Share maana yake nikufanya biashara au kazi kwa pamoja baina ya watu wawili au zaidi, au inaweza ikawa kampuni moja au zaidi ya moja, ili kupata manufaa na faida zaidi pia ni kuleta maendeleo na kupiga hatua katika hiyo kazi mnayofanya.
Mfano:
Michael ameweka share na kampuni ya Maji ya Kilimanjaro na wameandikishiana mkataba, makubaliano yao ilikuwa share iwe asilimia 50% kwa 50% kwa hiyo michael atahakikisha Maji ya Kilimanjaro yanakuwa safi na salama, chupa iwe ya kuvutia, Maji ndani yake iwe ina ladha safi na matamu kwa kunywea kila rika, yawe yanapatikana nchini kote Tanzania na hata nje ya nchi, kwahiyo kama kwa siku unauza katoni 200 kila aina ya chupa ya Kilimanjaro nina maanisha robo Lita, nusu Lita, Lita moja, Lita moja na nusu, Lita mbili, mpka Lita 10 au 12.........
Kwa hiyo mwisho wa siku unaangalia umeuza katoni ngapi na kila moja na bei yake jumla, kwa hiyo kama utapata million 50 kwa wiki ina maana kwamba utamlipa mwenye Maji ya Kilimanjaro shillingi 25 million,
Ikitokea umeshindwa kuuza bidhaa yako kwa sababu mbali mbali utakuta kampuni inafilisika na utashindwa kuelewana na mwenye kampuni, mwisho wa siku utakuta umetumia hela Nyingi kufanya hiyo biashara halafu baadhi ya vitu vyako vya thamani vinapigwa mnada kusudi uweze kulipa hela ya mwenye kampuni, kwa hiyo utajikuta umekuwa maskini wa kutupa, au mmoja wenu anaweza kufariki halafu upande mwingine wa ndugu wakataka kuendeleza Mali na ukatokea migogoro mikubwa, na ndugu wakaathirika kwa namna moja ama nyingine.
ZINGATIA HAYA UNAPOTAKA KUWEKA SHARE.
unaweza kuweka share na
Kampuni mbali mbali
Chuoni
Shuleni
Kwenye muziki
Mahotelini
Hospitalini n.k
Ili kuweka share na kuzidi kuyaona mafanikio , kwanza unatakiwa use mbunifu katika biashara yako, wafanya kazi wako wawe na sifa nzuri na zilizoeleweka, bidhaa zako ziwe katika usalama na ziwe safi, location ya kufanya biashara yako iwe ya kueleweka na yenye movement za watu wengi, Wateja wako wapate Huduma kwa muda muwafaka, bei ya bidhaa yako iwe ya kawaida ambayo itamfanya mteja yeyote aweze kuinunua bidhaa yako, kwa kufuata haya biashara yako itaimarika sana na kuweza kuwa juu kipesa. Ukishindwa kufuata haya umaskini utakusubiri.........
Nadhani nimejibu swali lako vyema.