kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Kabla hujacomment mawazo ya mzanzibari kwanza ujue ni mzanzibari wa aina gani. Nililojifunza karibu kila mzanzibari mwenye uchotara wa kiarabu atakupa hoja sawa na wale watawala waliyotawala zanzibar wakati wa usultani. Ni mzanzibari mwafrika mtupu na chotara wachache ndio watakuambia furaha ya kukombolewa visiwa hivyo kwa mapinduzi ya 1964 na kuonesha kupenda muungano na ndugu zao wa tanganyika.Kaka Mohammed Said,
Kwanza nakuamkia.
Pili, khutba zako kwenye social media zinaendelea kuwapotosha watu kuhusu mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964. Bila ya mapinduzi haya wengi wetu visiwani leo tungelikuwa wakwezi au wateka maji.
Mapinduzi ya Zanzibar hayakumpinduwa Mzanzibari kama unavyosema wewe. Natumai unafahamu vizuri vipi waarabu kutoka Oman walifika kuitawala Zanzibar.
Wa-Omani waliichukuwa Zanzibar kwa nguvu kinyume na matakwa ya Wazanzibari wenyewe baada ya kumshinda mreno, sasa na wao kwanini wasiondoshwe kwa nguvu? Ni kweli kuwa Wa-Omani walimfukuza mreno kutoka Zanzibar, lakini baada ya Wa-Omani kuwarejeshea utawala wao Wazanzibari, walijifanya wao wafalme wa visiwa hivi.
Kwahivyo, kupinduliwa kwa Wa-Omani katika mwaka 1964 ilikuwa ni muendelezo wa events ambazo wao wenyewe Wa-Omani walizianzisha. Wa-Omani walivivamia visiwa vya Zanzibar kwa nguvu na wakajifanya wafalme na kwahivyo kwa wenyeji wa kizanzibari kutafuta msaada 1964 kutoka kwa wamakonde wa Tanga (kama unavyoeleza) ili kuwaondoa wavamizi visiwani mwao hayafanyi mapinduzi ya Zanzibar kuwa sio halali.
Tanzania tuliwasaidia wapigania uhuru kutoka Msumbiji, South Africa, Zimbabwe, etc. je, ushindi wao sio halali leo kwasababu walisaidiwa na watu kutoka nje? Kumwita jirani yako kuja kukusaidia kumtoa alievamia nyumba yako ni kosa?
Kama Wa-Omani walikuwa wenye nia njema, basi baada ya kumuondosha mreno visiwani wangeliwarejeshea wenyewe Wazanzibari utawala wao na sio wao Wa-Omani kujifanya wafalme kwa nguvu zao.
Eti unasema mfalme wa Zanzibar hata siku moja hajamuuwa muafrika hata mmoja. Are you in your proper senses Sir? Umesahau waafrika walivyokuwa wakikandamizwa kielimu visiwani? Muafrika gani alikuwa akipata nafasi ya kuingia secondary school? Hao akina Jumbe na Ali Hassan Mwinyi sio ilikuwa ni fluke tu? Kumuuwa mtu kwani ni lazima umtie kisu au kumnyonga kwa kamba?
Leo tunamshukuru Mola kwenye familia yetu tuna PhD moja, Masters 2, bachelors karibu zitakuwa 3 kwani mmoja yupo mwaka watatu akielekea kwenye graduation yake. Hivyo chini ya huyo Sultani wako asieuwa watu tungelifikia level hii? Inasikitisha mtu kama wewe mwenye kufahamu mambo kutoa mifano isiyokuwa na maana.
Hawa machotara walikua daraja la pili wakati wa usultani. Hivi leo baadhi wanalaumu mapinduzi na wanajidai kama wao ndio wazanzibari halisia licha kua ni machotara wenye damu ya mama mwaafrika aliyefikishwa zanzibar kama mtumwa na kubakwa na mwarabu.