Diesel generator
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 706
- 661
Kwanini mnafanya ugaidi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naam hapo ndipo pembe za mnafiki zilizogundishwa kwa gundi zinapodondoka na kumuacha akiaibika. Ama kweli mnafiki hana aibu. Watu wanapanga njama za kuabisha wenzao kwa dhana za kutunga!!Kwezisho,
Siku ile niliomba nipate faragha niswali.
Walinipatia Alhamdulilah.
Nililia na Allah katika sijda kuwa aninusuru kama alivyomnusuru
Issa bin Maryam kuuliwa na Wayahudi.
Alhandulilah Allah SW alipokea dua zangu.
Angalia hapo chini nini kilitokea:
Sasa hapo ikawa nimelipata jingine. Kumbe wauza unga hawakamatwi hadi amri itoke juu. Sasa kama amri haikutoka ndiyo muuza unga atapita aingize sumu zake mitaani? Hili likazidi kunidhihirishia kuwa kukamatwa kwangu hakukuwa na uhusiano wowote na vita dhidi ya mihadarati bali ni vita vile vile vikongwe dhidi ya Uislam.
Nikawa pale usiku kucha. Sasa wakati niko pale wakidhani nimelala. Wakawa wenyewe kwa wenyewe wanazungumza kuhusu hii ‘operation’ neno walilotumia ni kuwa 'leo tume-dial wrong number.' Wakawa wanasema, “Huyu bwana mbona hakuelekea kama muuza unga tena huyu mtu bwana kasoma kweli kweli” Wanadhani mie nimelala kumbe ni macho nawasikiliza. (Vipi utalala katikati ya michongoma?). We umeona jinsi alivyokuwa akijibu na kuchambua mambo.” Hilo ndilo likawa gumzo lao wakinisifia kwa ufasaha na mantiki lakini wakizungumza kwa sauti ya chini kabisa. Hapa ikanidhuhirikia kuwa hawa vijana walikuwa wanatimiza wajibu wao wa kazi tu lakini kiini khasa cha kukamatwa kwangu hawakuwa wanakifahamu.
Walionikamata walikuwa vijana kama wanne na wote walijitambulisha kwa majina ya Kiislam. Nilijua ni waongo kwa kuwa Muislam anonekana katika uso na katika matumizi ya lugha. Ila kitu kimoja lazima nikiri. Wale vijana walikaa na mimi kwa wema na hawakunibughudhi hata kidogo. Hata nilipokuwa nakwenda msalani kijana alienisindikiza alinitaka radhi akasema, ”Nakusindikiza kwa sababu ni sheria lakini sisi tunakustahi kwa hiyo utuwie radhi kwa kukufuta hadi msalani.”
Asubuhi wakubwa wakaja kazini lakini hakuna alienikabili. Walikuwa wakinichungulia kutoka mlangoni kama simba ndani ya kizimba kwenye zoo, nami nikawa najifanya siwaoni. Ndipo akaja mkubwa mmoja tena akaniita kwa jina langu na kwa heshima na bashasha sana, "Bwana Mohamed tuwie radhi sana pamekuwa na makosa kidogo tuwie radhi sasa hivi tutakuruhusu uende nyumbani. ” Akatoka nje akawa akipiga simu. Kisha akarudi ndani akaamrisha nibebewe mizigo yangu na gari la polisi linirudishe nyumbani. Kistaarabu kabisa nikakataa gari ile huku nikifanya maskhara kuwa naogopa gari ya polisi asijepiga simu akasema mrudisheni huyo mtuhumiwa. Ofisi nzima ikacheka. Hapo ndipo wale wakamataji wangu wa usiku wakabeba mizigo yangu nami nafuata nyuma tunatoka nje ya uwanja.
Achi...Nafikiri thread yangu ipo wazi tu. Kwa hiyo unataka kunithibitishia wanaowalawiti waislamu huko mahabusu/jela ni wakristo?
Na waziri alisema uchunguzi utafanyika kwa sababu ilikuwa ni tuhuma. Hivyo tuhuma inaweza kuwa kweli au si kweli.
Lakini nisisitize tu kwamba kuhusisha tuhuma za jinai au makosa mengine na UDINI ni kueneza chuki tu.
Citymist,Kwanini mnafanya ugaidi?
