Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Mohamed Said ''Mzungu wa Unga,'' 2007 Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere

Ki usema ukweli hipo hivi wenye MOHAMED SAID MOHAMED wengi sana wapo kwenye list ya wauza madawa ya kulevya na wengi wao ndo wale waarabu koko wapo kwenye kundi la watch list kwenye mitambo na system za uwanja wa ndege na mipakani so yawezekana walivyoingiza passport yako ikamatch jina so uliingizwa kwenye chumba kuhakikiwa kuwa we ni mmoja wapo?
Wenye jina MOHAMED kiukweli hata huku mtaani ni wajanja wajanja fulani hivi(JARIBU KUCHUNGUZA NYENDO ZA WATU WENYE JINA MOHAMED)
 
CDF mabeo alikuwa na cheo na muumini mkubwa na pia alikuwa mwenyekiti wa parokia ya segerea kama sikosei so kuwaaga ni kuwa anaachana na hiyo nafasi rasmi na kuanza kutumika rasmi tena kwa asilimia 100% kama mkuu wa jeshi sasa kuwaaga ni dhambi kama alikaa nao vizuri afanyaje.Na je kama anaamini hata hiyo nafasi imesababishwa na maombi ya waumini wenzake asiwaage? WAISLAM MSIWE MNATAFSIRI MATUKIO KATIKA MLENGO WA KUSHOTO TU ACHENI KULALAMIKA PIGENI kazi
 
Antonio,
Ahsante.
Huo ni uwanja mwingine ambao singependa kuingia kwa sababu zilizo wazi kabisa.

Naingia Maktaba In Shaa Allah nimepata kutoa mada Chuo Kikuu cha Johannesburg katika maeneo hayo labda utaweza kupata kitu.
Kwakua hujataka tujadili haya Hakuna shida
Antonio,
Tafadhali hebu soma hii mada nimeeleza historia ya mijadala ya aina hii
ilivyo tatanishi:
Mohamed Said: THE LEGACY OF SHEIKH AHMED DEEDAT (1918 - 2005)
 
Mtu...mbona mimi sikutukani nakujibu kiungwana?

Nini kinakughadhibisha kiasi hiki?
Huu ni mjadala tu tujadiliane kwa nia ya kufahamishana matatizo katika jamii yetu ambayo kwa hakika tunayo ili ipatikane njia ya kuyaondoa.

Matusi yatatuvurugia mjadala wetu.
Nilikufahamisha kuwa "munafiqun," si sawa "grammatically."

Neno lenyewe pia unalitumia sivyo.
Tafuta mtu akuelekeze.
 
Billie,
Labda hujanisoma vizuri.

Walionikamata hawakunikamata kwa jina bali kwa kitambulisho maalum passport yangu na wakaniambia niitambue.

Nami niliwauliza kwani hawafanyi uchunguzi?

Nikajibiwa wanafanya uchunguzi na ndiyo maana nimetiwa mbaroni.

Rejea kusoma upya.
 
Antonio...mimi nakuhurumia wewe kwani nina hakika kama umesoma hiyo paper ushatambua kilicho mbele yako.

Mimi natafiti na kuandika "audience " yangu ni dunia nzima.

Mwenzangu wewe unalenga JF.

Hii paper niliombwa baada ya kusikika pake University of Johannesburg na nikaitoa tena Islamic Propagation Centre International (IPCI)Durban na nilifanya hivyo.

Hii ni taasisi aliyoasisi Sheikh Ahmed Deedat wakati wa uhai wake.
 
Kidudukuntu mbona unamkwepa Sivalon ikiwa wewe hakika ni mkweli na mpenda haki na uadilifu?

Au tusema post imekupita na wala hujakisikia kitabu hicho kilichochapwa Ndanda Peramiho 1992?
 
Billie Sivalon katika kitabu chake kaweka takwimu zote kuhusu hilo.

Tafuta kitabu chake usome.
Hili ndilo tatizo la kujadili kitu usichokijua.
 
Mtu...mwendawazimu anazo dalili zaidi ya hizo mojawapo ni kutukana...
 
Antonio...mimi nakuhurumia wewe kwani nina hakika kama umesoma hiyo paper ushatambua kilicho mbele yako.

Mimi natafiti na kuandika "audience " yangu ni dunia nzima.

Mwenzangu wewe unalenga JF.
Hii paper niliombwa baada ya kusikika pake University of Johannesburg nikaitoa tena Islamic Propagation Centre International (IPCI)Durban na nilifanya hivyo.

Hii ni taasisi aliyoasisi Sheikh Ahmed Deedat wakati wa uhai wake.
Mkuu hiyo huruma yako kwangu ndio maarifa yangu au ndio uelewa wangu. No matter unafanya hizi kwa dunia au tz tu. Ninachosema ni hiki maarifa ya kweli yatoka kwa Mungu. So Kati ya Mungu wako na Mungu wangu ninae mwamini ni yupi aweza kua Mungu WA kweli mpk akatupatia maarifa thabiti?

