masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Kama ilivyo ada, nimetembelea kwetu Xmas hii ili kuona mandhari na uzuri wa Rungwe, kwetu.
Kilichonisikitisha ni Chivanjee Tea Estate kuanza kufa kwa kukosa matunzo.
Waziri wa Kilimo ndg Bashe aingilie kati haraka, MO aachilie mashamba ya chai kule Jivanjee Chivanjee Tea Estate, Tukuyu.
Mashamba yamekufa na yameotea vichaka. Kazi na vibarua kwa wananchi wa karibu zimepotea.
Ulafi wa kumiliki ardhi na mashamba nchi nzima bila kuwa na uwezo wa kuyaendeleza ,tunaona kwa macho.
Upande wapili mashamba yanayo milikiwa na wakulima pale Kyimbila yako hali nzuri kabisa.
Nimeweka clip zote mbili, Jivanjee Tea Estate iliyotelekezwa na Mohammed Enteprises(MO), Wakulima Tea Estste inayoendelea kutunzwa na wananchi.
Mbunge wa sehemu hii ndg. Anton Mwantona ni bubu, hajui hata kinachoendelea