Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli za kunishughulikia zilipoaanza.

Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni kurekebisha mitambo.

Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu wa usalama.

Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.

Nilichukuliwa hadi kwenye chumba kimoja na hapo niliwakuta maofisa wa usalama watatu wakanikaribisha kwa taadhima kisha wakanambia kuwa niko chini ya ulinzi kwa kuwa zimewafikia taarifa zangu kuwa mimi nasafirisha mihadarati. Mpaka hapa sikuwa na hofu bado ilinijia picha kuwa yawezekana wamefananisha majina.

Niliwaambia huenda Mohamed Said muuza madawa ya kulevya siyo mimi niliye mbele yao. Wakaniambia kwa kujiamini kabisa kuwa taarifa zao ni madhubuti muuza unga ni mimi na wamekuwa wakinifuatilia siku nyingi. Hapo ndipo walipotoa pasi yangu na kuniomba niitambue kama hiyo pasi ni yangu au la. Niliwajibu kuwa hakika hiyo ndiyo pasi yangu khasa.

Wakaniamuru sasa tutoke twende nikachukue mizigo yangu ili wafanye upekuzi wa mihadarati katika mizigo niliyotokanayo Tehran. Hapo ndipo nilipojuwa kuwa niko katika lindi kubwa la matatizo na ubongo wangu ukaanza kufanya kazi kwa haraka huku nikisoma dua kumuomba Allah ulinzi wake kwani kwa hakika nilijua kama ni njama zimekamilika na leo imefika siku yangu.

Nikajiuliza itakuwaje watakapotoa madawa kwenye mizigo yangu. Nikaanza kufikiri vichwa vya habari vya magazeti yatakavyopambwa na habari zangu. Ikanijia yakini kuwa watu wa usalama wameniwekea madawa ya kulevya katika mizigo yangu ili waniangamize na maadui zangu wapumzike na shari yangu.

Nilimgeukia yule ofisa mkuu aliyekuwa ananihoji nikamwambia kuwa sitokubali kugusa mizigo yangu bila kuwapo mashahidi isijekuwa mizigo yangu ishawekewa hayo madawa ya kulevya kwani nilikotoka Tehran mizigo ilikuwa imekaguliwa na ilikuwa salama.

Hoja yangu kubwa kwao ilikuwa kupata uhakika kutoka kwao kuwa wananijua vizuri kiasi cha kuthibitisha kuwa kweli mie ni msafirishaji wa madawa ya kulevya. Jibu nililopewa ni kuwa wao wanafanya kazi kutokana na taarifa zilizowafikia. Wakasema, “Sisi tunazo taarifa zako kamili kuwa wewe ni msafirisha madawa ya kulevya.”

Nikawauliza,“Baada ya kupata taarifa hizo zangu nyie mmechunguza kutafuta ukweli?” Wakasema, “Ndiyo maana leo tumekukamata.” Nikawaambia, “Si kweli kama kwa sababu mie nafahamika Dar es Salaam takriban kwingi maana ndio nilikozaliwa na kukulia. Hapo Kariakoo ukiwaambia watu kuwa Mohamed ni “Mzungu wa Unga” kila mtu atacheka maana huo kwao ndugu zangu ni mzaha mbaya.”

Walitaka kujua nilkwenda kufanya nini Iran. Niliwaambia nilialikwa na serikali ya huko kuhudhuria mkutano. Wakataka kujua vipi nilipata mwaliko. Nikawajibu kuwa hilo swali sina jibu labda waiulize serikali ya Iran. Nikawaeleza kuwa mbona siku zote napita hapo uwanjani nikenda sehemu tofauti duniani kwa mialiko na kutoa mada sijakamatwa kimezidi nini katika hii safari ya Iran?

Niliwaeleza kuwa miezi michache iliyopita nilikuwa Chuo Kikuu Cha Ibadan kwa mwaliko tena mkutano umefadhiliwa na serikali ya Marekani na wamenipa na tiketi toka Dar es Salaam hadi Lagos na kuniweka hoteli na kunilipa fedha.