Kumjibu mtu kwamba apitie makala au tafiti ulizoandika na kuandaa miaka mingi huko ni kukwepa hoja
 
Ndugu zangu,
Mambo haya hapo chini ndiyo yaliyonifanya nikawa maarufu humu JF
ingawa yaliwashtua wengi na wengi walighadhibika.

Hawakupenda waamini kuwa kile walichidhani ndiyo historia ya uhuru wa Tanganyika
sicho:

Mohamed Said: UHURU DAY: TUWAKUMBUKE MASHUJAA WA UHURU WA TANGANYIKA

Unajua historia ya hawa wazalendo hapo chini pamoja na ya Baba wa Taifa kwa dhahiri
yake?

Vipi alijuana na Idd Faiz Mafungo Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagamoyo, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu?

Umapatapo kuona au kusoma popote kuhusu wazalendo hawa waliopigania uhuru wa Tanganyika?

IDD%2BFAIZ%2BMAFUNGO.JPG

Kushoto: Idd Faiz Mafungo (Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya) Mratibu wa safari ya Baba wa Taifa UNO 1955,
Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagamoyo, Julius Kambarage Nyerere, Abdu Kandoro na Haruna Taratibu Dodoma 1956.
 
Antonio...vipi utajua usiyoyajua ikiwa husomi tafiti? Sijipigii zumari lakini hapa JF nimewafunza wasomaji wangu mengi ambayo walikuwa hawayajui katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Mimi ndiyo niliyoweka hadharani Nyaraka za Sykes zilizoeleza historia nzima ya Waafrika katika jitihada za kujikomboa.

Mimi ndiyo niliyowaleta wazalendo waliokuwa bega kwa bega na Baba wa Taifa katika kuijenga TANU watu ambao historia iliwasahau kabisa.

Haya yote nimeweza kuyafanya na kuwaelimisha wasomaji wangu kupitia utafiti.

Nimeweza kupitia utafiti kushirikishwa na kazi zangu kuchapishwa na Oxford University Press Nairobi na New York na kazi hizi zimetoa mwanga mpya katika historia ya nchi yetu.

Sasa unapoogopa kusoma...
 
Mtu...mbona mimi sikutukani nakujibu kiungwana?

Nini kinakughadhibisha kiasi hiki?
Huu ni mjadala tu tujadiliane kwa nia ya kufahamishana matatizo katika jamii yetu ambayo kwa hakika tunayo ili ipatikane njia ya kuyaondoa.

Matusi yatatuvurugia mjadala wetu.
Nilikufahamisha kuwa "munafiqun," si sawa "grammatically."

Neno lenyewe pia unalitumia sivyo.
Tafuta mtu akuelekeze.
Hakuna mahali nimetumia hilo neno
 
Antinio...vipi utajua usiyoyajua ikiwa husomi tafiti? Sijipigii zumari lakini hapa JF nimewafunza wasomaji wangu mengi anbayo walikuwa hawayajui katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Mimi ndiyo niliyoweka hadharani Nyaraka za Sykes zilizoeleza historia nzima ya Waafrika katika jitihada za kujikomboa.

Mimi ndiyo niliyowaleta wazalendo waliokuwa bega kwa bega na Baba wa Taifa katika kuijenga TANU watu ambao historia iliwasahau kabisa.

Haya yote nimeweza kuyafanya na kuwaelimisha wasomaji wangu kupitia utafiti.

Nimeweza kupitia utafiti kushirikishwa na kazi zangu kuchapishwa na Oxford University Press Nairobi na New York na kazi hizi zimetoa mwanga mpya katika historia ya nchi yetu.

Sasa unapoogopa kusoma...
In fact siogopi kusoma ila nachoweza kusema duniani kote ktk history kuna mambo mengi. Kuna history za zidumu fikra za mwenyekiti na history za upande wa pili ambazo ndio zenye ukweli.

Hili haliko tu tz ni dunia nzima so ktk hilo sioni hoja ya msingi sn muzee...

Km utanipatia mail yako nitakutumia vitu vingine uongeze ili uwe vzr zaidi lkn so far bado uko nusu nusu though you think you are on top....
 
Kipi kikufanyacho useme kuwa mimi nadhani ni bingwa?
Kuwa niko nusu umenipaza.

Mie bado mwanafunzi ndiyo kwanza naanza alifu kwa kijiti.

Itakuwa bora hivyo vitu uviweke hapa jamvini ili sote
kwa pamoja tufaidike.

Tukamilishe kile Maalim Faiza anakiita ''Elimu bila Khiyana.''
 
Back
Top Bottom