kmbwembwe
Wakristo Wanapanga Biashara Ya Utumwa
Watumwa walikuwa wanachukuliwa kutoka hata katika wakati wa Ufalme wa Kirumi, lakini “biashara halisi ya Utumwa” ilianza mnamo karne ya 16 baada ya ujio wa mataifa ya Kikristo ya Ulaya.
Edward A. Alpers wa Chuo Kikuu cha Dar-es Salaam, anaandika kwamba; “kama tunavyoleta utofautisho baina ya biashara inayoambatana katika watumwa ambayo ilichuruzika katika sahara kutoka magharibi mpaka kaskazini ya Afrika kuanzia siku za nyuma sana za wakati wa utawala wa Ufalme wa Kirumi, kwa upande mmoja, na kioja tunacho kiita The West African Slave Trade kwa upande mwingine, kwa hiyo lazima tulete tofauti hiyo hiyo kwa Afrika ya Mashariki.”
Walter Rodney pia wa Chuo, Kikuu cha Dar es Salaam, anaanza kuandika kijitabu chake “West Africa and the Atlantic Slave-Trade kwa maneno yafuatayo: - Wakati wote lazima ikumbukwe kwamba biashara ya utumwa iliyo;fanyi- ka katika bahari ya Atlantiki” lilikuwa ni tukio katika histo- ria ya dunia, iliyo husisha mabara matatu – Ulaya, Afrika na Marekani.
Watu walio toka kwa dhamira ya kutafuta watumwa walikuwa Wazungu waliotoka katika kila nchi kati ya Sweeden kwa upande wa Kaskazini na Ureno kwa upande wa magharibi. Wareno walifika Afrika ya Magharibi muda mfupi kabla ya kuingia nusu karne ya kumi na tano. Mara moja na kwa haraka sana walianza kukamata (watumwa) Waafrika na kuwapeleka kufanya kazi Ulaya kama watumwa, hususan katika Ureno na Hispania.
Lakini maendeleo muhimu sana kwa biashara hii ya utumwa yalikuwa katika karne ya kumi na sita, ambapo mabepari wa Kizungu walitambua kwamba wangepata faida kubwa sana kwa kutumia nguvukazi ya Waafrika kuujenga na kuuendeleza utajiri wa nchi zote za Amerika.
Matokeo yake, Waafrika walipelekwa Amerika ya kaskazini, Amerika ya kati, Amerika ya kusini na Visiwa vya Caribbean kwa ajili ya kukidhi haja ya nguvukazi ya watumwa kwenye machimbo ya dhahabu na shaba, na kwenye mashamba ya kilimo cha mazao ya miwa, pamba na tumbaku. Biashara hii mbaya ya kununua na kuuza binadamu ilidumu kwa kipindi cha miaka (400) mia nne, kwani Atlantic slave-Trade (Biashara ya Utumwa wa kupitia bahari ya Atlantiki) ilikoma mwishoni mwa miaka ya 1870.
“Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu jinsi Biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilivyopangwa huko Ulaya, na kuhusu faida kubwa iliyokusanywa na nchi kama Uingereza na Ufaransa. Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu safari za kutisha kutoka Afrika hadi Marekani kuvu- ka bahari ya Atlantic. Waafrika walipangwa kama dagaa kwenye meli za kubeba watumwa, na matokeo yake walikufa wengi sana.”
Na dagaa walioje! Kwa maelezo zaidi kuhusu upakiaji huu wa watumwa kwenye meli, soma taarifa ifuatayo: - Moja ya hati yenye kuuvunja moyo sana katika nyaraka zote zinazotisha ni “Plan of the Brookes,” mpango mbaya sana wa karne ya kumi na nane wa kupanga watumwa kwenye meli ya kubeba watumwa ‘Brookes’… Kwa mahesabu sahi- hi, teknolojia ya kushtua ilitengenezwa - futi na inchi, chumba cha kusimama na nafasi ya kupumua iliwekwa kwa matumaini ya faida kubwa. Mtu mmoja Bwana Jones anapendekeza kwamba wanawake watano wahesabiwe kama wanaume wanne, na wavulana watatu au wasichana watatu wafanywe kuwa sawa na watu wazima wawili … kila mtumwa mwanaume aruhusiwe futi sita kwa futi moja na inchi nne (1’4”x6’) kama nafasi ya chumba chake, kila mwanamke alipewa nafasi ya upana wa futi tano na inchi kumi na futi moja na inchi nne…. (5’10”x1’4”); na inaendelea hivyo mpaka kila mtu anapata nafasi – watumwa 451.
