Sooth,
Siwezi kukuzuia kufikiri utakavyo.
Njozi hakuwa akizungumza na wewe au mfano wa watu kama wewe.
Njozi amezungumza na ulimwengu na umemsikia.
Imetutosha sisi kuwa wahusika walichoweza kufanya ni kukipiga marufuku kitabu.
Haikuwa kwa wao kutoa majibu ya "myths," "conspiracy theories," and what have you.
Kwetu hilo lilikuwa jibu tosha.
Hata historia ya uhuru wa Tanganyika ni "myth," hawakupata kuwepo watu kama
Ali Msham, Tatu biti Mzee, Mama biti Maalim na mfano wa hawa.
Huu ni udini tu.
Usokuwa udini ni kuwafuta mashujaa hawa katika historia na nafasi zao zikajazwa na uongo.
Sultani Abdul Rauf Songea Mbano hakupambana na Wajerumani kwa silaha wala hakuwepo kabisa.
ALI MSHAM, TAWI LA TANU NA DUKA LA MAFUTA YA TAA LA MAMA MARIA NYERERE
↑
Nashukuru Mzee wangu na wala sio mara yangu ya kwanza kukusoma katika mabandiko yako hapa yahusiyo historia.
Kwa kukumbusha tu kuna sehemu kwenye maandiko yako ulisema mama Maria Nyerere aliwahi kuwa na duka la mafuta ya taa Magomeni ila mwanae Andrew Nyerere akakanusha kwamba mama yake hakuwa na duka wala kuuza mafuta ya taa popote .
Shida ambayo tunapata sisi vijana wa leo ni hatujui ni wapi tusimamie
Nashukuru sana
UncleBen,
Simama kwenye ukweli.
Penye ukweli uongo hujitenga.
Tuanze na historia ya
Ali Msham.
Ali Msham alikuwako na picha zake na tawi la TANU aliloanzisha nyumbani
kwake wanae wamenipa na mimi nikaziweka katika mtandao.
Kulia wa kwanza Ali Msham aliyekaa kwenye meza ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Sote tumeziona.
Picha zile zimemuonyesha
Ali Msham akiwa na
Nyerere, John Rupia, Zuberi
Mtemvu, Sheikh Suleiman Takadiri, Bi. Titi Mohamed na wazalendo wengine
miaka ya 1954/55.
Mtoto wa
Ali Msham, Abdulrahman Ali Msham ndiye alionieleza mimi historia ya
baba yake wakati wa kupigani uhuru wa Tanganyika.
Kuhusu duka la mafuta ya taa wanasema baba yao alimuanzishia
Mama Nyerere
mradi wa kuuza mafuta ya taa na kabla ya kufungua duka wakiuza katika kwama.
Baadae biashara ilipokua ndipo
Ali Msham akamfungulia
Mama Maria duka pale
nyumbani kwake.
Abdulrahman alinieleza kuwa
Mama Maria katika kazi alizokuwa akifanya pale
dukani alikuwa akifuma sweta na alikuwa na kijana wake
Joseph Kiboko Nyerere.
Kijana aliyekuwa akimsindikiza
Mama Maria jioni kurejea kwake alikuwa
Abdallah
Omari Likonda ambae alikuwa mpwa wake
Ali Masham.
Huyu
Abdallah Omari Likonda yu hai hadi leo.
Ikiwa leo hii historia hawaitaki wala hapana haja ya ubishi.
Historia ya TANU iliandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni College mwaka wa 1981.Jina la
Abdulwahid Sykes halikutajwa popote lakini mimi nimeandika kitabu kizima
kuhusu mchango wake katika TAA na TANU.
Mimi nawaachia wasomaji wangu waamue wenyewe nani mkweli na nani muongo.
Abdulrahman Ali Msham akiwa amesimama nje ya nyumba yao ilipokuwa tawi la TANU 1954/55