Mohammed Dewji vs S.S Bakhressa

Kuna siku nimeenda duka moja mjini apa dom kununua home theater,,nataka kulipa kwa cheque nikaambiwa andika jina Mohamed interprises..nilishangaa sana huyu jamaa anawezaje kumanage adi vitu vdogo ukiachia mbali more than 40 sub companies he had..
 
huyo mo ni wakuchunguzwa anatupiga sana kama ni kweli ndio tajiri no.1 afrika mashariki na anamiliki kampuni zaidi ya 42 nchini na zinafanya vizuri hivyo kwanini azidiwe kulipa kodi na mwenye kampuni 13 tu?
 
Hapo cjaelewa coz tunaambiwa bakhressa ndio mfanyabiashara no 1 anaelipa kodi tanzania baada ya kiwanda cha bia je huyo Mo na hayo makampuni yake 42 ni mlipa kodi no ngapi

Kutokana na biashara yake ni lazma alipe kodi kubwa..but mo dewji ana investment ambayo kimcng kodi haiangaliwi sana eg real estates
 
Mo anapesa za kurithi na Bakhresa anapesa yake hio ni moja ya sababu.
 
Mo ana product nyingi za mchanganyiko mpaka balaa ndugu zangu nachokijua anauza kuanzia mishumaa,utambi,kandili bicycle phoenix,vibiriti,sabuni,mafuta ya kula na makorokoro kibao
huyu Mo ni nouma sana kila takataka anatengeneza halafu yupo mjini hadi vijijini tofauti na Bakhresa yeye kwenye vinywaji tu wakati mwenzie hadi sisimizi anatengeneza halafu bei sawa na bure
 
huyu GSM nae anakuja kwa kasi yupo ktk cement, construction, real estate, pikipiki, magodoro, mabati, retail na tusioyajua.
Hayo tusiyoyajua ndio yanayomuingizia pesa ya maana
 
1. BAKHRESA = VINYWAJI NA NAFAKA NA BEI IKO JUU

2. MO = VIBIRITI,MISHUMAA,TAMBI,BLUEBAND,DAWA ZA MBU,TUMBAKU,KILIMO,SUKARI,NGANO,SEMBE,MAKAKAO,KAHAWA,NYEMBE


NB: MO YUPO HADI KIJIJINI KWETU,HALAFU HABAGUI KWENYE MASUALA YA KAZI
 
1 BAKHRESA ILI UPATE KAZI LAZIMA UWE MPEMBA NA MUISLAM

2 MO HAKUNA UDINI HABAGUI WATU,UWE NA ELIMU USIWE NAYO KAZI UNAPATA

KWENYE MISHAHARA HAO WOTE HOVYO KABISAAAAAAAAAAA MSHAHARA MKUBWA LAKI NA 20
 
Wadau kuna tetesi Yale malori ya Mo yaliyopigwa moto na waasi kule Kongo ni kwa sababu ya chuki za kibiashara .....? Mo namkubali sana huyo jamaa alivyofanya ubunifu kwenye biashara ya maji ya chupa nilimpigia saluti...very creative

Unamaanisha chuki za wacongo wafanyabiashara towards Mo?
 
Unamaanisha chuki za wacongo wafanyabiashara towards Mo?

Exactly mkuu....ila hiyo nimeinyaka nyuma ya kapeti...nasikia jamaa anawaburuza kinyama pande hzo....almost kila bidhaa essential amecover alafu very cheap
 
Kwani utajiri wa FORBES unaangalia fedha unauyoingiza tu au thamani ya uwekezaji wako na pesa uliyonayo?
FORBES
Ni jarida/gazeti la marekani ambalo linahusiana na masuala ya kibiashara. linatoka kila wiki, hata mwezi.
Jarida hili la Forbes linahusu UWEKEZAJI, PESA, VIWANDA, SOKO LA BIASHARA, MAWASILIANO, TEKNOLOJIA YA KISASA, n.k
Ilianza rasmi mwaka 1917, ikimilikiwa chini ya bwana Steve Forbes na sasa inamilikiwa na Michael Perlis, makao makuu ya Forbes yapo marekani jimbo la new york city,
Forbes sio kwamba wanakaa na pesa bali hawa na ni zaidi ya benki, kuhusu masuala yote ya kibiashara wao wanahusika na ila kuhusu suala la pesa ndani benki huwa wanakadiria ila sio kweli,
Wanasema mengi anamilika dolla 550 million,
Mo dewji dolla 1.2 billion
Diamond platnumz dolla 4 million.
Wao wanakadiria ni kiasi gani pesa ulizo nazo benki kutokana na biashara ulizonazo au kazi unayofanya inakulipa kiasi gani cha pesa........
 
Thanks,nafikiri nilikosea Kiswahili kama wewe ulivokosoea 1917.Nilivoku-quote katika comment yako nilikuwa na maana hao FORBES wanaangalia pesa uliyonayo bank au wanaangalia thamani ya uwekezaji wako mf IPTL mitambo yao thamani yakr ni Bil.300 basi watahesabu utajiri wa mwenye IPTL ni hiyo Bil.300.
 
Mbali na Tanzania huyo MO ana kiwanda nchi gani nyingine?
Manake Bakhresa ana viwanda nchi zote zilizotuzunguka kasoro Kenya na Zambia.
 
nasubiri wajuvi wa mambo waje watiririke kuhusu hili la MO kumzidi SSB kwa utajiri kwa mujibu wa vigezo vya forbes.
Hawa forbes na utafit wao uchwara waende zao sie watz tunafahamu bakhresa ndo tajiri namba 1 tz hata kwa macho ya kutazama tu.Sio kila kitu hadi wazungu watuaminishe bana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…