Mohammed Dewji: Mchakato wa mabadiliko Simba umekamilika, aweka bilioni 20

Mohammed Dewji: Mchakato wa mabadiliko Simba umekamilika, aweka bilioni 20

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,016
Reaction score
6,759
Mchakato wa mabadiliko Simba umekamilika- Mo - "Time ya Ushindani (FCC) imeshatupa ruhusa, hivyo mchakato wa mabadiliko ya Simba umekamilika, tumepewa vipengele vichache vya kufanyia kazi kama kutoa fedha," - Mohammed Dewji.

====

MWENYEKITI wa Bodi ya wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji "Mo Dewji' leo Ijumaa Julai 30, 2021 amekabidhi kitita cha Sh20 Bilion za uwekezaji wa Simba.

Amesema hanunui hisa asilimia 49 kwa pesa hiyo bali 43 Bilioni.

"Mpaka sasa nimeshalipa Simba zaidi ya Sh21 Bilioni, ukiachana na pesa nyingine za ziada za maandalizi ya msimu, usajili na nyinginezo ninazotoa”

"Mimi nimetoa jasho na machozi kwenye Simba, nimetoa muda mwingi kwa ajili ya Simba, nimepoteza fursa nyingi kwenye biashara zangu kwa ajili ya Simba."

"Sisi tumewekeza na hawezi kutokea mtu akatupa hela ya udhamini, sawa sawa na wenzangu, hili sitakubali. "

"Hakuna mtu mkubwa kuliko Simba, hii timu tumeikuta na tutaiacha, hata mimi nimeikuta."

Lakini kuna watu wanasema Mohammed Dewji hana pesa, leo hii nakabidhi cheki ya Sh 20 Bilioni," amesema.

Alitania kwamba kama akisema pesa hiyo Bilioni 20 tayari ameshaipa Simba na wamemalizana kwenye zile Bilioni 21. Mohammed Dewji amekabidhi kitita cha Sh 20 Bilion za uwekezaji wa Simba.

Dewjii.JPG


=========

Ni wakati sasa wa Simba kugomea Bilioni 20 za Mo na kutaka Thamani ya Klabu iongezwe au kama kuna mwenye Mzigo zaidi Aje.

Anaonekana wzi anagomea wadhamini wengine, kiuhalisia thamani ya simba imepanda. Kama Yanga TV tu ni zaidi ya hizo Bilioni 20 tena kwa miaka kumi vipi kuhusu Brand ya Simba?

Kwa maelezo yake Bil 21 ametumia kwa miaka 4 , mbona hasemi faida aliyopata? . Kama ametumia kwa miaka 4 bil 21 , maana yake hizi 20 zitaisha baada ya Miaka 4 tena!.. Then whats next ataendelea kutoa hisani ya fedha zake? au ataanza kula matunda ya uwekezaji wake?

Anasema ahanunui hisa kwa 20B bali ni 43B, Ipo kwenye mkataba?. Je hizo alizokuwa anatoa kumbe alikuwa anazihesabu. Je zijazo atatoa au atawaambia watumie hizo 20B alizowapa?

Kwa nini Valuation ya Hisa imefanywa kiholela, Na kwa nini hakuna wawekezaji wengine waliojitokeza kupambana kwenye kupata hiyo Dili ya uwekezaji?

Ni strategy za kibiashara ambazo zitaiwezesha Simba kujiendesha na kutengeneza faida toka hizo B20 SABABU hata Mo mwenyewe anaonekana KUPOTEZA PESA katika huo udhamini kwa madai yake.

Kumbuka huu ni mchakato wa Mabadiliko ya uendeshaji wa timu, siyo mchakato wa kumpa Mo Timu. Hii Press ni ya kibabe sana. Inaonekana Simba OG ni kama wamenyongea na wanaendeshwa tu.

KWENYE MAJUKWAA NA USHABIKI SIMBA ISHANGILIE USHINDI KUWAJIBU YANGA KWA HILI
KIBIASHARA NA KIMKAKATI SIMBA IMEPIGWA KWEUPE.

Ifikirie Mwaka 2035 Bado familia ya Mo itakuwa inaimiliki hii klabu kwa 49% hata kama Mo atakuwa hayupo hai. Hizo 20B zitakuwa zimeyeyuka kitambo sana. Naiona Simba na Mo Family wakiburuzana kortini baadaye.
Itakuwa kesi ya: Tuachieni Timu yetu Vs Turudishieni Pesa zetu 49%
 
Aweke mara ngapi!

Wakati katamka wazi kabisa kwamba katika kipindi cha miaka minne amesha tumia billion 21 katika uendeshaji wa club kama Mishahara, posho, nauli, kambi na mengineyo.

Halafu bado mnaulizia billion 20?
 
Utopolo muache kelele sasa au mtafute kelele nyingine kama kawaida yenu, bilioni ishirini zimewekwa tena bado za moto.

Tuliwaambia hizo pesa sio kazi kwa MO ameshatoa zaidi ya hizo kwa timu hamkutaka kusikia.

Sasa ujumbe uwafikie vimbelembele wote kina Oscar Oscar, na Kitenge popote walipo.
 
Kwahiyo thamani ya klabu ya simba bado ni bilioni 20?
Mimi nafikiri thamani ya klabu imepanda tayari, na je, ni nani aliyefanya tathmini ya klabu ya simba na kusema ni hiyo bilioni 20
 
Yaani MO kaokota dodo Simba, Kwasasa Kama kaweka 20b Ina maana waki iingia mkataba na Azam au mdhamini yoyote ana haki ya kugawana kinacho ingia na Klabu ya Simba.

Ndio maana aligomea mkataba wa Azam ili avute muda kwakua alikua hajaweka mzigo 20 b ingekua ngumu yeye kugawana faida ya udhamin wa Azam na Klabu ya Simba.

Maana wenye akili wange piga kelele.
 
Ni jambo jema ila wale pinga pinga lazima watakuja kuponda au kuleta issue zingine,

Wanaweza kusema Bil 20 zimewekwa coz Haji Manara kaondoka.
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom