Mohammed Dewji: Sio lazima kuja mjini ndio utajirike

Mohammed Dewji: Sio lazima kuja mjini ndio utajirike

ngoja tuingie chimbo

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Katiba Mpya itasimamia MAFISADI wasiingize Michele na sukari vilivyo chini ya kiwango kama wakati ule miaka ya tisini!!!

Pia itawachukulia hatua kali za kinidhamu WATU kama mtajwa KWA kuhatarisha usalama wa watumiaji KWA faida Binafsi kamaa alivofanya mtajwa kwenye uzi Huu!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
 
Hakuna vijana vijijini, wanakimbilia mijini na waliopo wanaendesha boda boda......EXCUSES, malalamiko, kutaka kufanyiwa mambo, Uvivu na kuogopa kazi ngumu ndio sababu ya vijana kuacha kuyaboresha mashamba ambayo baba na babu zao yaliwapa maisha.
Kwa jembe la mkono utalima heka ngapi kwa miaka mingapi mpaka utajirike kama Mo anavyotaka?

Sikubaliani na sababu zako zote ulizoandika hapo juu.
 
Mo inabidi atulie tu. Watu wana mafaili ya mchezo mchafu wa utajiri wake.
Siwakubali kanjibays lakini kama mm ni kijana mdogo nikatakiwa kusikiliza kati ya anayesema yule alikuwa mwizi/alirithi au muhusika anayesema nilianza na katani nitamsikiliza muhusika. He is +ve na anaambukiza +ve thinking kwa wengine. Kuna fikara zinaongeza idadi ya wazururaji badala ya motisha ya kuchapa kazi.
 
Kwa jembe la mkono utalima heka ngapi kwa miaka mingapi mpaka utajirike kama Mo anavyotaka?

Sikubaliani na sababu zako zote ulizoandika hapo juu.
Ni sawa kukubali kutokukubaliana. Ila kwa jembe la mkono mm nimeshuhudia kikundi cha vijana wakifanikiwa kwa kulima vitunguu.
 
He is +ve na anaambukiza +ve thinking kwa wengine. Kuna fikara zinaongeza idadi ya wazururaji badala ya motisha ya kuchapa kazi.
Kama unataka kupandikizwa positive thinking basi nenda kwa motivational speakers.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Mimi naamini sana anachokisema vijana wengine Dar ni kukimbizana na hela ya kula na kulipia pango ukienda mikoani kuna vijana wanapesa mpaka unajiona mjinga! Nendeni hata Kahama hapo vijana wanapesa na mitaji ya mamilioni! Very true Mr MoDewji!
 
Kama unataka kupandikizwa positive thinking basi nenda kwa motivational speakers.
Kwa umri wangu hakuna motivation itakayonifaa, labda ya mazoezi na kuhakikisha sipati presha na kisukari huko ninapoelekea. Hata hivyo still ningekuwa kwenye nafasi ya kusikiliza nisingeopt wenye fikra kuwa utajiri hauwezi patikana mashambani.
 
Hahahaaaa same here brother. Hakuna motivational speaker anaeweza kunibadilisha maisha yangu kwa umri huu. Labda wale wa lishe bora na mazoezi tu ili nisipate magonjwa yasiyoambukiza huko mbele ya safari. Tupige tizi bro.
 
Hata hivyo still ningekuwa kwenye nafasi ya kusikiliza nisingeopt wenye fikra kuwa utajiri hauwezi patikana mashambani.
Umesikia kilio cha wakulima juu ya ukosefu wa masoko ya mazao Kama korosho, vanila, mahindi (except mwaka huu), mbaazi, pamba, ufuta, chai, kahawa ,n.k.

Kuna tofauti kubwa kati ya kilimo halisi na kilimo cha kwenye makaratasi (ama ushairi). Kwenye makaratasi kilimo ni utajiri.

Mifumo ya masoko na masoko yenyewe Ina shida Sana nchi hii
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Vijana waliokimbilia Mjini wamefanikiwa sana kwenye Tasnia ya Upanya Rodi.
 
Umesikia kilio cha wakulima juu ya ukosefu wa masoko ya mazao Kama korosho, vanila, mahindi (except mwaka huu), mbaazi, pamba, ufuta, chai, kahawa ,n.k.

Kuna tofauti kubwa kati ya kilimo halisi na kilimo cha kwenye makaratasi (ama ushairi). Kwenye makaratasi kilimo ni utajiri.

Mifumo ya masoko na masoko yenyewe Ina shida Sana nchi hii
Sexless kilimo huwa kina hasara nakubali, maparachichi yameliza watu msimu uliopita ila bado katika hivyo vilio kuna watu kilimo kinawatoa kwenye umaskini.
 
Katiba mpya itasimamia elimu Bora kwa WANANCHI wetu Ili waweze kujiajiri WENYEWE na kupata ubunifu wa kutosha katika ujasiria Mali na uthubutu wa kufanya pasipo hofu na uhakika wa masoko wa bidhaa zao!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!!

We jamaa bwana

Watu wanaongea mambo ya maana we unaleta story za alinacha

Inchi gan ya Africa iliwahi kutajirika Kwa katiba mpya?

Kama unashindwa kuwashitaki viongozi Kwa kuharibu katiba hii basi hata hiyo mpya ikiharibiwa utakaa kimya hivyo hivyo
 
Amerithi utajiri ila kaufikisha mara mbili ya aliporithi. Lakini hili swala sidhani kama la kupinga kwani huko vijijini kuna fursa tele. Leo hii tunaona watu wanalima mazao yenye pesa nyingi kama vanilla. Leo hii tunaona migodi iko vijijini huko kwa hiyo ni sawa anachosema. .
Yah baba zao walikuwa wanakaa vijijini huko na utajiri waliupatia huko

Ova
 
Sexless kilimo huwa kina hasara nakubali, maparachichi yameliza watu msimu uliopita ila bado katika hivyo vilio kuna watu kilimo kinawatoa kwenye umaskini.
Ktk nchi yetu hatukupaswa kuwa na hadith za watu kukimbilia mijini ama graduates kukosa kazi kama masoko na mifumo yake ingekuwa mizuri. Lkn imevurugwa makusudi ili matajiri wachache wawndelee kufaidika na maskini kuonja joto ya jiwe.
 
Well sikupingi ila masikini hawapaswi kusubiri serikali au matajiri wawatoe kwenye kuonja joto ya jiwe unless masikini huyo ameshazeeka.
 
Back
Top Bottom