Mohammed Said na Mapinduzi ya Zanzibar

Mohammed Said na Mapinduzi ya Zanzibar

Ni kama vile vile makhalifa wa kiislamu walivyoeneza utumwa bara asia!!!Au wewe hujui hilo kaka???

Kwa Nini Wakristo Wengi Sana Waliunga Mkono Utumwa?

Wakristo wengi wazungu waliona kwamba utumwa, kulingana na maneno ya kasisi mmoja Mbaptisti, “husimama kuwa taasisi ya Mungu.”

Hapa kuna baadhi ya hoja za kawaida zilizotolewa na Wakristo wakati huo:

Sababu za Kibiblia

• Ibrahimu, "baba wa imani," na wazee wote wa ukoo walishikilia watumwa bila kibali cha Mungu (Mwa. 21:9–10).

• Kanaani, mwana wa Hamu, alifanywa mtumwa kwa ndugu zake (Mwa. 9:24–27).

• Amri Kumi zinataja utumwa mara mbili, kuonyesha kuukubali kabisa kwa Mungu (Kut. 20:10, 17).

• Utumwa ulikuwa umeenea katika ulimwengu wote wa Kirumi, na bado Yesu hakuupinga kamwe.

• Mtume Paulo aliamuru hasa watumwa kuwatii mabwana zao (Efe. 6:5–8).

• Paulo alimrudisha mtumwa aliyetoroka, Filemoni, kwa bwana wake (Filem. 12).

Sababu za Uinjilisti

• Utumwa huwaondoa watu kutoka katika tamaduni za “kuabudu shetani, kufanya uchawi, uchawi” na maovu mengine.

• Utumwa huleta wapagani katika nchi ya Kikristo ambapo wanaweza kusikia injili. Mabwana Wakristo hutoa mafundisho ya kidini kwa watumwa wao.

• Chini ya utumwa, watu hutendewa kwa wema, kama wageni wengi wa kaskazini wanavyoweza kuthibitisha.

• Ni kwa manufaa ya wamiliki wa watumwa kuwatendea vyema watumwa wao.

• Watumwa wanatendewa kwa ukarimu zaidi kuliko wafanyakazi katika viwanda vinavyokandamiza vya kaskazini.

Sababu za Kijamii

• Kama vile wanawake wameitwa kuchukua nafasi ya chini (Efe. 5:22; 1 Tim. 2:11–15), vivyo hivyo watumwa huwekwa na Mungu mahali pao.

• Utumwa ni njia ya Mungu ya kulinda na kutoa kwa ajili ya jamii duni (kuteseka "laana ya Hamu" katika Mwa. 9:25 au hata adhabu ya Kaini katika Mwa. 4:12).

• Kukomeshwa kungesababisha maasi ya watumwa, umwagaji damu, na machafuko. Fikiria “utawala wa ugaidi” wa umati wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa.

Sababu za Kisiasa

• Wakristo wanapaswa kutii mamlaka za serikali, na mamlaka hizo zinaruhusu na kulinda utumwa.

• Kanisa linapaswa kuzingatia mambo ya kiroho, si ya kisiasa. ( Usichanganye dini na siasa kama tunavyoambiwa na CCM )

• Wale wanaounga mkono kukomeshwa ni, katika maneno ya James H. Thornwell, "wasioamini Mungu, wasoshalisti, wakomunisti ."
 
Kaka Mohammed Said,

Kwanza nakuamkia.

Pili, khutba zako kwenye social media zinaendelea kuwapotosha watu kuhusu mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964. Bila ya mapinduzi haya wengi wetu visiwani leo tungelikuwa wakwezi au wateka maji.

Mapinduzi ya Zanzibar hayakumpinduwa Mzanzibari kama unavyosema wewe. Natumai unafahamu vizuri vipi waarabu kutoka Oman walifika kuitawala Zanzibar.

Wa-Omani waliichukuwa Zanzibar kwa nguvu kinyume na matakwa ya Wazanzibari wenyewe baada ya kumshinda mreno, sasa na wao kwanini wasiondoshwe kwa nguvu? Ni kweli kuwa Wa-Omani walimfukuza mreno kutoka Zanzibar, lakini baada ya Wa-Omani kuwarejeshea utawala wao Wazanzibari, walijifanya wao wafalme wa visiwa hivi.

