Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
John,
Hapana mimi naeleza kama ninavyokua kutokana na uzoefu.
Naamini kabisa kuwa wasingeweza kumfanyia mtu aliyetokea
Vatican haya waliyonifanyia mie.
Juu ya haya sikukatazi kuwa na fikra tofauti.[/QUOTE
Extremism utawajua tu, unaamini wakati umeshasema wamarekani ndio walikuchongea Tz kutokana na kauli zako huko nigeria, kwa iyo unadhani mkristo angechongewa na wamarekani akiwa vatican asingekamatwa sababu ya dini yake. Kwani ulikamatiwa masuala ya dini au madawa ya kulevya, kwani hakuna wauza madawa ya kulevya waki kristo. Umelewa udini na kilevi hicho kitakutoka pindi roho itapokutoka, meanwhile ishi maisha yako yaliyobaki with your griefness na udini wako wa kikereketwa.
Kuna wachumi bora kwenye jamii zaidi ya Waislam?
Hebu tazama tu miji yote ya Tanzania na huko ulipopataja ilijengwa na Nani? kwa wingi wake na ni akina nani ni wafanya biashara wa kutukuka, hapo awali hadi leo hii?
Hivi huwa hamuoni au ni ujinga tu uliowajaa?
Mwenyezi Mungu ana shani yake, unapofikiri kuwa ukimnyima mtu elimu kwa hizaya ndiyo utammaliza basi Yeye humfungulia mengine usiyoyafikiria.
Umenyima elimu kampa biashara ambayo huyo asiye na elimu anakuajiri wewe mwenye elimu.
Huyo ndiyo Allah.
kwani kumuita MTU we au wewe ni tusi?, hivi unakijua kiswahili na miundo yake, mimi, wewe, yeye, ayo maneno yanaashilia matusi??Kuwa na adabu huwezi kumuita Mohamed Said "we" kama a naleta udini katika mada zake acha kuzisoma sio unajitoa ufaham kwa kuwa upo nyuma ya keyboard.
Huyu mzee ni muhimu sana kwa elim ya historia hapa jamvini, kama unamuuliza, basi fanya hivyo kwa staha
umsamehe kwani kakosea nini?, kwani kumuita mtu wewe ni tusi?, nijuavyo mimi hiko ni kiwakilishi cha jina (noun) cha nafsi ya pili umoja, ni kama kusema mimi au yeye tu, nyinyi ndio yawapasa kumuomba radhi kwakua mmemnukuu vibayaFdizzle,
Huwa kawaida hoja zinapopamba moto kuna wengine hawawezi kuhimili
na hil huwatoa adabu na kupandisha ghadhabu.
Tumsamehe hapa tuko kujadiliana kiungwana.
Mbona umetukatili Sheikh? Kisa hakijesha naamini..Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli za kunishughulikia zilipoaanza.
Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni kurekebisha mitambo.
Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu wa usalama.
Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.
Nilichukuliwa hadi kwenye chumba kimoja na hapo niliwakuta maofisa wa usalama watatu wakanikaribisha kwa taadhima kisha wakanambia kuwa niko chini ya ulinzi kwa kuwa zimewafikia taarifa zangu kuwa mimi nasafirisha mihadarati. Mpaka hapa sikuwa na hofu bado ilinijia picha kuwa yawezekana wamefananisha majina.
Niliwaambia huenda Mohamed Said muuza madawa ya kulevya siyo mimi niliye mbele yao. Wakaniambia kwa kujiamini kabisa kuwa taarifa zao ni madhubuti muuza unga ni mimi na wamekuwa wakinifuatilia siku nyingi. Hapo ndipo walipotoa pasi yangu na kuniomba niitambue kama hiyo pasi ni yangu au la. Niliwajibu kuwa hakika hiyo ndiyo pasi yangu khasa.
Wakaniamuru sasa tutoke twende nikachukue mizigo yangu ili wafanye upekuzi wa mihadarati katika mizigo niliyotokanayo Tehran. Hapo ndipo nilipojuwa kuwa niko katika lindi kubwa la matatizo na ubongo wangu ukaanza kufanya kazi kwa haraka huku nikisoma dua kumuomba Allah ulinzi wake kwani kwa hakika nilijua kama ni njama zimekamilika na leo imefika siku yangu.
Nikajiuliza itakuwaje watakapotoa madawa kwenye mizigo yangu. Nikaanza kufikiri vichwa vya habari vya magazeti yatakavyopambwa na habari zangu. Ikanijia yakini kuwa watu wa usalama wameniwekea madawa ya kulevya katika mizigo yangu ili waniangamize na maadui zangu wapumzike na shari yangu.
