Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Nnaona hoja imekuingia na unaanza kubwabwaja na kuhororoja bila mpango. Ulifikiri "yetu" ingekusaidia?

Unioneshe mto wakati nna kisima uani kwangu, si upunguani huo.
Kebehi ni jadi yako, kila kitu kwako ni mashindano. Utakapokuwa umelala na unatafakari utatambua mantiki ya ninachokuambia. Warithishe wajukuu zako fursa za nchi hii, sio manung'uniko ya babu zako.
 
Kebehi ni jadi yako, kila kitu kwako ni mashindano. Utakapokuwa umelala na unatafakari utatambua mantiki ya ninachokuambia. Warithishe wajukuu zako fursa za nchi hii, sio manung'uniko ya babu zako.

Warithishe wajukuu zako ilm, si fursa.

Fursa zilikuwepo kabla yako na zitabaki kuwepo. Walikuwepo kina Qar'un na Suleiman, leo wako wapi? Wameondoka na amali zao tu.

Wanaonug'unika babu zangu, wewe kinakuuma nini? Au una uhusiano na babu zangu?
 
Kwani elimu sio fursa? Kama una maanisha mali, hata hiyo elimu huwezi kuipata bila mali. Kaulize ada ya shule ya Feza na uulize matokeo yao ya mitihani. Shukuru umesoma bure enzi za Nyerere wewe mama.
 
Kwa fikra kama hizi, mtu mweusi atausikia ukwasi redioni na kwa wazungu. Jifunze tofauti ya utajiri na ukwasi ndipo utaelewa maana ya kutumia fursa.
 
Kwa umri wa huyu mzee alipaswa kuwa na busara. Ni kwa nini kila linalomhusu au kumkuta maishani lazima analihusisha na dini?
Mwana...
Unajitisha bure hii ni historia hakuna udini wowote lakini ikiwa wewe mwenyewe unapenda kujiaminisha hivyo sikuzuii.
 
Kebehi ni jadi yako, kila kitu kwako ni mashindano. Utakapokuwa umelala na unatafakari utatambua mantiki ya ninachokuambia. Warithishe wajukuu zako fursa za nchi hii, sio manung'uniko ya babu zako.
Sooth,
Fursa gani tuwarithishe wajukuu zetu?

Kuwa nä wao watakujalipwa Bilioni 91+ za Memorandum of Understanding kati ya Misikiti na Serikali?

Fursa kuwa nä wao watakuja kuhodhi nafasi zote katika Wizara ya Elimu na NECTA?

Fursa kuwa viongozi wao wataheshimiwa na hawatabambikiwa kesi na kutupwa gerezani?

Fursa kuwa historia yao itaenziwa na haitafanyiwa njama ya kufifilishwa?

Nk. nk. nk...
 
Sooth nilikuambia kabla isome kwanza historia ya Waislamu kabla hujataka kuwajadili.

Wewe utufunze sisi.

Nani alitufunza kuunda TANU nä kupigania uhuru wa Tanganyika?

Hivi hujui kuwa tulikuwa tunajenga Chuo Kikuu 1968 tukahujumiwa na EAMWS iliyokuwa inasimamia mradi huo ikavunjwa?

Kisa kizima nimekieleza katika kitabu cha Sykes.

Soma historia yetu kwanza kabla hujaja na masimango?

Hivi unajua kwa nini Sheikh Suleiman Takadir hatajwi kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika?

Hivi unafahamu kwa nini Mufti Sheikh Hassan bin Amir alifukuzwa Tanzania Bara?

Unajua mchango wa Sheikh Hassan bin Ameir katika TANU?

Yapo mengi lakini ni vyema twende taratibu ili wasomaji wasielemewe lakini kwako wewe hujui kitu katika haya acha kujibaraguza.

Isome historia ya wazee wetu.
 
Udini kazini.
Dongo...
Catalogue ya Library of Congress Washington DC imeweka kitabu cha Sykes chini ya "Political History," na hivi ndiyo utambuzi wake ulimwenguni kote.

Huo "udini," ni uoga wenu kutaka kweli isisemwe.
 
Kwani elimu sio fursa? Kama una maanisha mali, hata hiyo elimu huwezi kuipata bila mali. Kaulize ada ya shule ya Feza na uulize matokeo yao ya mitihani. Shukuru umesoma bure enzi za Nyerere wewe mama.