Kwahivyo, kupinduliwa kwa Wa-Omani katika mwaka 1964 ilikuwa ni muendelezo wa events ambazo wao wenyewe Wa-Omani walizianzisha. Wa-Omani walivivamia visiwa vya Zanzibar kwa nguvu na wakajifanya wafalme na kwahivyo kwa wenyeji wa kizanzibari kutafuta msaada 1964 kutoka kwa wamakonde wa Tanga (kama unavyoeleza) ili kuwaondoa wavamizi visiwani mwao hayafanyi mapinduzi ya Zanzibar kuwa sio halali.

Tanzania tuliwasaidia wapigania uhuru kutoka Msumbiji, South Africa, Zimbabwe, etc. je, ushindi wao sio halali leo kwasababu walisaidiwa na watu kutoka nje? Kumwita jirani yako kuja kukusaidia kumtoa alievamia nyumba yako ni kosa?

Kama Wa-Omani walikuwa wenye nia njema, basi baada ya kumuondosha mreno visiwani wangeliwarejeshea wenyewe Wazanzibari utawala wao na sio wao Wa-Omani kujifanya wafalme kwa nguvu zao.

Eti unasema mfalme wa Zanzibar hata siku moja hajamuuwa muafrika hata mmoja. Are you in your proper senses Sir? Umesahau waafrika walivyokuwa wakikandamizwa kielimu visiwani? Muafrika gani alikuwa akipata nafasi ya kuingia secondary school? Hao akina Jumbe na Ali Hassan Mwinyi sio ilikuwa ni fluke tu? Kumuuwa mtu kwani ni lazima umtie kisu au kumnyonga kwa kamba?

Leo tunamshukuru Mola kwenye familia yetu tuna PhD moja, Masters 2, bachelors karibu zitakuwa 3 kwani mmoja yupo mwaka watatu akielekea kwenye graduation yake. Hivyo chini ya huyo Sultani wako asieuwa watu tungelifikia level hii? Inasikitisha mtu kama wewe mwenye kufahamu mambo kutoa mifano isiyokuwa na maana.
Kwa Mohamed Said unapoteza muda tu.

Huyo kwanza ni mzee, na Mzee huwezi kumbadilisha akili yake.

Na pili ni Muarabu Mweusi huyo. Ukitaka kuwajua vizuri waarabu weusi nenda Sudan. Kisa cha Sudani kuvunjika na kuzaa Sudani Kusini ni hao waarbu weusi wa Sudani.

Ngozi zao ni nyeusi, na wakati mwingine ni nyeusi tii kabisa, lakini wameuvaa uarabu kindakindaki kupitia dini ya Uislam. Huwaambii kitu kuhusu Mwarabu.

Huyo ndo Muhamed Said. Yeye kichwani mwake haoni utumwa, bali anaona ujio wa Uislam kwa sisi wa ngozi nyeusi kwamba ni jambo la heri na la baraka. Yeye haoni shida nchi ikiwa chini ya Mwarabu. Anachojali kuliko vyote ni Uislam. Mwafrika akiwa mtumwa wa Mwarabu ilimradi ni Muislam kwa Mohamed Said haina shida.
 
Kwa Nini Wakristo Wengi Sana Waliunga Mkono Utumwa?

Wakristo wengi wazungu waliona kwamba utumwa, kulingana na maneno ya kasisi mmoja Mbaptisti, “husimama kuwa taasisi ya Mungu.”

Hapa kuna baadhi ya hoja za kawaida zilizotolewa na Wakristo wakati huo:

Sababu za Kibiblia

• Ibrahimu, "baba wa imani," na wazee wote wa ukoo walishikilia watumwa bila kibali cha Mungu (Mwa. 21:9–10).

• Kanaani, mwana wa Hamu, alifanywa mtumwa kwa ndugu zake (Mwa. 9:24–27).

