Hivi karibuni tajiri Mohammed Dewji alipost kupitia tittwer yake kuonesha cheki ya Tshs Billion 20 kuikabidhi klabu ya Simba ikiwa ni malipo ya ununuzi wa hisa za Klabu hiyo kongwe nchini. Ikumbukwe cheki hiyo imekuja baada ya watani wa jadi wa Simba, klabu ya Yanga kuingia mkataba mnono na kituo cha AZAM.
Cheki hiyo inaonesha kasoro zifuatazo.
1.
Hakuna jina la benki wala akaunti ya mlipaji
2.
Hakuna jina la benki wala akaunti ya Klabu ya Simba
3.
Kwenye eneo la mpokeaji hakuna saini kuthibitisha kupokea kitita hiko. Lakini upande wa MO kuna saini
Nimeweka picha ya cheki hiyo ili Thinkers wa JF muweze kuzoom wenyewe na kuona hizo dosari.
Soka letu linaweza kufika mbali sana iwapo wajanja wajanja wakabainishwa na kuwekwa pembeni. Tunahitaji mabadiliko na mipango endelevu kwa ajili ya soka letu...
View attachment 1879675 Dewji akikabidhi cheki
View attachment 1879666