo haijawahi kutokea Simba au timu yoyote ya Tanzania kupata angalau sare tu pale Nigeria, iwe Lagos au Aba, tena kuanzia vilabu kama Simba (enzi za Racca Rovers) au Pan Africa (wakicheza na Ibadan Shooting Stars) na pia timu yetu ya Taifa, mara zote tulichezea kichapo.
 
Labda kitambulisho cha NIDA

Kingekuwa ni kitambulisho cha NIDA angekipata kwa nguvu!

Hiki ni kitu kinachotoka kwa hiari, kwa magumashi, ambacho Mwameja alitaka FAT wamchongee wamtumie, wakati washatukanana, wakampiga chini!

South Afrika hawakutaka mifarakano na FAT wala Simba, wamenunua mchezaji wakatuma hela FAT na ujumbe hii hela pelekeni Simba. FAT kabla ya kuwaambia tuna hela yenu mkononi wakakumbusha deni lao, Simba wakazingua, FAT wakakaza hukumu!

Mwameja kawatukana, kaondoka kibaharia. Yakamkuta mbele. Anakuja kulia leo.
 
Sina Shaka na taarifa hii, Mwameja ni moja kati ya wachezaji wengi wa kitanzania waluotendewa mabaya na aidhw viongozi wa FAT au vilabu vyenyewe.
Kweli kabisa, Ndolanga na katibu wake Rage walikuwa watu waovu sana.
Hivyo vikwazo anavyodai aliwekewa na Rage na Ndolanga ni kweli lakini lakini havikua sababu ya yeye kukwamishwa bali deal ilikua imeshaharibiwa na Kasim Dewji kwa ujuaji wake.
A classic one sided story.
Acheni kuwatetea, mnafikiri moja ya sababu ya FAT kuvunjwa na kuanzishwa TFF ni nini?

Hata Ken Mkapa aliwahi kulalamika kuhusu Rage wakati akiwa katibu mkuu wa FAT, jinsi Yanga walivyodhulumiwa pesa za CAF. Kitendo hicho ndicho kilipelekea Rage kufungwa jela.
 
Acha uongo mkuu, ndolanga aligoma kutoa ITC, Ishu ya stella mlizidiwa uwezo na bolizozo
 
Asiyejua maana haambiwi maana. Wewe umeyasoma kama historia wengine wameyaishi, kalagabaho
Unahisi mimi ni dogo eeh? Kwa taarifa yako hadi hizo mechi za simba hadi anafika fainali nilikuwa nahudhuri, my dad was redio presenter (RTD) kila game nilikuwa natimba nae, ishu ya mwameja ni ndolanga aliingiza figisu.
 
Unahisi mimi ni dogo eeh? Kwa taarifa yako hadi hizo mechi za simba hadi anafika fainali nilikuwa nahudhuri, my dad was redio presenter(RTD) kila game nilikuwa natimba nae, Ishu ya mwameja ni ndolanga aliingiza figisu
Ngoja nikwambie ndugu yangu. Sisemi kwamba magoli ya Stella yalikua ya uzembe. Yalikua ni magoli mazuri sana. Lile la George Bizzie alilomgeuzageuza beki Rashid Abdallah kama anakaanga chapati na hata lile la dakika ya 70 alilofunga Jean Boli Zozo kwa kombora la mita 30

Lakini Simba alikua anauwezo wa kushinda hata goli sita siku hiyo. Sina namna ya kukuaminisha kua mechi ilihujumiwa na Azim Dewji kwasababu hata ukiniambia nikuletee ushadi siwezi kufanya hivyo. Basi wewe amini hivyo kua Simba alizidiwa

Kuhusu Mwameja na Readings nilifahamu kwenda kwake South, nilifahamu mazungumzo yake na Jomo Sono na makubaliano yao, nilifahamu uingiliaji kati wa Kasim Dewji na hata hizo figisu za Ndolanga. Ni kweli Ndolanga akitaka kumbania lakini ilikua haijafikia hatua hasa ya ku saini mkataba.