Lakini Muswada wa Bunge unaruhusu watumwa 454. Kwa hiyo hati hiyo inahitimisha kwamba kama watumwa watatu zaidi wangeweza kuwekwa kwa kubanwa katikati ya wale waliotamkwa kwenye mpango, mpango huu ungeweza kuchukua idadi ile ile ambayo imeelekezwa kwenye muswada.
3
Mara Waafrika walipofikishwa upande mwingine wa bahari ya Atlantic, kwa hakika walikuwa katika “Dunia Mpya”, iliyojaa ukandamizaji na ukatili. Taarifa ifuatayo inaweza kusaidia kuelewa hali ilivyokuwa wakati huo. Rodney anaandika:
“Kuanzia wakati walipofika (Wakristo) Wazungu hadi 1600, takriban Waafrika milioni moja (1, 000,000) walichukuliwa kwenye meli za kubeba watumwa. Wakati wa kipindi hicho, Wareno walikuwa ndio wafanya biashara wakuu wa biashara ya watumwa huko Afrika ya Magharibi. Ama wali- wapeleka Waafrika huko Brazil, ambayo nchi hiyo ilikuwa koloni lao, au vinginevyo waliwauza kwa waloezi wa Kihispania huko Mexico, Amerika ya kati, Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbean. Mnamo karne ya kumi na saba, kiasi cha Waafrika wapatao milioni saba hadi nane kutoka Afrika ya magharibi walivushwa bahari ya Atlantic.
Wadachi walijumuika na Wareno kama wafanya biashara wakuu wa biashara ya utumwa mnamo karne ya kumi na saba, na karne iliyofuata Waingereza wakawa wafanya biashara wakubwa kushinda wote wa biashara ya utumwa. Wakati biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilipofikia kileleni mnamo karne ya kumi na nane, meli za Kiingereza zilikuwa zinachukua zaidi ya nusu ya jumla yote ya watumwa na idadi iliyobaki iligawanywa baina ya Wadachi, Wafaransa, Wareno na Wadane (Danish).
“Ilipofika karne ya kumi na tisa, palikuwepo na mabadiliko mengine ya watu ambao walishika nafasi mbele katika kuinyonya Afrika. Nchi za Ulaya zenyewe hazikushiriki kikamilifu kwenye biashara ya utumwa, lakini badala yake Wazungu ambao waliloea Brazil, Cuba, na Amerika ya Kaskazini ndio ambao walipanga sehemu kubwa ya biashara. Waamerika (U.S.A) ndiyo katika kipindi hicho hicho tu walipata uhuru kutoka kwa Waingereza, hili lilikuwa taifa jipya (U.S.A.) ambalo lilikuwa na mgawo mkubwa kabisa kuliko wote katika biashara ya watumwa katika biashara ya Atlantiki katika kipindi cha miaka hamsi- ni ya mwisho, kwa kuchukua kiwango kikubwa zaidi cha watumwa kuliko ambavyo imewahi kufanya huko nyuma.
“Ilipoanza “biashara ya watumwa ya Atlantiki kwenye pwani ya Afrika ya Magharibi, ilichukua utaratibu wa kutu- mia nguvu moja kwa moja wa Wazungu kuwashambulia Waafrika waliokuwa wanaishi karibu na pwani. Mabaharia wa kwanza wa Kireno walipofika kwenye pwani inayoju- likana leo kama Mauritania, waliacha meli zao na kuanza kuwawinda watu waitwao, Moors watu walioishi katika jimbo hilo. Kwa kweli, hii haikuwa biashara hata kidogo – ilikuwa uvamizi wa nguvu. Hata hivyo, baada ya mashambulizi kadhaa ya kushtukizwa, Waafrika wa pwani wakawa na kawaida ya kulinda kwa zamu na walijilinda kwa nguvu dhidi ya washambuliaji wao Wazungu.
Katika kipindi kifupi tu, Wareno walitambua kwamba uvamizi haikuwa mbinu inayofaa na iliyo salama katika kujaribu kuwapata watumwa. Zaidi ya hayo, pia walitaka dhahabu na bidhaa zingine za Kiafrika, ambazo wangeweza tu kuzipata kwa njia ya kununuliana na kuuziana kwa amani. Kwa hiyo badala ya kuvamia, Wareno waliona afadhali kutumia bidhaa zilizo tengenezwa kiwandani ili kuwatia moyo Waafrika kubadilishana na bidhaa zao na hata kuweza kuwafikisha mateka wa Kiafrika kwenye meli za Wazungu kwa urahisi. Mpango huu haukufanywa na Wareno pekee, lakini hata wazungu wengine wote walitambua na kukubali kwamba huo ulikuwa mpango mzuri zaidi wa kupata bidhaa hapa Afrika; na ilikuwa kwa njia hii waliweza kupata mamilioni ya watumwa