“Mbona hamkunikamata wakati ule?” Nikafungua mlango mwingine nikawaambia, “Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyasa Muislam?” Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa naponzwa na dini yangu.

Baada ya kukurukakara nyingi na mabishano makubwa kuhusu mie kukubali kufanyiwa upekuzi wa mizigo yangu alikuja binti mmoja katika wao na yeye akanihakikishia kuwa wao ni serikali na sio wahuni. Hawathubutu kuniwekea dawa katika mizigo yangu hivyo akanisihi sana kwa upole nikubali ili wajitoe wasiwasi na wataniachia endapo hakuna kitu.

Niliomba apatikane shahidi wa kushuhudia mizigo yangu kabla ya kufanyiwa upekuzi lakini hakuna mtu aliyekubali kuchukua dhima ile katika maofisa waliokuwa kazini pale uwanja wa ndege usiku ule. Upekuzi ukafanyika hadi mwilini. Hakuna kitu. Wakanipela katika choo maalum cha kutolea madawa kwa njia ya haja kubwa.

Nikakataa kujisaidia pale. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuona choo kama kile. Choo chenyewe ni cha aluminium. Tofauti na vyoo vya pale ambavyo siku zote ni vichafu, hiki kilikuwa kisafi sana kiasi mtu unaweza hata kutengewa chakula na akala bila ya kuhisi kinyaa.

Nilitegemea wataweka ahadi yao kuwa ikiwa hawatakuta madawa ya kulevya katika mizigo yangu watanirejeshea uhuru wangu wataniachia niende nyumbani. Haikuwa hivyo. Wakanirudisha ofisini kwao. Sasa wakaacha madawa ya kulevya wakahamia katika vitabu na “audio cassette” nilizokuwa nimepewa kama zawadi kule Tehran wakaniluliza kwa nini naingiza vitu vile khasa kanda za Khomeni na vitabu vyake nchini. Nikawauliza, “Kwani kanda na vitabu vya Khomeni haviruhusiwi kuingizwa Tanzania?
Ni kisa kizr kujifunza lakini kimeniboa ulipoingiza utetezi wako wa kidini,,
Vatican na Tehran kwa kipindi hicho cha 2007 wapi kuliongoza kwa mihadarati,,

Nyie watu kwann badala ya kusimamia kwenye KWELI yenu ili mpate HAKI yenu mnakimbilia kulilia udini wenu,,
Si kosa lenu nasikia Kitabu chenu eti tangia mwanzo wa Aya hadi mwisho wake hakuna neno,, KWELI,, bali mna HAKI tu.
Wew umekamatwa kwa kuhisiwa tu ,, na ktk nafsi yako una hakika na KWELI yako kwamba ktk mizigo yko yote huna mihadarati hata kidogo,,

Sasa kwann usisimamie ktk KWELI yko badala yke unajitetea kwa kusema Vatcani kuna Wakristo wengi kuliko hapo Airpot,,

Huu ni utetezi wa kishamba na kutojiamini ktk Imani yako,, maana Huamini ktk KWELI ,, muda wote roho yko imejaa kutojimini ktk KWELI,,
 
Kama kuna mtu anajiona yupo salama kwasababu ni Mwislamu au Mkristo huyo ni Mpumbavu sana, ingekuwa dini Fulani ndio tiketi ya Kwnda Mbinguni basi wale wa dini nyingne wanajiaumbua tu, siku ya Hukumu utahukumiwa kwa kwanini Ulikuwa Mkristo na sio kwnini ulikuwa mkristo na ukaukataa uislam, Siku ya Mwisho utauhukumiwa kwanini ulikuwa Muislamu, ila sio kwanini ulikuwa muislamu na ukautaa Ukristo. Maana Uislamu n Imani ambayo Mungu anaitambua na Kuna watu wake anawatumia huko, alkadharika na Ukristo pia. Utahukumiwa pale ulipokuwepo sio kule ambapo haukuwepo, Wapumbavu wachache wenye sauti ndio wanachochea kusema dini fulan haifanyi, dini haina shida watu ndio wana shida.. Muabudu Mungu kibinafs....