• Amri Kumi zinataja utumwa mara mbili, kuonyesha kuukubali kabisa kwa Mungu (Kut. 20:10, 17).

• Utumwa ulikuwa umeenea katika ulimwengu wote wa Kirumi, na bado Yesu hakuupinga kamwe.

• Mtume Paulo aliamuru hasa watumwa kuwatii mabwana zao (Efe. 6:5–8).

• Paulo alimrudisha mtumwa aliyetoroka, Filemoni, kwa bwana wake (Filem. 12).

Sababu za Uinjilisti

• Utumwa huwaondoa watu kutoka katika tamaduni za “kuabudu shetani, kufanya uchawi, uchawi” na maovu mengine.

• Utumwa huleta wapagani katika nchi ya Kikristo ambapo wanaweza kusikia injili. Mabwana Wakristo hutoa mafundisho ya kidini kwa watumwa wao.

• Chini ya utumwa, watu hutendewa kwa wema, kama wageni wengi wa kaskazini wanavyoweza kuthibitisha.

• Ni kwa manufaa ya wamiliki wa watumwa kuwatendea vyema watumwa wao.

• Watumwa wanatendewa kwa ukarimu zaidi kuliko wafanyakazi katika viwanda vinavyokandamiza vya kaskazini.

Sababu za Kijamii

• Kama vile wanawake wameitwa kuchukua nafasi ya chini (Efe. 5:22; 1 Tim. 2:11–15), vivyo hivyo watumwa huwekwa na Mungu mahali pao.

• Utumwa ni njia ya Mungu ya kulinda na kutoa kwa ajili ya jamii duni (kuteseka "laana ya Hamu" katika Mwa. 9:25 au hata adhabu ya Kaini katika Mwa. 4:12).

• Kukomeshwa kungesababisha maasi ya watumwa, umwagaji damu, na machafuko. Fikiria “utawala wa ugaidi” wa umati wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa.

Sababu za Kisiasa

• Wakristo wanapaswa kutii mamlaka za serikali, na mamlaka hizo zinaruhusu na kulinda utumwa.

• Kanisa linapaswa kuzingatia mambo ya kiroho, si ya kisiasa. ( Usichanganye dini na siasa kama tunavyoambiwa na CCM )

• Wale wanaounga mkono kukomeshwa ni, katika maneno ya James H. Thornwell, "wasioamini Mungu, wasoshalisti, wakomunisti ."
Kaka ushatoka kwenye kukandia chama chetu ASP umehamia kwa watu wa msalaba!!!Inshaalah
 
Kwahiyo ndio maana anachukia wazee wetu kufanya mapinduzi 1964
Kwa Mohamed Said unapoteza muda tu.

Huyo kwanza ni mzee, na Mzee huwezi kumbadilisha akili yake.

Na pili ni Muarabu Mweusi huyo. Ukitaka kuwajua vizuri waarabu weusi nenda Sudan. Kisa cha Sudani kuvunjika na kuzaa Sudani Kusini ni hao waarbu weusi wa Sudani.

Ngozi zao ni nyeusi, na wakati mwingine ni nyeusi tii kabisa, lakini wameuvaa uarabu kindakindaki kupitia dini ya Uislam. Huwaambii kitu kuhusu Mwarabu.

Huyo ndo Muhamed Said. Yeye kichwani mwake haoni utumwa, bali anaona ujio wa Uislam kwa sisi wa ngozi nyeusi kwamba ni jambo la heri na la baraka. Yeye haoni shida nchi ikiwa chini ya Mwarabu. Anachojali kuliko vyote ni Uislam. Mwafrika akiwa mtumwa wa Mwarabu ilimradi ni Muislam kwa Mohamed Said haina shida.
 