Ni kwamba Readings hawakua tena na nia ya kuendelea na hiyo deal baada ya Jomo Sono kuwasiliana nao na kuwataka waachane na Mwameja baada ya kua amekiuka makubaliano yao ya kua yeye (Sono) awe wakala wake, kwa hiyo issue ya mtimanyongo wa Ndolanga ikawa kama pumu imepata mkohozi. Nadhani umenielewa Mkuu
 

Kwenda kufanya majaribio aihitaji idhini ya FAT/TFF ila uhamisho wa kimataifa unaitaji kuidhinishwa na wao. Kimsingi hakuna sababu ya kuzia mchezaji kwenda nje kwani si kwamba ni yy tu mnufaika bali hata Team yetu ya Taifa. Pia inafungua milango kwa vijana wengi kuongeza bidi. Hatukuwa na wachezaji nje ya nchi na hili la akina Ndolanga linaweza kuwa sababu kuu. Roho mbaya
 
Hicho kipindi mwameja baada ya kufeli huko reading ikabidi abaki huko akifanya kazi ya kuchuma matunda
 
Kwa mechi hii nadhani viongozi wetu walituuza.

Katika kikosi chetu Moses Odhiambo ndiyo alikuwa mchezaji aliyefunga na kutoa assist nyingi sana aliposajiliwa kuja simba akitokea Moro united.

Kilichotokea ni kwamba game yetu round ya pili first leg tulipaswa kwenda kucheza Nigeria dhidi ya Enyimba international ambayo ilikuwa haiko sawa sawa msimu huo kila mtu aliamini kwa form ya simba msimu ule tulikuwa tunaenda kuwatoa kuwafunga nyumbani au walau tungata magoli lakini katika dakika za mwisho za safari tukaambiwa Moses Odhiambo passport yake ilikuwa na shida hivyo asingeweza kusafiri na timu kwenda Nigeria hali iliyowashusha morali sana wachezaji na mashabiki kwa mchezaji tegemeo kukosa mchezo muhimu kama ule.

Kwanini nasema kulikuwa na hujuma ni kwamba Viongozi wa timu walitakiwa kuhakikisha kila kitu kiko sawa kwa wachezaji wao badala ya kusubiri maandalizi ya zimamoto na kama hawakuhujumu timu basi ulikuwa ni uzembe wa hali ya juu sana.

Mpaka leo siamini kabisa kama ule mchezo tulitolewa kwa kuzidiwa mbinu za uwanjani huenda ama tulihujumiana wenyewe au kulikuwa na uzembe wa kiwango cha juu kwa viongozi wetu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bongo kuna watu wana roho mbaya kishenzi. unaweza kuua. shenzi kabisa Ndolanga
 
#PESAZAKOOOZINAPITIAAAA FAT EMBU FUNGUKA ZAIDII LEO SIOO APRIL 1
 
Hayo ya mwameja, ukisikia ya yusuf macho jinsi alivofanyiwa na hawa jamaa unaweza toka machozi japo hayakuhusu
 
Hii sekeseke naikumbuka lakini sikuwahi kujua ilikuwa vipi ila leo nimejua, ndolanga mshamba sana
Huyu mzee Ndolanga ni mpuuzi A+ nakumbuka katika hili sakata huyu mzee alitoa tamko moja la kijinga sana kuhusu Mwameja kuwa kamwe hatochezea Taifa Stars km yeye bado ni mwenyekiti wa FAT. Kulikuwa na mechi moja kati ya Taifa Stars na Zaire. Kipa alikuwa Mwameja. Zaire walisawazisha kupitia kwa mchezaji wao Nzalambila Nsiala hilii zee likasema kbs kuwa mwameja hawezi tena kuchezea taifa stars. FAT ilikuwa km yake sijui mnakumbuka lilishampiga ngumu mtu na likafungwa sema Mkapa alilitoa. Jizi mno hili zee hopeless.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo mechi aliuza Azim Dewji sio Mwameja ndio maana unaona hakuna madhara yaliyompata ila uliza kilichotokea kwa Azim baada ya wazee kupiga kunuti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…