Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Wewe msukununu, jenga uislamu achana na ukatoliki.
Chuakachara,
Hiki ni kitabu kimechapwa mwaka wa 1992 na kimeuzwa madukani.

Kunitukana mimi ni kunionea mimi nimemjibu mtu kwa kumweleza
ukweli na kumpa rejea hiyo.

Sikua na ni ya kukughadhibisha ndugu yangu na zipo rejea nyingine
nzito kuliko hiyo ya Sivalon (1992).

Ipo nyingine ya P van Bergen (1981).

Rejea zote hizi kwa kweli zinatisha na kwa sasa huwezi kuzipata hapa
nchini.
 
Haya mambo mnayoyajadili yako very sensitive katika jamii zetu, hasa kwa context ya majadiliano yenu. Mnajenga ufa kati ya dini hizi mbili.... nimesoma story yako kuwa kama angalikuwa mkristo anatoka Vatican........
 
Msimamo au mtazamo wa Nyerere kuhusu uislam ulikuwaje especially kabla na baada Ya nchi kupata uhuru?
Sherrif,
Kitabu cha Abdul Sykes kimeeleza yote hayo.
Siwezi kukupa jibu katika mistari michache ya JF.

Utajua mengi kwa kusoma kitabu.

Nimeeleza historia nziima ya Baba wa Taifa toka siku ya kwanza anakutana
na Abdul Sykes hadi uhuru unapatikana na yaliyopitika baada ya uhuru.

Nimepita kote majimboni alikokuwa anapokelewa na wananchi dhalili masikini
lakini wana ari kubwa.

Angalia picha hiyo hapo chini ya 1956 yuko Dodoma na Idd Faiz Mafungo,
Sheikh Mohamed Ramiyya, Abdu kandoro
na Haruna Taratibu:



Una kurasa 350 za kusoma lakini nakuhakikishia hutokiweka kitabu chini.

Usidhani najipigia zumari hiki kitabu tunakwenda toleo la nne Kiswahili na la
tatu Kizungu.

Kimependwa sana.
 
Nitakitafuta hicho kitabu. Huyu father
John Sivallone alikuwa na mtazamo gani kuhusu uislam?
 
Haya mambo mnayoyajadili yako very sensitive katika jamii zetu, hasa kwa context ya majadiliano yenu. Mnajenga ufa kati ya dini hizi mbili.... nimesoma story yako kuwa kama angalikuwa mkristo anatoka Vatican........
Chuakachara,
Hakika yanachoma sana na ndiyo maana niliamua kuandika historia hii
ili tuwatambue wale waliovunja misingi ya umoja na haki iliyosimikwa
na wazee wetu waliopigania uhuru wa Tanganyika kwa mategemeo
makubwa ya ustawi wa kila Mtanganyika bila kujali dini yake wala kabila.

Nitakueleza kitu.

Ikiwa unaona haya yangu ni ''sensitive,'' msome Sivalon (1992) kisha
msome Njozi (2002) utaelewa kwa nini serikali ilikipiga marufuku kitabu
kile.

Kuondoa ufa ni kukubali kuwa tunalo tatizo na lazima lizungumzwe kwa
uwazi na hali ya upogo baina ya waumini wa dini kuu hizi mbili irekebishwe.

Kufagia taka chini ya zulia haitatusaidia.
 
Una maoni gani hivi sasa chama kilichopiganiwa na wazee wako yani ccm hivi sasa viongozi wake wakuu na jumuiya zake ni wakristo watupu na pia wote ni kutoka kanda ya ziwa? nini maoni yako katika hili?
 
Umeanza vizuri kama unaakili timamu kumbe mpuuzi tu
 
Askofu akamatwe aulizwe kwanini umeleta kanda za Huyu Mchungaji nchini kwetu...hicho kitu hakijawahi kutokea kamwe
 
Askofu akamatwe aulizwe kwanini umeleta kanda za Huyu Mchungaji nchini kwetu...hicho kitu hakijawahi kutokea kamwe
Claytonx,
Huu ndiyo ukweli wa hali ya nchi yetu na haitatusaidia kuukataa
ukweli huu.

Juu ya heshima ya masheikh hawa Waziri wa Mambo ya Ndani
Thomas Chikawe akawakejeli masheikh mahafidh wa Qur'an
kuwa upo uwezekano wa wao kuwa mashoga.

Kejeli hizi kawafanyia ndani ya Bunge na haikuwa lolote.

Huu ndiyo ukweli wa hali ya nchi yetu na haitatusaidia kuukataa
ukweli huu.
 
We nae ni walewale watanzania hatutaki udini.
 
We nae ni walewale watanzania hatutaki udini.
Thomas...
Mimi nimeona hilo neno lakini nasema watu wana makuzi tofauti.

Sisi kitu cha kwanza ambacho mama zetu wanatufunza mara tu
tukiwa na akili kidogo ni adabu.

Mimi siwezi kumuita mtu, ''we'' kwa kuwa nimefunzwa kufanya
hivyo ni kumvunjia mtu heshima.

Sitegemei kila mtu awe kwao kafunzwa hivyo ndiyo kisa cha mie
kukukaa kimya.
 
Uko vizuri sana mkuu Mohammed Said
I truly enjoy reading your works. Endelea kutujuza yaliyofichwa katka historia Ya Tanganyika
 
Sherrif...In Shaa Allah kila inapotokea nafasi tutabadilishana mawazo.
 
Unatafuta kwa kuwatoa watu ktk kiza na kueleza ukweli bila fitina yoyote historia ya nchi kifupi naweza kusema ni Chuki binafsi husda zao juu yko Allah atakunyia wepec
Teh teh teh...hivi wakati hayo yakifanyika yaani fitna na husda juu yenu, ninyi ambao mnakiri mpo wengu mlikuwa wapi?

Mlishindwa nini kuzuia hayo yote?
 
John,
Hapana mimi naeleza kama ninavyokua kutokana na uzoefu.

Naamini kabisa kuwa wasingeweza kumfanyia mtu aliyetokea
Vatican haya waliyonifanyia mie.

Juu ya haya sikukatazi kuwa na fikra tofauti.
Ni kwanini wasingemfanyia hivyo mtu aliyetoka Vatican ikiwa wanamsuspect ama wana taarifa mbaya kuhusu mtu huyo?

Lini mtaacha kulialia kwa kusema mnaonewa na hakuna wa kuwatetea? Allah si awatetee?

Unaandikaga vitabu vizuuri vya kuhusu historia ya nchi, lakini Uzwazwa wa Kidini haukuishi Mtu mzima weye Mohamed

Una udini umekukamata kama ukurutu.


Wabillah Tawfiq,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…