Blackman,hivi huyu ndo aliyeombewa kupewa PHD ktk Uzi Fulani?
Juan,Vita ya majimaji,chini, ya uongozi was kinjekitile ngwale,wale wa piganaji walikuwa wa Islam???,kweli!!!,ushaidi pls
Mkuu Maalim jee ya kweli haya?!. Japo Vatican ni nchi na ina ubalozi wake nchini, uliwahi kusikia kuna viza ya kuingia Vatican?!. Immigation wanaangalia mtu umetoka wapi, visa ni ya Italy, na nadhani ndio nchi iliyokuwa ikiongoza kuuza mihadarati ulaya nzima biashara ikimilikiwa na the Mafia na wote ni Wakristu!.“Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyasa Muislam?” Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa naponzwa na dini yangu.
.
Mbona huwa mkiguswa kidogo mnakimbilia kinga ya dini hio ni inferiority complex kwani maovu wameandikiwa watu wa dini Fulani,kama upo sawa acha wafanye kazi yao km hawajakutendea haki zipo mamlaka husika za juu unaweza kwenda kutoa malalamiko yako pia mahakama zipo kukutetea pia. Me MTU akianza kuhususisha dini ktk mambo namuona ana shida kidogo. Wao ufanya kazi Kwa taarifa wape ushiriano na pia ni haki yako kuwa na shahidi kabla ya kupekuliwa.
The Son...Huyu mzee huwa namheshimu ila likija suala la udini...... Tupa kule
The Son...
Dots katika uandishi huwa tatu tu...
Hizo za ziada tupate kule.
Sasa kama waislam walipigania vita ya uhuru sisi tuliozaliwa baada ya uhuru yanatuhusu nini? Yanatusaidia nini? Sisi tunajua hii nchi inaitwa Tanzania tutaishi hapa kwa Amani na upendo, Story zenu za mkoloni zimepitwa na wakati, Ongelea mambo ya teknolojia na maendeleo, Dini hizi ni propaganda za waarabu na wazungu, Wao wanakula bata mbaya na wanaenjoy maisha nyie wanawavisha makanzu na mabarakashia na MisalabaInterface,
Unajua ile paper yangu ilibadili mwelekeo wa ile conference na mimi
nilikuwa kati ya wazungumzaji wa mwisho.
Waamerika ingawa wanajifanya wanajua lakini si kuwa kila kitu kiko
hadhir kwao.
Naamini walishtuka sana nilipowaambia kuwa Waislam wa Tanzania
hawana ugomvi na USA wao wana matatizo yao ya ndani na utawala
ulioko madarakani.
Walishtuka nnilipowaambia kuwa Waislam ndiyo waliopigania uhuru wa
Tanganyika wakianza na kwa kunyanyua silaha dhidi ya Wajerumani.
Walishtuka nilipowaambia kuwa Waislam wa Tanzania wangependa kuwe
na mjadala wa wazi kujadili matatizo haya yote.
Bahati mbaya Sheria ya Ugaidi imesababisha viongozi wao kukamatwa na
taasisi zao kufungwa kwa uonevu tu.
Sasa pale Chuo Kikuu Cha Ibadan kitabu cha Sykes kimekuwa kikisomeshwa
toka 2003.
Wanafunzi na waalimu wakawa wanaijua hali ilivyo Tanzania na hii ndiyo
sababu ya wao kusema Sheria ya Ugaidi haiwezi kupitishwa Nigeria kwani
huko ni kutangaza vita na Waislam.
Waamerika wakawa kwa njia moja nimewavurugia mipango yao.
Yaliyofuatia hapo sasa ni historia.
Leta kaka tujue kilichojiriLeloo...
Nimesema kuwa nitakuwekeeni kidogo maana ni mkasa mrefu.
Sikutaka kuwachosha wasomaji wangu.
Ila ikiwa unataka kujua nini kiliendelea naweza nikakuwekea
kipande cha mwisho In Sha Allah.
Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli za kunishughulikia zilipoaanza.
Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni kurekebisha mitambo.
Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu wa usalama.
Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.
Nilichukuliwa hadi kwenye chumba kimoja na hapo niliwakuta maofisa wa usalama watatu wakanikaribisha kwa taadhima kisha wakanambia kuwa niko chini ya ulinzi kwa kuwa zimewafikia taarifa zangu kuwa mimi nasafirisha mihadarati. Mpaka hapa sikuwa na hofu bado ilinijia picha kuwa yawezekana wamefananisha majina.
