Mohammed 'Mo' Dewji ametelekeza mashamba ya chai Rungwe, ajira zatoweka

Mohammed 'Mo' Dewji ametelekeza mashamba ya chai Rungwe, ajira zatoweka

Hii si sababu ya kutelekeza mashamba. MO anafanya economic sabotage.
Waziri wa Kilimo ndg Bashe amka toka usingizini.
Kwanini aliuziwa in first place,sababu tija Iko chini kuliko gharama,bustani ni gharama mno Tz,sababu majority ya vitu vinatoka nje
 
Sidhan kama serikal haijui..bas Tu serikal zetu ndo shida..Ilaa pia nadhan pia next time nivizur kuadress kampuni kuliko jina la Mtu
 
Wameshakopea benki kwa shughuli nyingine😂😂😂😂
Mashamba yarudishwe kwa wananchi.
1735800864881.png

Tuna Mbunge wetu naona ni bubu, anaitwa Anton Mwantona, yuko kimya utafikiri halioni tatizo
 
View attachment 3187568
View attachment 3187580

Kama ilivyo ada, nimetembelea kwetu Xmas hii ili kuona mandhari na uzuri wa Rungwe, kwetu.

Kilichonisikitisha ni Chivanjee Tea Estate kuanza kufa kwa kukosa matunzo.
Waziri wa Kilimo ndg Bashe aingilie kati haraka, MO aachilie mashamba ya chai kule Jivanjee Chivanjee Tea Estate, Tukuyu.
Mashamba yamekufa na yameotea vichaka.
Kazi na vibarua kwa wananchi wa karibu zimepotea.
Ulafi wa kumiliki ardhi na mashamba nchi nzima bila kuwa na uwezo wa kuyaendeleza ,tunaona kwa macho.
Upande wapili mashamba yanayo milikiwa na wakulima pale Kyimbila yako hali nzuri kabisa.

Nimeweka clip zote mbili, Jivanjee Tea Estate iliyotelekezwa na Mohammed Enteprises(MO), Wakulima Tea Estste inayoendelea kutunzwa na wananchi.

Mbunge wa sehemu hii ndg. Mwantona ni bubu, hajui hata kinachoendelea
Tarehe 31 nilikuwa Katumba nilishangaa kuona mashamba yaliyikuwa yanapendeza hivi sasa yamevamiwa na vichaka, ushauri hayo mashamba wapewe maliasili ili yatunzwe kama misitu.
 
Tarehe 31 nilikuwa Katumba nilishangaa kuona mashamba yaliyikuwa yanapendeza hivi sasa yamevamiwa na vichaka, ushauri hayo mashamba wapewe maliasili ili yatunzwe kama misitu.
Ni uhujumu uchumi wa MO kwa wananchi wa Rungwe.
Na Wizara ya Kilimo utafikiri haina muwakilishi katika wilaya ya Rungwe, moja ya wilaya inayosifika kwa kilimo.
 
Chai inahitaji matunzo sana, ukizembea kwa miezi kadhaa kuirudisha kwenye hali yake inakuaga ni gharama zaidi.

Hao wakubwa wanapiga parefu saana maana bei wanayomuuzia mwenye kiwanda na kupiga faida ni kubwa sana ukilinganisha na bei wanayowalipa wachumaji na wafanyakazi wengine ni mbingu na ardhi.
 
Ni uhujumu uchumi wa MO kwa wananchi wa Rungwe.
Na Wizara ya Kilimo utafikiri haina muwakilishi katika wilaya ya Rungwe, moja ya wilaya inayosifika kwa kilimo.
Bashe, CCM na serikali yao hawaijui Rungwe, wao wanaijua Geita na Dodoma ambako wanamaslahi nako, wangeijua wasingeanzisha mashamba ya hovyo Dodoma.
 
Hii ndiyo shida ya wawekezaji wajanja wajanja na wababaishaji. Na hapo lazima ameshayawekea dhamana kwa ajili kujipatia mikopo ya mabilioni, kama alivyofanya kwenye yale mashamba mengine!
Mwanzoni na katikati ya miaka ya tisini huku kulikuwa kama paradiso enzi hizo haya mashamba yakiwa chini ya mwekezaji George Williamson (T) Tea Co., Ltd palichangamka sana na uchumi ulikuwa vizuri namkumbuka Mjomba wangu Mwaijande RIP alikuwa dereva wa lori Isuzu Injection TX mambo yalikuwa bambam siku hizi nasikia watu wote almost wamefutwa kazi viwanda vya Msekela na Chivanjee vimefungwa hakuna uzalishaji hata wakulima wadogo waliokuwa wanauza chai hapo kwake siku hizi wameotesha fito. Sad. Waziri Bashe aingilie kati tuuze chai watu wetu waneemeke!
 
Dah atafutwe mwekezaji mwingine kama imeshndikana
 
Back
Top Bottom