Mohammed Dewji vs S.S Bakhressa

Nailaumu nchi yangu inasera mbovu sana juu ya swala la uwekezaji maana hawa wote wakienda kukopa wanaeleweka na sera zinawalinda [emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
 
Nani kati yao ni mlipakodi mkubwa?

Sent from my GT-I9152 using JamiiForums mobile app
 
huyu GSM nae anakuja kwa kasi yupo ktk cement, construction, real estate, pikipiki, magodoro, mabati, retail na tusioyajua.
Cement sio zake, kachukua tender ya Dangote kuwa msambazaji mkuu nchini
 
Kuna tofauti kati ya tajiri na tajiri kijana,mohamed dewji ni tajiri kijana zaidi Africa sio tajiri wa jumla,tajiri wa jumla Africa ni dangote na kijana tajiri zaidi dunia ni mark mmiliki wa Facebook,vigezo vyao vya umri wa kijana sijajua Bado Ila nafikiri wanaanzia miaka 35 kushuka chini.
 
Wote wameiba viwanda nyetu kwa msaada wa magamba.
 
..Vyanzo vya fedha zao ni tofauti,dewji huwezi kuona maana anaInvest katika resources i.e steel unlike bakhresa ambae ameinvest in vyakula
 
Mo kafanya investment kubwa sana ndani na nje na karibia kila sekta kawekeza kwenye mawasiliano,kilimo,vinywaji, Chakula ,nishati nk
 
Biashara kubwa ya bakhresa ni ngano na vinywaji tu. Otherwise hana tofauti na warabu wenzie wa kariakoo. Over
 
Habari wakuu, mo dewji ameridhi kampuni ambayo ilikuwa ni ya baba yake, na kipindi ambacho baba take alikuwa anafanya biashara mo dewji alikuwa anasoma nje ya nchi, ( england, UK ) alipomaliza masomo yake akaamua kuendesha kampuni ya baba yake ikiwa ni kuweka share kwenye bidhaa za azam Bakhresa, na wakati huo alikuwa mbunge wa singida, katika share hiyo aliyeweka na bahresa, mo dewji alishangia kwa asilimia 75% na huku said salim Bakhresa alichangia kwa asilimia 25% na baada ya mo kustaafu ubunge na kuamua kusimamia biashara yake, alionekana yupo juu kibiashara na ni kwa mapema mno kuwa tajiri Mkubwa na kumpiku bakhresa asilimia kubwa ya watanzania na afrika mashairi huamini Bakhresa ndio tajiri wa kwanza katika kanda hiyo afrika mashairi lakini si kweli, na bidhaa za mo ziliandikwa azam kipindi alipoweka share, hii ni kuifanya bidhaa inunuliwe kwa haraka, hii ndio siri ya no dewji mwenye miaka 42 kuwa tajiri Mkubwa afrika ya mashariki na huku Bakhresa mwenye miaka 66 akishika nafasi ya tatu........
Kiukweli share katika biashara inalipa endapo utakuwa makini, vile vile share inaweza kukutia umaskini kama ukiwa mzembe, kila kitu kina faida na hasara.......
 
Mfano mzuri ni ule wa p.diidy alivyoweka share kwenye kampuni ya kinywaji cha CIROC VODKA mwaka 2007, share yake ilikuwa asilimia 50% lakini ameweza kukomaa na kupambana kwa nguvu zote kusudi aweze kuona mafanikio na hatimaye alimefanikiwa mwaka 2012 CIROC VODKA ni kinywaji ambacho kilimpa mafanikio makubwa na kuweza kufungua biashara zingine ikiwemo BAD BOY RESTAURANT, SEAN COMBS SHOES, DELLON TEQUILA, BAD BOY RECORDS STUDIO, hii inaonesha jinsi gani share ilivyo kuwa na mafanikio makubwa endapo utakomaa na kuwa makini, ukiangalia upande wa jay z ni mwanamuziki aliyepata fursa ya kumiliki biashara Nyingi lakini bado hajaweza kufikia kiwango cha p.diddy, jay z alinunua kampuni ya nguo kutoka kwa rafiki yake Damon dash, inaitwa ROCA WEAR, mwaka 2003, akaweka share na kampuni ya wine inayoitwa ACE OF SPADE, pia akamiliki studio kwa pesa zake mwenyewe baada ya kuona mafanikio kwenye kampuni mbili za mwanzo ( Roca wear, ace of spade ) ROC - A - FELLA STUDIO, DEF JAM RECORDS, na ROC - NATION, pia amenunua timu ya kikapu marekani inayojulikana kama BROOKLYN NET NEW YORK, pamoja na kumiliki kampuni zote hizo anamiliki dollar 560 U$D, na p.diddy anamiliki dollar 730 U$D,
Je ? Wajua ni kwanini jay z anapenda sana kutumia neno ( ROCKAFELLA )
Je? Hili neno lina maana gani haswa, tukutane siku nyingine ili niweze kufafanua kwa undani zaidi kuhusu jina hili la ROCAFELLA.
 
Nadhani Kinachomshusha Bakhressa Ndani Ya Miaka Hii Miwili Ni Kwasababu Amewekeza Pesa Nyingi Kwenye Baadhi Ya Miradi Ambayo Haijaaza Kumlipa.
Kwani utajiri wa FORBES unaangalia fedha unauyoingiza tu au thamani ya uwekezaji wako na pesa uliyonayo?
 
Mo atafanya sana biashara za kimataifa, nimsafirishaji mkubwa wa mazao ya nafaka katika nchi za magharibi na asia, kuna wakati alisema katika biashara ya mkonge anapata faida zaidi ya 200%, yuko na stock nyingi za commodities .
 
Bakresa bidhaa zake ni kubwa jinga vingi hazina thamani, Mo bidhaa chache zenye thamani energy, real estate, mining n.k.
 
Hapo cjaelewa coz tunaambiwa bakhressa ndio mfanyabiashara no 1 anaelipa kodi tanzania baada ya kiwanda cha bia je huyo Mo na hayo makampuni yake 42 ni mlipa kodi no ngapi
 
Bakresa bidhaa zake ni kubwa jinga vingi hazina thamani, Mo bidhaa chache zenye thamani energy, real estate, mining n.k.
Kama MO, MENGI, SSF, GSM et al hawawezi kutoa kauli kama yako kwa BAKHRESSA, basi we utakuwa JUU ZAIDI YAO HAO WOTE!
 
naomba ufafanuzi kidogo mkuu hapo kwenye share na ambavyo yaweza kukunufaisha au kukufirisi,,,
 
MO ni tajiri zaidi. Anamiliki biashara za aina nyingi sana kuanzia real estate hadi manufacturing industry
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…