Mkuu Maalim jee ya kweli haya?!. Japo Vatican ni nchi na ina ubalozi wake nchini, uliwahi kusikia kuna viza ya kuingia Vatican?!. Immigation wanaangalia mtu umetoka wapi, visa ni ya Italy, na nadhani ndio nchi iliyokuwa ikiongoza kuuza mihadarati ulaya nzima biashara ikimilikiwa na the Mafia na wote ni Wakristu!.
Nimewahi kusafiri kutoka Tanzania na mzungu fulani lakini ni raia wa Tanzania, tukafika Marekani, wote wawili tukaonyesha passport zetu za Tanzania, mwenzagu akaruhusiwa, mimi nikazuiliwa nikachukuliwa picha na alama za vidole ndipo nikaruhusiwa!. Uhalifu ni uhalifu tuu, hauna dini, rangi wala kabila, japo wanaojilipua wengi ni watu wa dini fulani, hatuwatambui kwa dini yao, bali kwa uhalifu wao!, japo magaidi wengi ni watu wa dini fulani lakini hatuwatambui kwa dini yao bali kwa ugaidi wao!.
Ingefanyika sensa ya dini za wahalifu wote walioko magerezani, amini msiamini, watu mngeshangaa humu na kusema mnazingiziwa!. Tembelea hapa
Mapapa 560 wa Madawa ya Kulevya watajwa. Wamo
Kwenye list hii kati ya majina haya 560, majina 120 ni ya asili ya kizungu, majina 320 ya asili ya Kiarabu, majina 119 ni asili ya Kiafrika na jina moja ni la number ya gari.
Jee wajua what does this mean? .
NB. Naombeni sana msichanganye asili ya majina na dini za watu, majina ni majina tuu na dini ni imani, mtu anaweza kuwa na majina ya asili ya Kiarabu na akawa Mwislamu, au Mkristo na mtu mwenye jina la asili ya Kizungu akawa Mwislamu au Mkristo na wenye majina ya asili nao vivyo hivyo.
Mtu ukiisha tanguliza mawazo hasi ya kunyanyaswa kwa sababu ya dini yako, hata pale utakapofanyika ukaguzi wa ziada wa halali kabisa kwa ajili ya kujiridhisha, utaona una nyanyaswa!. Please stopuni hizi negativity, think positive, hata ukiwa treated harshly, lakiwa ukiwa positive kuwa hilo jambo linafanyika in good faith and not an ill motive, utakuwa na amani ndani ya moyo wako.
Mtu yoyote akiwa ni frequent flyer na safarri zenyewe za nchi za mashaka mashaka, kushukiwa ni kawaida!, mimi siamini ulisachiwa kwa ajili ya dini yako..
Hata hivyo pole kwa masahibu yaliyokufika!.
Paskali