Elimu ni fursa kubwa sana kwa waliyonayo lakini sidhani kama wewe umebahatika kuwa nayo.

Feza unajuwa kuwa ni shule ya wa "dini yenu"?
 
Sooth,
Fursa gani tuwarithishe wajukuu zetu?

Kuwa nä wao watakujalipwa Bilioni 91+ za Memorandum of Understanding kati ya Misikiti na Serikali?

Fursa kuwa nä wao watakuja kuhodhi nafasi zote katika Wizara ya Elimu na NECTA?

Fursa kuwa viongozi wao wataheshimiwa na hawatabambikiwa kesi na kutupwa gerezani?

Fursa kuwa historia yao itaenziwa na haitafanyiwa njama ya kufifilishwa?

Nk. nk. nk...
Haya madai yameshachoka. Unataka kuyarudia mara ngapi? Songa mbele, mkitumia fursa ninazowaonyesha hamtalialia tena. Huwezi kuwa na political influence bila kuwa na economic influence. Kamateni fursa ya economic influence. La sivyo tusaidie kuiondoa serikali ya CCM ambayo ilifumba macho wakati hayo yakitendeka.
 
Eliu ni fursa kubwa sana kwa waliyonayo lakini sidhani kaa wewe umebahatika kuwa nayo.

Feza unajuwa kuwa ni shule ya wa "dini yenu"?
Najua na hainipi shida. Kitu kizuri ni kizuri bila kujali ni cha nani. Lakini shule hizo ni za waturuki ambao wana muono wa magharibi zaidi kuliko mashariki ya kati. Ni muono ninaoukubali na ninaokushawishi uupokee.
 
Naam, nahisi huo muono wa Mashariki ya Kati ndiyo ulipelekea wale babu zako kuwa mstari wa mbele kupigania Uhuru wa Tanganyika.

Nimewahi kumsoma Mshume Kiyate katika hizo harakati, huyu "hero" alikuwa wa dini yenu na alikuwa akimfadhili mpaka marehemu Nyerere resheni ya nyumbani na ingawa hakuna asiyejuwa kuwa marehemu Nyerere alikuwa msomi wa kutukuka. Uliwahi kumsoma Mshume Kiyate?
 
Haya madai yameshachoka. Unataka kuyarudia mara ngapi? Songa mbele, mkitumia fursa ninazowaonyesha hamtalialia tena. Huwezi kuwa na political influence bila kuwa na economic influence. Kamateni fursa ya economic influence. La sivyo tusaidie kuiondoa serikali ya CCM ambayo ilifumba macho wakati hayo yakitendeka.
Sooth,
Nimekuambia soma historia ya Waislam.
 
Sooth,
Nimekuambia soma historia ya Waislam.
Mimi nimesoma Mwembechai Killings inatosha kuelewa fikra zinazoongoza manung'uniko yenu. Kila anayesimama kunung'unika-awe Ponda au Mohamed Said lazima atanukuu kitu kilichomo ndani ya Mwembechai Killings. Ndani ya Mwembechai Killings hakuna ushahidi, ni myths na conspiracy theories. You can do better than that.
 
Naam, nahisi huo muono wa Mashariki ya Kati ndiyo ulipelekea wale babu zako kuwa mstari wa mbele kupigania Uhuru wa Tanganyika.

Nimewahi kumsoma Mshume Kiyate katika hizo harakati, huyu "hero" alikuwa wa dini yenu na alikuwa akimfadhali mpaka marehemu Nyerere resheni ya nyumbani na ingawa hakuna asiyejuwa kuwa marehemu Nyerere alikuwa msomi wa kutukuka. Uliwahi kumsoma Mshume Kiyate?
Hawa wazee walikuwa kitu kimoja wakati wa kudai uhuru ndio maana walifanikiwa kwa kiasi kikubwa. Tatizo ni mimi na wewe tunaobaguana kwasababu ya mahaba ya dini zetu(sio Mungu wetu).
 
Sooth,
Siwezi kukuzuia kufikiri utakavyo.
Njozi hakuwa akizungumza na wewe au mfano wa watu kama wewe.

Njozi amezungumza na ulimwengu na umemsikia.
Imetutosha sisi kuwa wahusika walichoweza kufanya ni kukipiga marufuku kitabu.

Haikuwa kwa wao kutoa majibu ya "myths," "conspiracy theories," and what have you.
Kwetu hilo lilikuwa jibu tosha.

Hata historia ya uhuru wa Tanganyika ni "myth," hawakupata kuwepo watu kama Ali Msham, Tatu biti Mzee, Mama biti Maalim na mfano wa hawa.

Huu ni udini tu.

Usokuwa udini ni kuwafuta mashujaa hawa katika historia na nafasi zao zikajazwa na uongo.

Sultani Abdul Rauf Songea Mbano hakupambana na Wajerumani kwa silaha wala hakuwepo kabisa.

ALI MSHAM, TAWI LA TANU NA DUKA LA MAFUTA YA TAA LA MAMA MARIA NYERERE

Nashukuru Mzee wangu na wala sio mara yangu ya kwanza kukusoma katika mabandiko yako hapa yahusiyo historia.

Kwa kukumbusha tu kuna sehemu kwenye maandiko yako ulisema mama Maria Nyerere aliwahi kuwa na duka la mafuta ya taa Magomeni ila mwanae Andrew Nyerere akakanusha kwamba mama yake hakuwa na duka wala kuuza mafuta ya taa popote .
Shida ambayo tunapata sisi vijana wa leo ni hatujui ni wapi tusimamie
Nashukuru sana
UncleBen,
Simama kwenye ukweli.
Penye ukweli uongo hujitenga.

Tuanze na historia ya Ali Msham.

Ali Msham alikuwako na picha zake na tawi la TANU aliloanzisha nyumbani
kwake wanae wamenipa na mimi nikaziweka katika mtandao.

DSCN1793.JPG

Kulia wa kwanza Ali Msham aliyekaa kwenye meza ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Sote tumeziona.

Picha zile zimemuonyesha Ali Msham akiwa na Nyerere, John Rupia, Zuberi
Mtemvu, Sheikh Suleiman Takadiri, Bi. Titi Mohamed
na wazalendo wengine
miaka ya 1954/55.

Mtoto wa Ali Msham, Abdulrahman Ali Msham ndiye alionieleza mimi historia ya
baba yake wakati wa kupigani uhuru wa Tanganyika.

Kuhusu duka la mafuta ya taa wanasema baba yao alimuanzishia Mama Nyerere
mradi wa kuuza mafuta ya taa na kabla ya kufungua duka wakiuza katika kwama.

Baadae biashara ilipokua ndipo Ali Msham akamfungulia Mama Maria duka pale
nyumbani kwake.

Abdulrahman alinieleza kuwa Mama Maria katika kazi alizokuwa akifanya pale
dukani alikuwa akifuma sweta na alikuwa na kijana wake Joseph Kiboko Nyerere.

Kijana aliyekuwa akimsindikiza Mama Maria jioni kurejea kwake alikuwa Abdallah
Omari Likonda
ambae alikuwa mpwa wake Ali Masham.

Huyu Abdallah Omari Likonda yu hai hadi leo.
Ikiwa leo hii historia hawaitaki wala hapana haja ya ubishi.
Historia ya TANU iliandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni College mwaka wa 1981.Jina la Abdulwahid Sykes halikutajwa popote lakini mimi nimeandika kitabu kizima
kuhusu mchango wake katika TAA na TANU.

Mimi nawaachia wasomaji wangu waamue wenyewe nani mkweli na nani muongo.

DSCN1803.JPG

Abdulrahman Ali Msham akiwa amesimama nje ya nyumba yao ilipokuwa tawi la TANU 1954/55
 
Hawa wazee walikuwa kitu kimoja wakati wa kudai uhuru ndio maana walifanikiwa kwa kiasi kikubwa. Tatizo ni mimi na wewe tunaobaguana kwasababu ya mahaba ya dini zetu(sio Mungu wetu).

Sijuwi ni nani alikubagua?

Maana katika historia ya kivukoni sikuona "hawa wazee" waliokuwa "kitu kimoja" kutajwa bali niliona superman mmoja tu akitajwa kuwa ndiye aliyekuwa mdai uhuru pekee wa Tanganyika. Au wewe uliwaona?

Bado hujajibu swali langu, jee, uliwahi kumsoma Mshume Kiyate?

Ukimaliza unaweza kutupa kidogo historia ya vita vya maji maji? Maana nnaona huyu Mohamed Said anatupiga porojo tu eti anadai kuwa Songea Mbano anaitwa Abdul Rauf! mimi simuelewi-elewi, vipi wewe?
 
Back
Top Bottom