Nanren,
Tofauti kubwa kati yako na mie ni kuwa hawa niwaaandikao nawajua vizuri
na nayajua ambayo wewe huyajui hata kidogo.
Ndugu yangu wewe kifua kinakufukuta kwa joto ukiwasoma hawa.
Mimi ninapowaandika hawa moyo yangu unapata utulivu kwa kuwa nimekamilisha
lile wengi walilokuwa wakiniambia nitimize baada ya kuwahoji.
''Mohamed haya yasiishie katika makaratasi uandike historia yetu isije ikapotea,''
walikuwa wakinambia na baada ya hapo wataniombea dua.
Sikuandika uchochezi wowote lakini nitaeleza yaliyotokea 1962/63 kati ya
Abdul
Sykes, Dossa Aziz, Mwalimu Kihere na
Julius Nyerere.
Nanren,
Hebu pitia hapo chini kwanza kabla hatujaendelea mbele:
Jackline,
Abdul Sykes na
Dr. Kleruu walianza kuandika historia ya TANU 1962/63
baada ya mazungumzo kati ya
Abdul Sykes,
Mwalimu Kihere na
Dossa
Aziz.
Aliyekuja na fikra hii alikuwa
Mwalimu Kihere na
Nyerere akaunga mkono
na yeye ndiye aliyesema
Abdul aandike kwa kuwa yeye anajuwa mengi
kutokana na historia ya baba yake
Kleist Sykes, kuwa muasisi wa African
Association.
Abdul Sykes akajitoa baada ya kumdhihirikia kuwa kilichokuwa kinatafutwa si
historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Dr. Klerruu alikamilisha ule mswada lakini kitabu hakikuchapwa hadi hii leo.
Inasemekana huu mswada na baadhi ya yale ambayo
Abdul aliyoandika upo
katika maktaba ya CCM mahali fulani hakuna ajuaye wapi.
Hata hivyo kuna mwana TANU mmoja katika vijana wa Youth League aliuiba
huu mswada akabadilisha hapa na pale na kuchapa kitabu kwa jina lake alichokiita
historia ya TANU.
TANU walimuonya asichape tena kitabu kile.
Kitabu hiki mimi alinipa baba yangu na naamini kilimvunja moyo sana kwa yale
aliyokuta mle kwani yeye aliiona TANU ilivyoanza toka ile siku ya kwanza kwani
Abdul Sykes alikuwa rafiki yake wa karibu sana toto utoto wao.
Kitabu hiki hakina tofauti kubwa sana na kile kitabu cha Kivukoni College, ''Historia
ya TANU.''
Ikawa sasa kama imewekwa sheria fulani kuwa ni marufuku mtu kuja na historia
ambayo haitaanza na
Mwalimu Nyerere.
Ikawa hata inaposemwa kuwa
Nyerere alichukua uongozi wa TAA mwaka wa 1953
haielezwi kachukua vipi na kachukua kutoka kwa nani.
Ikawa kwa njia hii jina la
Abdul Sykes halitajwi.
Ikawa vilevile ni mwiko mkubwa kueleza historia ya Waislam katika kuunda TANU na
kupigania uhuru wa Tanganyika kiasi mwaka wa 1988 gazeti la Africa Events (London)
toleo zima lilikusanywa kwa mimi kule kumtaja
Abdul na
Ally Sykes,
Saadan Abdul
Kandoro,
John Rupia na mchango wa Waislam katika kuasisi TANU.
Nanren,
Ikiwa mie kuiandika historia hii ni uchochezi basi hii ni bahati mbaya sana kwako.
Sasa TANU ilipoamua kuandika historia yake katika jopo la uandishi alikuwapo
Hassan
Upeka.
Upeka alileta katika jopo lile ''notes,'' alizoziandika kuhusu vipi TANU iliasisi wa kutokana
na mahijiano aliyofanya na
Abdul Sykes kabla hajafa 1968.
Jibu alilopewa
Upeka ni kuwa historia hiyo inayoandikwa haina uhusiano wowote na
Abdul.
Hizi habari kanieleza
Upeka mwenyewe.
Hivi ndivyo historia ya TANU ilivyoandikwa na
Abdul Sykes na mdogo wake
Ally na wazalendo
wengine wakawa kwa khiyana tu wamefutwa.
Haiwezekani kuwa
Abdul Sykes jina lake lilifutwa katika historia ya TANU kwa kuwa alikuwa,
''mchochezi.''
Africa Events lilipopkea makala yangu wakaichapa katika gazeti la March/April 1988 uk. 37 - 41.
Nilichosema katika makala ile ni kuwa haiwezi kukamilika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika
bila kueleza mchango wa Waislam na kuwataja watu kama
Abdul Sykes na mdogo wake
Ally,
Saadan Abdu Kandoro na
John Rupia.
Makala hii iliwashtua wengi na matokeo yake ndiyo huko kukusanywa gazeti lote na kuchomwa moto.
Wasomaji ndiyo wataamua kama huo ni uchochezi au la.
Kuna mengi yalifuatia baada ya kituko hicho.
Kwa sasa na tusimame hapa.
Kushoto: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdul Sykes na Lawi Sijaona
siku ya kumuaga Nyerere Ukumbi wa Arnautoglo safari ya pili UNO 1957 .
Nanren,
Hayo mengine wala sina haja ya kukujibu.
Nakuacha uungue kwani maradhi ya hasad shida kupona.