Mohammed Dewji: Sio lazima kuja mjini ndio utajirike

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Msomeni hapa alichosema:

"Vijana wengi tunakimbilia mjini, na takwimu zinaonesha kuwa vijana wengi ambao wapo nje ya Dar es Salaam na matajiri zaidi kuliko waliopo mjini, sio lazima kuja mjini ndo utajirike mimi nilianza kulima katani" - @moodewji

Dewji.jpg
 
Huyu mtu ni kweli alianza kulima kateni ndio akifika hapo alipo au amerithi huo utajiri?
Amerithi utajiri ila kaufikisha mara mbili ya aliporithi. Lakini hili swala sidhani kama la kupinga kwani huko vijijini kuna fursa tele. Leo hii tunaona watu wanalima mazao yenye pesa nyingi kama vanilla. Leo hii tunaona migodi iko vijijini huko kwa hiyo ni sawa anachosema. .
 
Katiba mpya itasimamia elimu Bora kwa WANANCHI wetu Ili waweze kujiajiri WENYEWE na kupata ubunifu wa kutosha katika ujasiria Mali na uthubutu wa kufanya pasipo hofu na uhakika wa masoko wa bidhaa zao!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!!
 
Amerithi utajiri ila kaufikisha mara mbili ya aliporithi. Lakini hili swala sidhani kama la kupinga kwani huko vijijini kuna fursa tele. Leo hii tunaona watu wanalima mazao yenye pesa nyingi kama vanilla. Leo hii tunaona migodi iko vijijini huko kwa hiyo ni sawa anachosema. .
Usilolijua ni kama usiku wa kiza.
 
Kulima mpaka utajirike lazima uwe na mtaji wa kutosha, yeye alilima Katani kwa sababu mtaji wa kutosha ulikuwepo.

Atambue vijana wengi wanaokimbilia mijini hawana mitaji ya kutosha, ndio maana huja mjini kufanya biashara ndogo ndogo za mitaji midogo [ machinga].

Hata kama ukiniambia vijana wajiunge kwenye vikundi ili wapate mikopo /mitaji, bado kuna ukiritimba mkubwa kwenye utoaji wa hiyo mikopo, udogo wa mikopo, na masharti ya mikopo yenyewe, ni baadhi ya mambo yanayowakwamisha vijana vijijini.
 
Hapa Mo anatuongopea. Mo utajiri wake umetokana na kurithi ama kuendeleza utajiri wa babake.

Babake Mo alijitajirisha kwa kuchukua mashamba ya katani ya serikali kama mwekezaji.

Halafu akawa anatumia hati za hayo mashamba kuchukua fedha toka mabenki ya nje. Huku mashamba akiyatelekeza.

Mo asitufanye sisi kuwa wajinga.
 
Hapa Mo anatuongopea. Mo utajiri wake umetokana na kurithi ama kuendeleza utajiri wa babake.

Babake Mo alijitajirisha kwa kuchukua mashamba ya katani ya serikali kama mwekezaji.

Halafu akawa anatumia hati za hayo mashamba kuchukua fedha toka mabenki ha nje. Huku mashamba akiyatelekeza.

Mo asitufanye sisi kuwa wajinga.
Anafikiri watu hawajui au wamesahau.
 
Hapa Mo anatuongopea. Mo utajiri wake umetokana na kurithi ama kuendeleza utajiri wa babake.

Babake Mo alijitajirisha kwa kuchukua mashamba ya katani ya serikali kama mwekezaji.

Halafu akawa anatumia hati za hayo mashamba kuchukua fedha toka mabenki ha nje. Huku mashamba akiyatelekeza.

Mo asitufanye sisi kuwa wajinga.
Ndio maana baadhi ya hayo mashamba aliyokuwa anayatumia kuombea mikopo benki halafu hakuyaendeleza alikuja kunyan'ganywa kipindi kile cha Magufuli.
 
Fuatilia historia ya hayo mashamba ya mkonge ndio utajua.
Hapa si tunazungumzia fursa, sasa mie nimekubaliana na hoja kuwa fursa ziko nyingi huko vijijini. Nadhani kuna mahala hatujaelewana.

Ila pia ningependa kujua hiyo historia ya mashamba ya mkonge, nielimishe na mimi nijue.
 
Kulima mpaka utajirike lazima uwe na mtaji wa kutosha, yeye alilima Katani kwa sababu mtaji wa kutosha ulikuwepo.

Atambue vijana wengi wanaokimbilia mijini hawana mitaji ya kutosha, ndio maana huja mjini kufanya biashara ndogo ndogo za mitaji midogo [ machinga].

Hata kama ukiniambia vijana wajiunge kwenye vikundi ili wapate mikopo /mitaji, bado kuna ukiritimba mkubwa kwenye utoaji wa hiyo mikopo, udogo wa mikopo, na masharti ya mikopo yenyewe, ni baadhi ya mambo yanayowakwamisha vijana vijijini.
Hakuna vijana vijijini, wanakimbilia mijini na waliopo wanaendesha boda boda......EXCUSES, malalamiko, kutaka kufanyiwa mambo, Uvivu na kuogopa kazi ngumu ndio sababu ya vijana kuacha kuyaboresha mashamba ambayo baba na babu zao yaliwapa maisha.
 
Back
Top Bottom