Nilimgeukia yule ofisa mkuu aliyekuwa ananihoji nikamwambia kuwa sitokubali kugusa mizigo yangu bila kuwapo mashahidi isijekuwa mizigo yangu ishawekewa hayo madawa ya kulevya kwani nilikotoka Tehran mizigo ilikuwa imekaguliwa na ilikuwa salama.
Hoja yangu kubwa kwao ilikuwa kupata uhakika kutoka kwao kuwa wananijua vizuri kiasi cha kuthibitisha kuwa kweli mie ni msafirishaji wa madawa ya kulevya. Jibu nililopewa ni kuwa wao wanafanya kazi kutokana na taarifa zilizowafikia. Wakasema, “Sisi tunazo taarifa zako kamili kuwa wewe ni msafirisha madawa ya kulevya.”
Nikawauliza,“Baada ya kupata taarifa hizo zangu nyie mmechunguza kutafuta ukweli?” Wakasema, “Ndiyo maana leo tumekukamata.” Nikawaambia, “Si kweli kama kwa sababu mie nafahamika Dar es Salaam takriban kwingi maana ndio nilikozaliwa na kukulia. Hapo Kariakoo ukiwaambia watu kuwa Mohamed ni “Mzungu wa Unga” kila mtu atacheka maana huo kwao ndugu zangu ni mzaha mbaya.”
Walitaka kujua nilkwenda kufanya nini Iran. Niliwaambia nilialikwa na serikali ya huko kuhudhuria mkutano. Wakataka kujua vipi nilipata mwaliko. Nikawajibu kuwa hilo swali sina jibu labda waiulize serikali ya Iran. Nikawaeleza kuwa mbona siku zote napita hapo uwanjani nikenda sehemu tofauti duniani kwa mialiko na kutoa mada sijakamatwa kimezidi nini katika hii safari ya Iran?
Niliwaeleza kuwa miezi michache iliyopita nilikuwa Chuo Kikuu Cha Ibadan kwa mwaliko tena mkutano umefadhiliwa na serikali ya Marekani na wamenipa na tiketi toka Dar es Salaam hadi Lagos na kuniweka hoteli na kunilipa fedha.
“Mbona hamkunikamata wakati ule?” Nikafungua mlango mwingine nikawaambia, “Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyasa Muislam?” Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa naponzwa na dini yangu.
Baada ya kukurukakara nyingi na mabishano makubwa kuhusu mie kukubali kufanyiwa upekuzi wa mizigo yangu alikuja binti mmoja katika wao na yeye akanihakikishia kuwa wao ni serikali na sio wahuni. Hawathubutu kuniwekea dawa katika mizigo yangu hivyo akanisihi sana kwa upole nikubali ili wajitoe wasiwasi na wataniachia endapo hakuna kitu.
Niliomba apatikane shahidi wa kushuhudia mizigo yangu kabla ya kufanyiwa upekuzi lakini hakuna mtu aliyekubali kuchukua dhima ile katika maofisa waliokuwa kazini pale uwanja wa ndege usiku ule. Upekuzi ukafanyika hadi mwilini. Hakuna kitu. Wakanipela katika choo maalum cha kutolea madawa kwa njia ya haja kubwa.
Nikakataa kujisaidia pale. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuona choo kama kile. Choo chenyewe ni cha aluminium. Tofauti na vyoo vya pale ambavyo siku zote ni vichafu, hiki kilikuwa kisafi sana kiasi mtu unaweza hata kutengewa chakula na akala bila ya kuhisi kinyaa.
Nilitegemea wataweka ahadi yao kuwa ikiwa hawatakuta madawa ya kulevya katika mizigo yangu watanirejeshea uhuru wangu wataniachia niende nyumbani. Haikuwa hivyo. Wakanirudisha ofisini kwao. Sasa wakaacha madawa ya kulevya wakahamia katika vitabu na “audio cassette” nilizokuwa nimepewa kama zawadi kule Tehran wakaniluliza kwa nini naingiza vitu vile khasa kanda za Khomeni na vitabu vyake nchini. Nikawauliza, “Kwani kanda na vitabu vya Khomeni haviruhusiwi kuingizwa Tanzania?
