Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Bora trump awapige vita tu... mtu anajilipua ili aue watu ni mtu wa kukaa nae kweli?
Uislamu hauko hivi...usiwe unaongea maneno ya kusikia vijiweni fuatilia ukweli ,ukweli utakufanya uwe na mawazo chanya....
 
Fred...
Ikiwa pana dhulma dhulma itakuwapo tu useme au ukae kimya.

Itashangaza ikiwa ipo haki sawa kwa jamii nzima na mtu akaja
na shutuma za dhulma.

Kwa ajili hii basi huwezi kutoa waa kuingiza katika kichwakile
kisichopo.

Hili la kwanza.

Pili mimi sijapata kutukana dini ya mtu yeyote kwani Allah kakataza
hilo.

Wasomaji wangu watakuwa mashahidi katika hili ila ukweli ni wajibu
usemwe.
 
Inshaallah Allah akuepushe na fitina. Uisalamu nikusema kwl hata ukichukiwa Allah atakulinda inshallah.
Mwaipungu,
Nilikuwa nawashangaza walimu wangu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
walipokuwa wanasomesha historia ya utaifa wa Tanganyika.

Nilikuwa nawaeleza mambo wenyewe wanashangaa na nikiwaambia kuwa
ikiwa wanataka kusomesha uongo na waendelee lakini mimi haya majina
ninayowapa ndiyo wazalendo waliomtia Mwalimu Nyerere katika siasa za
kudai uhuru Dar es Salaam na huko majimboni.

Nikawa nawaeleza pia yote yaliyotokea baada ya uhuru kupatikana mwaka
wa 1961 na kuwapa fikra zangu kwa nini wao leo wanasomesha historia siyo.

Nilikuwa nalichangamsha sana darasa na walimu walinipenda.
 
Its absolutely true that Tanzanian history has been cooked by some few mad people but the true history still lies in minds of a few intellects. Muslims played 90% to to independence of Tanzania of today and if it wasn't them, then I think it would have come later than 1961. Just to shade in some light I wish people ask themselves where did this freedom fighter we hear today come from? What is his history? Its just fragments of his history but the truth still lies out there. Anyway I wish people dig up the history of TAA, they would just know how cooked history is today.
 

Ina maana hata akina Max Mmuya na Mohammed Bakari walikuwa wakipindisha ukweli?
 
Dah umeongea vizuri sana
 
Chizcom,
Tatizo ni kuwa huifahamu historia ya Pwani ya Afrika ya Mashariki na Waarabu.
Waarabu hawakuchukua koloni lolote.

Waislam ndiyo watu wa kwanza kuweka msingi wa elimu hizi sehemu zetu kupitia
madras na ndiyo walikuwakuwa wanajua zle 3Rs yaani Reading, Writing and Arithmetic.

Ishumi kalieleza hili vizuri bahati mbaya nimesahau ''paper'' yake na mwaka.

Lakini Waislam baada ya uhuru walifanya juhudi za elimu na walianza kujenga shule na
waliweka hadi jiwe la Chuo Kikuu kupitia East African Muslim Welfare Society (EAMWS).

EAMWS ina historia yake pekee na nimeieleza katika Sehemu ya Tatu ya kitabu cha Abdul
Sykes
na ni historia iliyojaa simanzi.

Hutoweza kujadili historia ya Uislam na Waislam Tanzania bila kusoma historia hii ya EAMWS
na vipi ilikuja kupigwa marufuku na serikali mwaka wa 1968 na serikali ikawaundia Waislam
BAKWATA.

Huu ndiyo ikawa mwisho wa juhudi za Waislam katika kujenga shule na mradi wa Chuo Kikuu
ukafa.
 
Mwaipungu,
Tunaweza kuangalia hapa kwani jicho halisahau kile jicho la camera liliona:
UHURU DAY: TUWAKUMBUKE MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA



Selemani Mamba
Shujaa wa Maji Maji





Sultan Abdulrauf Songea Mbano wa Songea
Shujaa wa Maji Maji




Kushoto aliyesimama ni Ally Kleist Sykes, na kulia kwake ni
Abdulwahid Kleist Sykes, mbele kushoto ni Kleist Sykes
Mbuwane na Abbas Kleist Sykes. Katika hawa aliye hai ni Abbas.
Ukoo huu umeacha kumbukumbu nyingi kwa maandishi katika harakati za
kuunda African Association 1929 na kuunda TANU 1954. Picha hii imepigwa
mwaka wa 1942 Abdul aliporudi Dar es Salaam kutoka Lower Kabete Kenya
alipokuwa akipata mafunzo ya kijeshi katika King's African Rifles kabla
hajakwenda Burma kujiunga na Burma Infantry. Angalia utaona Abdul amevaa
sare ya Jeshi la Mfalme wa Uingereza. Ilikuwa akiwa Burma Vita Vya Pili Vya Dunia
(1938 - 1945) ndipo alipoamua kuwa 6th Battalion iliyokuwa na askari kutoka
Tanganyika waunde TANU wakirudi Tanganyika kudai uhuru.