= halikadhalika

Wapi Yesu amesema kuweni Wakristo?

Fungua uzi tuwekane sawa kuhusu Uislam na Ukristo, hapa si mahala pake.
 
Mkuu athari mojawapo ya dini ni kuwafanya very smart people very dumb...

Huwezi kuamini mtu smart sana kama Mzee Mohamed dini imempofusha ufahamu kabisa...inatia huruma sana!

Sasa wewe kinakuuma nini?
 
Ni kisa kizr kujifunza lakini kimeniboa ulipoingiza utetezi wako wa kidini,,
Vatican na Tehran kwa kipindi hicho cha 2007 wapi kuliongoza kwa mihadarati,,

Nyie watu kwann badala ya kusimamia kwenye KWELI yenu ili mpate HAKI yenu mnakimbilia kulilia udini wenu,,
Si kosa lenu nasikia Kitabu chenu eti tangia mwanzo wa Aya hadi mwisho wake hakuna neno,, KWELI,, bali mna HAKI tu.
Wew umekamatwa kwa kuhisiwa tu ,, na ktk nafsi yako una hakika na KWELI yako kwamba ktk mizigo yko yote huna mihadarati hata kidogo,,

Sasa kwann usisimamie ktk KWELI yko badala yke unajitetea kwa kusema Vatcani kuna Wakristo wengi kuliko hapo Airpot,,

Huu ni utetezi wa kishamba na kutojiamini ktk Imani yako,, maana Huamini ktk KWELI ,, muda wote roho yko imejaa kutojimini ktk KWELI,,
Bihampupile,
Nakushauri usome mwanzo hadi mwisho wa kisa hicho khasa nini
kilitokea pale Chuo Kikuu Cha Ibadan.
 
Mpaka hapo ulipoishia ni kuwa message yako inalenga kwenye udini..! acha udini mkuu na propaganda za chuki dhidi ya muislamu na mkristu.
REJEA.

Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyasa Muislam?” Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa naponzwa na dini yangu.
Broo.. kama umesoma freshi masuhala ya udini yapo pembeni ila ukikurupuka utaona ni udini.. kila nafsi hujitetea yenyewe kutokana na mkasa inayokutana naoo.. hii ni hadithi fupi ya maisha yake na fikra zake alizieleza kwa wahusika pale paleee
 
Acha u.pu.m.bavu....majitu yanayoshindwa hoja yaananza vitisho..nani kakwambia Mohamed ni binadamu maalumu zaidi ya wanadamu wengine?

Hoja ndio zigombe,sio mnaleta vitisho vya kikoloni ku-suppress free speech."We" ni mtu na sio tusi,msilete udikteta maandazi.
Kwa waungwana wa mwambao mtu mwenye heshima yake haitwi 'we' na hivyo ndivyo tulivyofundishwa tangu tukiwa wadogo.
 
...
Liza...
Hilo neno, ''chokochoko,'' lilisemwa na Nanren ambae ndiye niliyempa jibu
hilo nililoweka hapo na wewe ukalisoma.

Sijakukusudia wewe ndugu yangu.
Ukirejea kusoma tena utaona.

Huyu Salum Abdallah bibi zangu wakisema kuwa ule, ''wazimu,'' wake umewaruka
wanae wote umenikumba mie.

Huyu mtu ana mengi bwana katika struggle ya Tanganyika maana yeye kapambana
na Waingereza toka enzi za African Association 1929.
Basi amani itawale mkuu.