Nilikujibu alikaa miaka 100

Huna isipokuwa chuki mara Waarabu ,mara Sultani mara machotara hamna chochote nyinyi vibaraka wa mkoloni muingereza . Nchi yote mumeichafua na watu kuwatia umasikini uliokithiri
Alikaaa miaka mia kumbe!!!Basi tumsubiri mzee SAIDI mohamedi aje kukujibia!!Kdumu chama cha mapinduzi🤣🤣🤣
 
Alikaaa miaka mia kumbe!!!Basi tumsubiri mzee SAIDI mohamedaje kukujibia!!Kdumu chama cha mapinduzi🤣🤣🤣
 
Alikaaa miaka mia kumbe!!!Basi tumsubiri mzee SAIDI mohamedi aje kukujibia!!Kdumu chama cha mapinduzi🤣🤣🤣

wakati tunamsubiri , jibu swali , maana ulisema ukijibiwa utajibu

nani aliuliwa na sultan jemshid , au kuibiwa mali yake au kunajisiwa au kutiwa kilema ??
 
Mimi nimetoka wewe ndio ulihamia , angalia ulichoandika hapa chini in red

Nelson Jacob lushasi said:

Ni kama vile vile makhalifa wa kiislamu walivyoeneza utumwa bara asia!!!Au wewe hujui hilo kaka???

kmbwembwe

Wakristo Wanapanga Biashara Ya Utumwa​

Watumwa walikuwa wanachukuliwa kutoka hata katika wakati wa Ufalme wa Kirumi, lakini “biashara halisi ya Utumwa” ilianza mnamo karne ya 16 baada ya ujio wa mataifa ya Kikristo ya Ulaya.

Edward A. Alpers wa Chuo Kikuu cha Dar-es Salaam, anaandika kwamba; “kama tunavyoleta utofautisho baina ya biashara inayoambatana katika watumwa ambayo ilichuruzika katika sahara kutoka magharibi mpaka kaskazini ya Afrika kuanzia siku za nyuma sana za wakati wa utawala wa Ufalme wa Kirumi, kwa upande mmoja, na kioja tunacho kiita The West African Slave Trade kwa upande mwingine, kwa hiyo lazima tulete tofauti hiyo hiyo kwa Afrika ya Mashariki.”

Walter Rodney pia wa Chuo, Kikuu cha Dar es Salaam, anaanza kuandika kijitabu chake “West Africa and the Atlantic Slave-Trade kwa maneno yafuatayo: - Wakati wote lazima ikumbukwe kwamba biashara ya utumwa iliyo;fanyi- ka katika bahari ya Atlantiki” lilikuwa ni tukio katika histo- ria ya dunia, iliyo husisha mabara matatu – Ulaya, Afrika na Marekani.

Watu walio toka kwa dhamira ya kutafuta watumwa walikuwa Wazungu waliotoka katika kila nchi kati ya Sweeden kwa upande wa Kaskazini na Ureno kwa upande wa magharibi. Wareno walifika Afrika ya Magharibi muda mfupi kabla ya kuingia nusu karne ya kumi na tano. Mara moja na kwa haraka sana walianza kukamata (watumwa) Waafrika na kuwapeleka kufanya kazi Ulaya kama watumwa, hususan katika Ureno na Hispania.

Lakini maendeleo muhimu sana kwa biashara hii ya utumwa yalikuwa katika karne ya kumi na sita, ambapo mabepari wa Kizungu walitambua kwamba wangepata faida kubwa sana kwa kutumia nguvukazi ya Waafrika kuujenga na kuuendeleza utajiri wa nchi zote za Amerika.

Matokeo yake, Waafrika walipelekwa Amerika ya kaskazini, Amerika ya kati, Amerika ya kusini na Visiwa vya Caribbean kwa ajili ya kukidhi haja ya nguvukazi ya watumwa kwenye machimbo ya dhahabu na shaba, na kwenye mashamba ya kilimo cha mazao ya miwa, pamba na tumbaku. Biashara hii mbaya ya kununua na kuuza binadamu ilidumu kwa kipindi cha miaka (400) mia nne, kwani Atlantic slave-Trade (Biashara ya Utumwa wa kupitia bahari ya Atlantiki) ilikoma mwishoni mwa miaka ya 1870.

“Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu jinsi Biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilivyopangwa huko Ulaya, na kuhusu faida kubwa iliyokusanywa na nchi kama Uingereza na Ufaransa. Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu safari za kutisha kutoka Afrika hadi Marekani kuvu- ka bahari ya Atlantic. Waafrika walipangwa kama dagaa kwenye meli za kubeba watumwa, na matokeo yake walikufa wengi sana.”