Niliwaambia huenda Mohamed Said muuza madawa ya kulevya siyo mimi niliye mbele yao. Wakaniambia kwa kujiamini kabisa kuwa taarifa zao ni madhubuti muuza unga ni mimi na wamekuwa wakinifuatilia siku nyingi. Hapo ndipo walipotoa pasi yangu na kuniomba niitambue kama hiyo pasi ni yangu au la. Niliwajibu kuwa hakika hiyo ndiyo pasi yangu khasa.
Wakaniamuru sasa tutoke twende nikachukue mizigo yangu ili wafanye upekuzi wa mihadarati katika mizigo niliyotokanayo Tehran. Hapo ndipo nilipojuwa kuwa niko katika lindi kubwa la matatizo na ubongo wangu ukaanza kufanya kazi kwa haraka huku nikisoma dua kumuomba Allah ulinzi wake kwani kwa hakika nilijua kama ni njama zimekamilika na leo imefika siku yangu.
Nikajiuliza itakuwaje watakapotoa madawa kwenye mizigo yangu. Nikaanza kufikiri vichwa vya habari vya magazeti yatakavyopambwa na habari zangu. Ikanijia yakini kuwa watu wa usalama wameniwekea madawa ya kulevya katika mizigo yangu ili waniangamize na maadui zangu wapumzike na shari yangu.
Nilimgeukia yule ofisa mkuu aliyekuwa ananihoji nikamwambia kuwa sitokubali kugusa mizigo yangu bila kuwapo mashahidi isijekuwa mizigo yangu ishawekewa hayo madawa ya kulevya kwani nilikotoka Tehran mizigo ilikuwa imekaguliwa na ilikuwa salama.
Hoja yangu kubwa kwao ilikuwa kupata uhakika kutoka kwao kuwa wananijua vizuri kiasi cha kuthibitisha kuwa kweli mie ni msafirishaji wa madawa ya kulevya. Jibu nililopewa ni kuwa wao wanafanya kazi kutokana na taarifa zilizowafikia. Wakasema, “Sisi tunazo taarifa zako kamili kuwa wewe ni msafirisha madawa ya kulevya.”
Nikawauliza,“Baada ya kupata taarifa hizo zangu nyie mmechunguza kutafuta ukweli?” Wakasema, “Ndiyo maana leo tumekukamata.” Nikawaambia, “Si kweli kama kwa sababu mie nafahamika Dar es Salaam takriban kwingi maana ndio nilikozaliwa na kukulia. Hapo Kariakoo ukiwaambia watu kuwa Mohamed ni “Mzungu wa Unga” kila mtu atacheka maana huo kwao ndugu zangu ni mzaha mbaya.”
Walitaka kujua nilkwenda kufanya nini Iran. Niliwaambia nilialikwa na serikali ya huko kuhudhuria mkutano. Wakataka kujua vipi nilipata mwaliko. Nikawajibu kuwa hilo swali sina jibu labda waiulize serikali ya Iran. Nikawaeleza kuwa mbona siku zote napita hapo uwanjani nikenda sehemu tofauti duniani kwa mialiko na kutoa mada sijakamatwa kimezidi nini katika hii safari ya Iran?
Niliwaeleza kuwa miezi michache iliyopita nilikuwa Chuo Kikuu Cha Ibadan kwa mwaliko tena mkutano umefadhiliwa na serikali ya Marekani na wamenipa na tiketi toka Dar es Salaam hadi Lagos na kuniweka hoteli na kunilipa fedha.
“Mbona hamkunikamata wakati ule?” Nikafungua mlango mwingine nikawaambia, “Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyasa Muislam?” Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa naponzwa na dini yangu.
Baada ya kukurukakara nyingi na mabishano makubwa kuhusu mie kukubali kufanyiwa upekuzi wa mizigo yangu alikuja binti mmoja katika wao na yeye akanihakikishia kuwa wao ni serikali na sio wahuni. Hawathubutu kuniwekea dawa katika mizigo yangu hivyo akanisihi sana kwa upole nikubali ili wajitoe wasiwasi na wataniachia endapo hakuna kitu.