Nitamfuatilia kiundani zaidi mtu huyo
 
Bihampupile,
Nakushauri usome mwanzo hadi mwisho wa kisa hicho khasa nini
kilitokea pale Chuo Kikuu Cha Ibadan.
Yaaani story yko ndg ni nzr na inamafundisho mzr umeharibu ktk kujitetea kwako,,

Hukupaswa kuchanganya Udini ktk Utetezi wko,, bali ulipaswa kusimamia ktk KWELI yako tu kwamba nina hakika kwamba sijameza mihadarati na hata mizigo yko pia ni KWELI tupu haina mihadarati,,

Vatcan hapo yann ktk Utetezi wako?
 
Yaaani story yko ndg ni nzr na inamafundisho mzr umeharibu ktk kujitetea kwako,,

Hukupaswa kuchanganya Udini ktk Utetezi wko,, bali ulipaswa kusimamia ktk KWELI yako tu kwamba nina hakika kwamba sijameza mihadarati na hata mizigo yko pia ni KWELI tupu haina mihadarati,,

Vatcan hapo yann ktk Utetezi wako?
Bihampupile,
Soma vyema.

Hapajakuwapo na chochote cha mie kujijitetea.
Nijitetee kwani nilikuwa nimeshtakiwa kwa kosa gani?

Lilikuwa swali la kweli wa hoja yangu na mantiki.
 
Kwezisho,
Siku ile niliomba nipate faragha niswali.
Walinipatia Alhamdulilah.

Nililia na Allah katika sijda kuwa aninusuru kama alivyomnusuru
Issa bin Maryam kuuliwa na Wayahudi.

Alhandulilah Allah SW alipokea dua zangu.
Angalia hapo chini nini kilitokea:

Sasa hapo ikawa nimelipata jingine. Kumbe wauza unga hawakamatwi hadi amri itoke juu. Sasa kama amri haikutoka ndiyo muuza unga atapita aingize sumu zake mitaani? Hili likazidi kunidhihirishia kuwa kukamatwa kwangu hakukuwa na uhusiano wowote na vita dhidi ya mihadarati bali ni vita vile vile vikongwe dhidi ya Uislam.

Nikawa pale usiku kucha. Sasa wakati niko pale wakidhani nimelala. Wakawa wenyewe kwa wenyewe wanazungumza kuhusu hii ‘operation’ neno walilotumia ni kuwa 'leo tume-dial wrong number.' Wakawa wanasema, “Huyu bwana mbona hakuelekea kama muuza unga tena huyu mtu bwana kasoma kweli kweli” Wanadhani mie nimelala kumbe ni macho nawasikiliza. (Vipi utalala katikati ya michongoma?). We umeona jinsi alivyokuwa akijibu na kuchambua mambo.” Hilo ndilo likawa gumzo lao wakinisifia kwa ufasaha na mantiki lakini wakizungumza kwa sauti ya chini kabisa. Hapa ikanidhuhirikia kuwa hawa vijana walikuwa wanatimiza wajibu wao wa kazi tu lakini kiini khasa cha kukamatwa kwangu hawakuwa wanakifahamu.

Walionikamata walikuwa vijana kama wanne na wote walijitambulisha kwa majina ya Kiislam. Nilijua ni waongo kwa kuwa Muislam anonekana katika uso na katika matumizi ya lugha. Ila kitu kimoja lazima nikiri. Wale vijana walikaa na mimi kwa wema na hawakunibughudhi hata kidogo. Hata nilipokuwa nakwenda msalani kijana alienisindikiza alinitaka radhi akasema, ”Nakusindikiza kwa sababu ni sheria lakini sisi tunakustahi kwa hiyo utuwie radhi kwa kukufuta hadi msalani.”

Asubuhi wakubwa wakaja kazini lakini hakuna alienikabili. Walikuwa wakinichungulia kutoka mlangoni kama simba ndani ya kizimba kwenye zoo, nami nikawa najifanya siwaoni. Ndipo akaja mkubwa mmoja tena akaniita kwa jina langu na kwa heshima na bashasha sana, "Bwana Mohamed tuwie radhi sana pamekuwa na makosa kidogo tuwie radhi sasa hivi tutakuruhusu uende nyumbani. ” Akatoka nje akawa akipiga simu. Kisha akarudi ndani akaamrisha nibebewe mizigo yangu na gari la polisi linirudishe nyumbani. Kistaarabu kabisa nikakataa gari ile huku nikifanya maskhara kuwa naogopa gari ya polisi asijepiga simu akasema mrudisheni huyo mtuhumiwa. Ofisi nzima ikacheka. Hapo ndipo wale wakamataji wangu wa usiku wakabeba mizigo yangu nami nafuata nyuma tunatoka nje ya uwanja.