Nadhani unaelewa kiswahili vizuri tu lakini nikukumbushe kitu, kitu chochote endapo utakiweka sehem isiyostahili kitakuwa ni uchafu, ndivyo kwa maneno ya kiswahili ukitumia sehem isiyostahili ni mskosa pia,, nikuulize swali baba yako utaweza kumuita we?kwani kumuita MTU we au wewe ni tusi?, hivi unakijua kiswahili na miundo yake, mimi, wewe, yeye, ayo maneno yanaashilia matusi??
swala la msingi si kumuita baba yako wewe au kuto muita hivyo!!, swala hapa ni je neno wewe ni tusi au si tusi (kwa wazazi wa aina yako, unaweza hata kutaman kumpa razi mwanao sababu ya kukuita hivyo)Nadhani unaelewa kiswahili vizuri tu lakini nikukumbushe kitu, kitu chochote endapo utakiweka sehem isiyostahili kitakuwa ni uchafu, ndivyo kwa maneno ya kiswahili ukitumia sehem isiyostahili ni mskosa pia,, nikuulize swali baba yako utaweza kumuita we?
Mugunga hapana sijaja hapa hapa nimeandika yaliyopita 2007 na mkasa huu uko kwenye blog yangu www.mohammedsaid.com toka 2008.
Nilipokwenda kwa maana ya "kuja" ni Chuo Kikuu Cha Ibadan na sikwenda kutafuta kuhurumiwa.
Nilikwenda kuwaeleza Wamarekani kile wasichokijua kuhusu Uislam na ugaidi Tanzania na haikuwa kwa nia ya kutafuta huruma.
Sanctus,Un
Mkuu unafikiria Wamarekani Na Vyombo vyao vya Usalama walikuwa nyuma ya ukweli hadi wewe ulipowaeleza kwenye Huo muhadhara Chuoni Ibadan? Siku hizi unajishughulisha Na nini baada ya Huo Mkasa? Unaendelea kuwasilisha papers kwenye makongamano?
Uelewa wako mdogo sana umelala niangalie "swali la msingi" wapi niliposema"we"ni tusk? Nimekujibu hilo neno like tumia sehem isiyostahili wewe na mimi hatujuani lakini yule mzee anajulikana humu kuwa ni mzee huwezi kumuita "we" ni kumkosea adabu nay si uungwana na nimekuuliza baba yako unaweza kumuita "we"swala la msingi si kumuita baba yako wewe au kuto muita hivyo!!, swala hapa ni je neno wewe ni tusi au si tusi (kwa wazazi wa aina yako, unaweza hata kutaman kumpa razi mwanao sababu ya kukuita hivyo)
Hii IPO kiusalama zaidi kulingana na hali halisi mfano hapa tz ukitokea west Africa hasa Nigeria,Pakistan,somalia,Nepal,sri Lanka, lzm ukaguliwe mara mbili mbili kujiridhisha je we ni Salama sbb kuna baadhi ya raia wa nchi hizo wana mashaka,unga,utapeli,ugaidi, nk hata China ukitokea west Africa utakaguliwa sana kuliko atokae east Africa, kuna nchi mfano Korea, Japan,Oman,UAE, Dubai,USA,Ulaya yote,Russia huwa si za kutilia sana shaka sababu ya nature zao na ni nadra sana kuwakuta kwenye matukio ya shaka kiusalama watakavo tiliwa shaka si sawa na atokae Iraq,Somali,Nigeria nk .ni ktk hali ya kiusalama tu.Mohamed Said,
Hivyo tunaongea lugha moja kuwa kwa sababu moja au nyingine nchi mbalimbali zinaweza kuweka vikwazo au mahojiano marefu zaidi kabla ya kuingia nchi Fulani au unaweza kuhojiwa kwanini ulipata kutembelea nchi Fulani au ukiwa na stika ya viza ya baadhi ya nchi ktk pasipoti yako basi unaweza kuzuiwa kuingia mfano huu hapa chini:
Citizens of all countries require a visa to visit Saudi Arabia except the citizens of the Gulf Cooperation Council members, Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, and United Arab Emirates.[1] All visitors must hold a passport valid for 6 months.[2] Visitors holding passports containing any Israeli visa or stamp may be refused entry; Israeli passport holders are refused admission and transit.[3][4]
In December 2013 Saudi Arabia announced its intention to begin issuing tourist visas for the first time in its history. Council of Ministers entrusted the Supreme Commission for Tourism and Antiquities with visa issuing on the basis of certain regulations approved by the Ministries of Interior and Foreign Affairs.[5] A limited tourist visa programme was cancelled in March 2014. Visa policy of Saudi Arabia - WikiVisually
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Ndo imefika mwisho au TECNO yangu tu.