Ufunguzi wa Jengo la African Asociation 1933 jengo lililojengwa na uongozi wa
Kleist Sykes kati ya 1929 - 1933 na hapa ndipo ilipoundwa TANU 1954 wanae
wawili Abdul na Ally wakiwa waasisi wa chama hicho.




Waasisi wa TANU 1954




Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake Sheikh Suleiman Takadir 1955



Hamza Kibwana Mwapachu 1913 - 1062



Kushoto: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes na Lawi Sijaona
katika dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1957



Kushoto: Bi. Tatu bint Mzee, wa tatu Julius Kambaraga Nyerere
wa tano Bi. Titi Mohamed wanamsindikiza Mwalimu Nyerere
Uwanja wa Ndege safari ya UNO 1955



Kulia: Bi. Titi Mohamed, Clement Mohamed Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Julius Nyerere
Nyuma kulia: John Rupia, Rajab Diwani na Mama Maria Nyerere
 
Ina maana hata akina Max Mmuya na Mohammed Bakari walikuwa wakipindisha ukweli?
Sherrif...
Sidhani kama walimu wale walikuwa wanapindisha ukweli.

Hawa walikuwa hawajui historia ya uhuru na mimi walikuwa wakiniuliza,
''Mohamed hebu tupe ushaidi wako wa haya.''

Jibu langu kwao lilikuwa, ''Hawa mimi ni wazee wangu wengine kwa damu
na wengine ujirani na wengine nimewaona kwa macho yangu hivyo nawajua.''

Hebu ingia hapa umsome babu yangu Salum Abdallah:
Mohamed Said: KUTOKA JF: BABU YANGU SALUM ABDALLAH

KUTOKA JF: BABU YANGU SALUM ABDALLAH
Mohamed Said June 17, 2016 0
Uncle Jei Jei:
Tatizo Nyerere si muislam kwa dini wala mmanyema kwa kabila.
Na kibaya zaidi, baba wa mwandishi huyu, aliwahi kuwekwa rumande na serikali ya Nyerere baada ya kuleta chokochoko za kidini zilizoanzishwa na AMNUT.
Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo
akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.
 
Mkuu kwa kweli umefanya jambo kuu la tarehe hii ya leo 9 desemba. Natamani kila mtu ajaribu kusoma hii historia.
 
Kwa mtaji huu naona kuna mengi sana yamechujwa katika historia Ya taifa hili
Motive ni ipi?
 
nime furahi sana kunielewesha itabidi nikutafute tufanikishe historia na kutafuta ukweli
 
Goo
 
WATU WADINI KAMA NINYI MNYONGWE TU, YANI UNAKAMATWA UNASEMA KWA 7BU NI MUISLAMU
Likandamwasada,
Hujui historia ya uhuru na tatizo la udini lilipoanzia katika nchi yetu.
Mada ya udini imekula muda mwingi sana hapa na mengi yamesemwa.

Inaelekea wewe ni mgeni katika ukumbi huu kwa hiyo kuna mengi ni
muhimu kwako kuyajua kabla ya kuchangia.

Ikiwa hujui historia ya Tanzania sema nami niko tayari kutoa darsa hapa.

Maalim Faiza mmoja wa waalimu katika somo hili husema,''Elimu bila
Khiyana.''

Lakini mimi nakuomba umsome kwanza Sivalon (1992):





Padri John Sivalon katika uk wa 37 wa kitabu chake anasema ''maadui wa
Kanisa Ukomunisti na Uislam.''

Sidhani kama ungependa Kanisa linyongwe.
 
nime furahi sana kunielewesha itabidi nikutafute tufanikishe historia na kutafuta ukweli
Chizcom,
Mimi nakushauri kwanza usome kitabu cha Abdul Sykes kabla ya hata
kuonana na mimi:



Ipo nakala ya Kiswahili.
 
Kwa mtaji huu naona kuna mengi sana yamechujwa katika historia Ya taifa hili
Motive ni ipi?
Sherrif...
Baada ya kupatikana uhuru kulifanyika Muslim Congress mbili mwaka wa 1962 na 1963
na Waislam chini ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) wakaja na mpango
wa elimu kwa vijana wa Kiislam kwani ukoloni uliwakandamiza sana Waislam katika elimu.

Kiongozi wa mipango hii alikuwa Mufti Sheikh Hassan bin Amir na Tewa Said Tewa.
Hakuna ambae hakutambua nguvu ya Waislam katika kupambana na ukoloni.

Hii ilitia hofu serikali iliyokuwa madarakani.

Matokeo yake ni kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa BAKWATA bila ridhaa ya Waislam
na Sheikh Hassan bin Amir akafukuzwa nchini na kurudishwa kwao Zanzibar.

Historia hii ikawa inaogopwa hadi leo na laiti kama si kwa Allah kunipa taufiq ya kuiandika
historia hii katika kitabu cha Abdul Sykes historia hii isingekuja kujulikana.
 

Msimamo au mtazamo wa Nyerere kuhusu uislam ulikuwaje especially kabla na baada Ya nchi kupata uhuru?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…