Maelezo haya unayatoa mwenyewe, kwamba vijana walikuwa wamekukamata kwa kuhisia kuwa wewe ni zungu la unga.
Lakini bado wewe mwenyewe katika simulizi zako unataka kuwaaminisha "your unsuspecting followers" kwamba ulikamatwa kwa sababu ya dini yako.
Hii si kutaka kufitinisha umma kweli?
 
Nanren,
Unakumbuka siku nilipokuhadithia historia ya babu yangu Salum Abdallah?

Nilikuambia uwe unafanya utafiti kabla ya kuandika.

Katika mkasa huu nakushauri urejee kukisoma kisa.

Walinikamata walinifahamisha, baada ya uchunguzi na kuridhika kuwa nauza unga.

Rudi kisome kisa upya.
 
Ni kweli shehe wakati mwingine waweza kamatwa either Kwa kukufananisha inatokea hivo na wajiridhishapo sio huwa wanakuachia,km ulivoachiwa na kuombwa radhi,pia elewa we ni Mtanzania huwezi tendea jambo kwa uso hatia nalo.Labda hoja yako kuu ni ipi, kushikiliwa sababu u muislam? wasio waislamu pia ushikiliwa rejea kumbukumbu zingine,Pia uthibitisho wa kujua sio waislamu zaid km ungeomba wakuonyeshe vitambulisho vyao usadiki majina yao, pia sidhani km ni njia nyepesi kuwatambua waislamu wote kwa Lafudhi zao kumbuka kuna wa mwambao na wa bara lafudhi haziwezi fanana.
Pia huyo Khomeini,wakina Shah nk wadhamini wao wakuu ni America, rejea habari za uchunguzi za historia ya taifa la Irani na mapinduzi yake na pia km muimili mkuu kwa ustawi wa America na jinsi ya kuitawala middle east.
 
Ni kweli shehe wakati mwingine waweza kamatwa either Kwa kukufananisha inatokea hivo na wajiridhishapo sio huwa wanakuachia,km ulivoachiwa na kuombwa radhi,pia elewa we ni Mtanzania huwezi tendea jambo kwa uso hatia nalo.Labda hoja yako kuu ni ipi, kushikiliwa sababu u muislam? wasio waislamu pia ushikiliwa rejea kumbukumbu zingine,Pia uthibitisho wa kujua sio waislamu zaid km ungeomba wakuonyeshe vitambulisho vyao usadiki majina yao, pia sidhani km ni njia nyepesi kuwatambua waislamu wote kwa Lafudhi zao kumbuka kuna wa mwambao na wa bara lafudhi haziwezi fanana.
Pia huyo Khomeini,wakina Shah nk wadhamini wao wakuu ni America, rejea habari za uchunguzi za historia ya taifa la Irani na mapinduzi yake na pia km muimili mkuu kwa ustawi wa America na jinsi ya kuitawala middle east.
Kenstar,
Inawezekana hujakielewa kisa.
 
Seikh Mohamed Said waama ni kisa cha aina yake..
 
kupewa kesi za kupandikizwa n kawaida sana hapa tz ila usihisishe kabisa na maswala ya kidini

tz hamana hayo mambo ya uislam au ukristo ndio kwanza nnasikia kwako
labda nchi kama marekani hayo mambo ndio yapo

usijaribu kupandikiza chuki za kidini kwa watu vita yake mbaya kuliko baa la njaa

narudia tena usipandikize chuki za kidini kwa watu ni mbaya kulikonunavyofikiri
 
Back
Top Bottom