Niliomba apatikane shahidi wa kushuhudia mizigo yangu kabla ya kufanyiwa upekuzi lakini hakuna mtu aliyekubali kuchukua dhima ile katika maofisa waliokuwa kazini pale uwanja wa ndege usiku ule. Upekuzi ukafanyika hadi mwilini. Hakuna kitu. Wakanipela katika choo maalum cha kutolea madawa kwa njia ya haja kubwa.
Nikakataa kujisaidia pale. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuona choo kama kile. Choo chenyewe ni cha aluminium. Tofauti na vyoo vya pale ambavyo siku zote ni vichafu, hiki kilikuwa kisafi sana kiasi mtu unaweza hata kutengewa chakula na akala bila ya kuhisi kinyaa.
Nilitegemea wataweka ahadi yao kuwa ikiwa hawatakuta madawa ya kulevya katika mizigo yangu watanirejeshea uhuru wangu wataniachia niende nyumbani. Haikuwa hivyo. Wakanirudisha ofisini kwao. Sasa wakaacha madawa ya kulevya wakahamia katika vitabu na “audio cassette” nilizokuwa nimepewa kama zawadi kule Tehran wakaniluliza kwa nini naingiza vitu vile khasa kanda za Khomeni na vitabu vyake nchini. Nikawauliza, “Kwani kanda na vitabu vya Khomeni haviruhusiwi kuingizwa Tanzania?
http://www.globalresearch.ca/non-mu...0-of-all-terrorist-attacks-in-america/5333619Mkuu Maalim jee ya kweli haya?!. Japo Vatican ni nchi na ina ubalozi wake nchini, uliwahi kusikia kuna viza ya kuingia Vatican?!. Immigation wanaangalia mtu umetoka wapi, visa ni ya Italy, na nadhani ndio nchi iliyokuwa ikiongoza kuuza mihadarati ulaya nzima biashara ikimilikiwa na the Mafia na wote ni Wakristu!.
Nimewahi kusafiri kutoka Tanzania na mzungu fulani lakini ni raia wa Tanzania, tukafika Marekani, wote wawili tukaonyesha passport zetu za Tanzania, mwenzagu akaruhusiwa, mimi nikazuiliwa nikachukuliwa picha na alama za vidole ndipo nikaruhusiwa!. Uhalifu ni uhalifu tuu, hauna dini, rangi wala kabila, japo wanaojilipua wengi ni watu wa dini fulani, hatuwatambui kwa dini yao, bali kwa uhalifu wao!, japo magaidi wengi ni watu wa dini fulani lakini hatuwatambui kwa dini yao bali kwa ugaidi wao!.
Ingefanyika sensa ya dini za wahalifu wote walioko magerezani, amini msiamini, watu mngeshangaa humu na kusema mnazingiziwa!. Tembelea hapa
Mapapa 560 wa Madawa ya Kulevya watajwa. Wamo
Kwenye list hii kati ya majina haya 560, majina 120 ni ya asili ya kizungu, majina 320 ya asili ya Kiarabu, majina 119 ni asili ya Kiafrika na jina moja ni la number ya gari.
Jee wajua what does this mean? .
NB. Naombeni sana msichanganye asili ya majina na dini za watu, majina ni majina tuu na dini ni imani, mtu anaweza kuwa na majina ya asili ya Kiarabu na akawa Mwislamu, au Mkristo na mtu mwenye jina la asili ya Kizungu akawa Mwislamu au Mkristo na wenye majina ya asili nao vivyo hivyo.
Mtu ukiisha tanguliza mawazo hasi ya kunyanyaswa kwa sababu ya dini yako, hata pale utakapofanyika ukaguzi wa ziada wa halali kabisa kwa ajili ya kujiridhisha, utaona una nyanyaswa!. Please stopuni hizi negativity, think positive, hata ukiwa treated harshly, lakiwa ukiwa positive kuwa hilo jambo linafanyika in good faith and not an ill motive, utakuwa na amani ndani ya moyo wako.
Mtu yoyote akiwa ni frequent flyer na safarri zenyewe za nchi za mashaka mashaka, kushukiwa ni kawaida!, mimi siamini ulisachiwa kwa ajili ya dini yako..
Hata hivyo pole kwa masahibu yaliyokufika!.
Paskali