Na dagaa walioje! Kwa maelezo zaidi kuhusu upakiaji huu wa watumwa kwenye meli, soma taarifa ifuatayo: - Moja ya hati yenye kuuvunja moyo sana katika nyaraka zote zinazotisha ni “Plan of the Brookes,” mpango mbaya sana wa karne ya kumi na nane wa kupanga watumwa kwenye meli ya kubeba watumwa ‘Brookes’… Kwa mahesabu sahi- hi, teknolojia ya kushtua ilitengenezwa - futi na inchi, chumba cha kusimama na nafasi ya kupumua iliwekwa kwa matumaini ya faida kubwa. Mtu mmoja Bwana Jones anapendekeza kwamba wanawake watano wahesabiwe kama wanaume wanne, na wavulana watatu au wasichana watatu wafanywe kuwa sawa na watu wazima wawili … kila mtumwa mwanaume aruhusiwe futi sita kwa futi moja na inchi nne (1’4”x6’) kama nafasi ya chumba chake, kila mwanamke alipewa nafasi ya upana wa futi tano na inchi kumi na futi moja na inchi nne…. (5’10”x1’4”); na inaendelea hivyo mpaka kila mtu anapata nafasi – watumwa 451.

Lakini Muswada wa Bunge unaruhusu watumwa 454. Kwa hiyo hati hiyo inahitimisha kwamba kama watumwa watatu zaidi wangeweza kuwekwa kwa kubanwa katikati ya wale waliotamkwa kwenye mpango, mpango huu ungeweza kuchukua idadi ile ile ambayo imeelekezwa kwenye muswada.3
Mara Waafrika walipofikishwa upande mwingine wa bahari ya Atlantic, kwa hakika walikuwa katika “Dunia Mpya”, iliyojaa ukandamizaji na ukatili. Taarifa ifuatayo inaweza kusaidia kuelewa hali ilivyokuwa wakati huo. Rodney anaandika:

“Kuanzia wakati walipofika (Wakristo) Wazungu hadi 1600, takriban Waafrika milioni moja (1, 000,000) walichukuliwa kwenye meli za kubeba watumwa. Wakati wa kipindi hicho, Wareno walikuwa ndio wafanya biashara wakuu wa biashara ya watumwa huko Afrika ya Magharibi. Ama wali- wapeleka Waafrika huko Brazil, ambayo nchi hiyo ilikuwa koloni lao, au vinginevyo waliwauza kwa waloezi wa Kihispania huko Mexico, Amerika ya kati, Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbean. Mnamo karne ya kumi na saba, kiasi cha Waafrika wapatao milioni saba hadi nane kutoka Afrika ya magharibi walivushwa bahari ya Atlantic.

Wadachi walijumuika na Wareno kama wafanya biashara wakuu wa biashara ya utumwa mnamo karne ya kumi na saba, na karne iliyofuata Waingereza wakawa wafanya biashara wakubwa kushinda wote wa biashara ya utumwa. Wakati biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilipofikia kileleni mnamo karne ya kumi na nane, meli za Kiingereza zilikuwa zinachukua zaidi ya nusu ya jumla yote ya watumwa na idadi iliyobaki iligawanywa baina ya Wadachi, Wafaransa, Wareno na Wadane (Danish).

“Ilipofika karne ya kumi na tisa, palikuwepo na mabadiliko mengine ya watu ambao walishika nafasi mbele katika kuinyonya Afrika. Nchi za Ulaya zenyewe hazikushiriki kikamilifu kwenye biashara ya utumwa, lakini badala yake Wazungu ambao waliloea Brazil, Cuba, na Amerika ya Kaskazini ndio ambao walipanga sehemu kubwa ya biashara. Waamerika (U.S.A) ndiyo katika kipindi hicho hicho tu walipata uhuru kutoka kwa Waingereza, hili lilikuwa taifa jipya (U.S.A.) ambalo lilikuwa na mgawo mkubwa kabisa kuliko wote katika biashara ya watumwa katika biashara ya Atlantiki katika kipindi cha miaka hamsi- ni ya mwisho, kwa kuchukua kiwango kikubwa zaidi cha watumwa kuliko ambavyo imewahi kufanya huko nyuma.