Hii ilitakiwa umkoti' huyu Mzee wetu Mohamed Said aid ,Pole zungu!
maelezo yako zungu yanaeleweka vizuri, ila yana ukakasi,
kwa nini unatajataja zaidi mambo ya kidini?
wewe ni kiongozi katika nchi hii kama unatajataja dini bira hata kutumia hekima, unadhani wengine watafanyaje?
hadi unajikita kwenye wingi!
Kama usipojisahihsha kwenye udini, huohuo udini utakukost, na unaweza kuta pamoja na yote wanakustukia kwa sababu ya mlengo wako wa kidini!
Mkuu jitahidi kubadilika.
Si hivo my Dada Kwa tz waislamu ndo wanaongoza kiuchumi na masuala yote ya biashara na uwekezaji fanya sensa angalia asilimia kubwa ya malori,daladala, mabasi,taxi soma ubavuni wamiliki wao 80% ni waislamu, anza viwanda vya dar Pugu road, Mandela,kilwa road,bagamoyo road, ingia maghorofa ya kkoo,nk nenda madukani,magengeni,nk asilimia 85 ni waislamu, ttzo nn sasa,waislamu wa tza wanashida moja hawapendani,ni wabinafsi,hawachangii masuala ya maendeleo yao mfano tu ni nadra sana kukuta hata kwenye michango mfano harambee za Ujenzi wa shule,misikiti,nk kukuta tajiri kajitolea zaid km ilivo Kwa upande wa dini zingine mfno ukistro,uhindu,nk ambapo wao ufanya harambee za michango ya kufa MTU unakuta MTU mmoja tu tena wa chini utoa na kutimiza ahadi ya kitu kikubwa,michango yao tu inaendesha tasisi zao bila kutegemea msaada nk,tofauti na waislamu ni wazito sana kuchangia manufaa yao zaid ya vile vifurahishavo macho mfano mashindano ya michezo,burudani nk.Tatizo haliko mfumo Kristo wala msikalie historia ndo vitu viwafanyavo mbaki nyuma japo mnanguvu kubwa kiuchumi anyway labda ni mipango ya Mungu kuleta mizania ya ubalance, wakristo kiuchumi ni wachache zaid kwenye nafasi za kitaaluma wanaonekana wana nguvu sababu ya Upendo na umoja wao.Cha msingi kitakiwacho muondoe dhana ya kujiona muu duni kitu ambacho akipo ni dhania tu hakuna abaguliwae nchini Kwa kunyimwa fursa kulingana na kuweza kwake,pia muondoe ubinafsi faidikeni nyote ki manufaa yenu na sote, futeni historia na dhana mfumo Christo ambayo ni dhana ya inferiority complex zaid kuliko hali halisi ni sawa na ukishaweka dhana ya kubaguliwa ukienda nchi za weupe kila wakufanyia wahisi unabaguliwa kumbe ni hisia tu.Wekezeni zaid kwenye elimu zote,harambee nk,ondoeni chuki za kuwabagua wengine wasio wa imani yenu kwenye shughuli zenu nk maana kuna kazi upewi kwenye maduka,viwanda,hotel,magari,biashara nk km wwe unatokea imani nyingine. Nakaribisha Hoja.Kuna wachumi bora kwenye jamii zaidi ya Waislam?
Hebu tazama tu miji yote ya Tanzania na huko ulipopataja ilijengwa na Nani? kwa wingi wake na ni akina nani ni wafanya biashara wa kutukuka, hapo awali hadi leo hii?
Hivi huwa hamuoni au ni ujinga tu uliowajaa?
Mwenyezi Mungu ana shani yake, unapofikiri kuwa ukimnyima mtu elimu kwa hizaya ndiyo utammaliza basi Yeye humfungulia mengine usiyoyafikiria.
Umenyima elimu kampa biashara ambayo huyo asiye na elimu anakuajiri wewe mwenye elimu.
Huyo ndiyo Allah.
napenda unavowajibu kwa busara japo wanakuwa wana mihemko kila unapowapa majibu mujaaarabu kabisaFyatu umeghadhibika.
Watu wa baadhi ya nchi wakifika US wanapigwa tena picha na kuchukuliwa upya biometric datas na sio kupekuliliwa.Hapo juu unasema umesafiri na mzungu hadi marekani kisha mwenzako ameachwa na wewe umekaguliwa(inawezekana hadi kwenye tigo) halafu bado unasema hakuna ubaguzi! Kweli wewe mwehu