Mohammed Dewji ajiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya simba, amteua Salim Abdallah (Try Again) kuchukua nafasi yake

MO dewji anapenda sana yeye kuwa centre ya kila kitu pale simba na chakushangaza zaidi yeye ana asilimia ndogo za Umiliki ila kila maamuzi ya timu yanatoka kwake tofauti na wanachama wenye hisa nyingi
Hela mwanaharamu anawageuza geuza anavyotaka
 
Kwahyo anataka abembelezwe?
Asuse tu asitichoshe na yeye bana
 
Naona humu watu wanajibu kikejeli eti km akiondoka aondoke tu.
Hususan wanawake,wanawake wanaongeaga tu kwa hisia zao za kike aiseeeh.
Mnashindwa ng'amua kwamba katika historia simba haikuwahi kufanya vizuri ukiondoa misimu ambayo Mo dewji amewekeza simba.
Asa aondoke huyo tuone km mtatambaa km mtambavyo.
 
Ila boss Wang huyu nae anapenda ku trend Hiv kwa situations club inavopitia alafu anakuja kusepa upuuz huu inawezakana n kweli ameona ametingwa na majukumu yake pia ishuu ya FCC kwa kuondoa tension kwa nn asinge step kimya kimya tu
Amezingua huyo manara alivomchamba kuhusu kupenda ku trend alikuwa sahihi
 
Kila lenye mwanzo Lina mwisho wake kikubwa ni kuweka misingi ya uendelevu

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Mo amebwaga manyanga huku kaweka hela zake?
MO ameipandisha timu ya Simba thamani kwa fedha nje ya mkataba na kaweka mzigo 20 b (kamanikweli) akaweka na CEO wake. Akiendelea kukaa pale alipo kimkakati Inabidi aendelee kumwaga mihela maana timu iki kwama wote Wana mkimbilia yeye.
Anachofanya sasaivi kwakua amesha weka mtaji 20b( Kama ni kweli) ndio maana ana mshinikiza Barbara aingize fedha kwa kuingia mikataba mbalimmbali ata ya ki pimbi ili kimahesabu Klabu ionekane imeingiza faida na shereholders waanze kugawana faida(gawio) kwa muda walio kubaliana.
Maana yake fedha zote zilizo ingia baada ya 20b kuwekwa, mfano mauzo ya wachezaji nisehemu ya faida, mikataba yote inayo ingiwa Sasa atapata gawio. Ali ugomea mkataba wa Azam kwakua kimsingi asinge faidika kwakua mzigo 20b ambao ni sehemu ya mtaji alikua ajauweka.
Sasa naamini kwakua amesha jitoa Ila amemwacha mwakilishi bwana Try again ule mkataba wa Azam, Simba wata u sign na faida itakua ya Pande zote yaani Klabu na mwekezaji. MO ni mwelevu kuliko mbumbumbu wengi.
Kwa Sasa itakua ngumu kwa watendaji wa Simba kumfuata MO kumwomba asaidie fedha za safari, bonasi na nyinginezo alizokua akizitoa MO nje ya mkataba.
Itabidi Simba wajifunze kuishi kwa budget yao waliyo ipanga mwanzoni mwa msimu. Pesa za Bure zinakwenda kukata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…