“Ilipoanza “biashara ya watumwa ya Atlantiki kwenye pwani ya Afrika ya Magharibi, ilichukua utaratibu wa kutu- mia nguvu moja kwa moja wa Wazungu kuwashambulia Waafrika waliokuwa wanaishi karibu na pwani. Mabaharia wa kwanza wa Kireno walipofika kwenye pwani inayoju- likana leo kama Mauritania, waliacha meli zao na kuanza kuwawinda watu waitwao, Moors watu walioishi katika jimbo hilo. Kwa kweli, hii haikuwa biashara hata kidogo – ilikuwa uvamizi wa nguvu. Hata hivyo, baada ya mashambulizi kadhaa ya kushtukizwa, Waafrika wa pwani wakawa na kawaida ya kulinda kwa zamu na walijilinda kwa nguvu dhidi ya washambuliaji wao Wazungu.

Katika kipindi kifupi tu, Wareno walitambua kwamba uvamizi haikuwa mbinu inayofaa na iliyo salama katika kujaribu kuwapata watumwa. Zaidi ya hayo, pia walitaka dhahabu na bidhaa zingine za Kiafrika, ambazo wangeweza tu kuzipata kwa njia ya kununuliana na kuuziana kwa amani. Kwa hiyo badala ya kuvamia, Wareno waliona afadhali kutumia bidhaa zilizo tengenezwa kiwandani ili kuwatia moyo Waafrika kubadilishana na bidhaa zao na hata kuweza kuwafikisha mateka wa Kiafrika kwenye meli za Wazungu kwa urahisi. Mpango huu haukufanywa na Wareno pekee, lakini hata wazungu wengine wote walitambua na kukubali kwamba huo ulikuwa mpango mzuri zaidi wa kupata bidhaa hapa Afrika; na ilikuwa kwa njia hii waliweza kupata mamilioni ya watumwa
Na mimi nilichukua kwako kaka
 
Karibu forodhani kaka tule urojo baadae!!!Niletee na kadi ya ACT wazalendo kaka

Forodhani yote mumeshaiuwa , kardinali wako huyu anakuambia Muungano kaleta Yesu na uulinde kwa nguvu zote , hii ndio hali

- May 02, 2016

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka waamini na wananchi kwa ujumla kutambua kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar si jambo la bahati nasibu.

Kardinali Pengo ameyasema hayo ofisini kwake hivi karibuni alipoitisha vyombo vya habari vya Kanisa Katoliki kuzungumzia pamoja na mambo mengine ongezeko la Parokia mpya jimboni kwake pamoja na mabadiliko kwa Maparoko na Maparoko Wasaidizi katika baadhi ya Parokia jimboni humo.

Asemema suala la Muungano linapaswa kuchukuliwa kwa uzito wa pekee kwa kila Mtanzania hasa waamini Wakatoliki na kwamba kila mwamini anapaswa kutambua kuwa amepewa jukumu na Mwenyezi Mungu kulinda na kuombea Muungano huo.
 
Dhuluma za waarabu ushahidi hauna ila dhuluma za ASP ushahidi unao!!!!Sawa mzee wangu walowezi wa kiarabu walikua watu bora zaidi kuliko babi zetu akina mzee karume
Nelson...
Umejaa na joto la chuki ya Uislam lugha ni hizo "Walowezi wa Kiarabu," kama vile ni jambo la jinai.

Lete ushahidi wa jela za mateso na mauaji.

Kauliwa Jaha Ubwa na Abdulaziz Twala ASP kindakindaki rafiki wa baba yangu.

Wanamapinduzi hawa.
Mauaji hayajasimama hadi leo.

Wewe unazungumza jambo usilolijua kabisa si kwa ndewe wala sikio.

Mimi nimeshiriki katika utafiti wa historia ya mapinduzi na tukaja na Kipumbwi na mengi ya Okello ambayo wewe umeyajua kwangu.
 
Back
Top Bottom