Mohammed Said na Mapinduzi ya Zanzibar

Kabla hujacomment mawazo ya mzanzibari kwanza ujue ni mzanzibari wa aina gani. Nililojifunza karibu kila mzanzibari mwenye uchotara wa kiarabu atakupa hoja sawa na wale watawala waliyotawala zanzibar wakati wa usultani. Ni mzanzibari mwafrika mtupu na chotara wachache ndio watakuambia furaha ya kukombolewa visiwa hivyo kwa mapinduzi ya 1964 na kuonesha kupenda muungano na ndugu zao wa tanganyika.
Hawa machotara walikua daraja la pili wakati wa usultani. Hivi leo baadhi wanalaumu mapinduzi na wanajidai kama wao ndio wazanzibari halisia licha kua ni machotara wenye damu ya mama mwaafrika aliyefikishwa zanzibar kama mtumwa na kubakwa na mwarabu.
 
Kaka gavana ngoja mimi nikuache naenda zanzbar mda huu!!!Nikutakie siku njema ndugu yangu

ibari kwanza ujue ni mzanzibari wa aina gani. Nililojifunza karibu kila mzanzibari mwenye uchotari wa kiarabu atakupa hoja sawa na wale watawala waliyotawala zanzibar wakati wa usultani. Ni mzanzibari mwafrika mtupu na chotara wachache ndio watakuambia furaha ya kukombolewa visiwa hivyo kwa mapinduzi ya 1964 na kuonesha kupenda muungano na ndugu zao wa tanganyika.
Hawa machotara walikua daraja la pili wakati wa usultani. Hivi leo baadhi wanalaumu mapinduzi na wanajidai kama wao ndio wazanzibari halisia licha kua ni machotara wenye damu ya mama mwaafrika aliyefikishwa zanzibar kama mtumwa na kubakwa na mwarabu.


usipakazie , Chaguzi zote zilisema nini wazanzibar waliowengi wanataka
 
kumbe huna kujua historia yoyote unataka ubishi tu , sawa na twende tu mpaka kesho
Tutaendelea kesho usijali ila uje na jibu jamshidi alikaa mda gani kwenye throne na mimi nitakuambia dhuluma zote alizofanya!!!!Kama upo zanzbar tutafutane nitakua hapo baada ya masaa matatu kasoro!!!
 
Facts
 
Huku ndiko nchi ilikofikishwa na hawa wanaojifanya weusi sana kuliko waafrika wengine


Your browser is not able to display this video.
 
Kaka elimu yako ni pana sana na sisi tunahitaji wasomi kama wewe wenye weledi wa kuelewa mamba!!!!
 
Hawa machotara walikua daraja la pili wakati wa usultani. Hivi leo baadhi wanalaumu mapinduzi na wanajidai kama wao ndio wazanzibari halisia licha kua ni machotara wenye damu ya mama mwaafrika aliyefikishwa zanzibar kama mtumwa na kubakwa na mwarabu.

Kama ilivyokuwa Afrika ya Magharibi, biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki ilikuwa mashuhuri na ilianzishwa kikamilifu na kutokana na maendeleo na jitihada za nchi za Kikristo za Ulaya. Bwana E. A. Alpers anaandika kwenye “African Slave-Trade (Biashara ya Utumwa ya Afrika):

Ushahidi zaidi kwamba biashara ya watumwa kwa vyovyote vile ilikuwa mashuhuri katika Afrika ya Mashariki kabla ya karne ya kumi na nane, imeletwa na Wareno. Hakika Wareno, wakiwa ndiyo waasisi (waanzilishi) wa Atlantic Slave-Trade, wangejaribu kuendeleza biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki kama wangeikuta tayari ipo na imekwisha shamiri. Lakini maandiko ya mwanzo ya Wareno yanataja tu biashara ya watumwa kwa kupitia tu.

Lililokuwa muhimu zaidi ni wale wafanyabiashara za dhahabu na pembe za ndovu walizipeleka Arabuni na India. Wavamizi wa Kireno walielekeza juhudi zao kwenye bidhaa hizo wakati wa karne ya kumi na sita na kumi na saba, sio tu kwenye pwani ya Kenya na Tanzania, bali pia katika Msumbiji na Zimbabwe. Hata nta na ambari zinaonyesha zilikuwa bidhaa muhimu zaidi kuzidi watumwa wakati mrefu sana wa kipindi hiki. Kwani tofauti na wakoloni katika nchi ya Amerika, Wareno kamwe hawakuanzisha uchumi wowote wa kilimo huko India.

Biashara ya watumwa ya Wareno kutoka Msumbiji kwenda India kwa nadra sana ili- fika idadi ya watu elfu moja katika kipindi cha mwaka mmoja wowote ule, na kwa kawaida ilikuwa chini ya nusu ya idadi hiyo. Huko Brazil ilikuwa haramu kufanya biashara ya watumwa hadi mwaka 1645, na kamwe haikulitiliwa maanani hadi mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa. Hadi mwaka wa 1753, wakati misingi ya biashara mpya ya watumwa ilikuwa inawekwa Afrika ya Mashariki, palikuwepo na jumla ya watumwa 4399 tu wa Kiafrika katika India yote ya Wareno.

“Misingi hii ni ipi? Licha ya mahusiano ya muda mrefu baina ya Waarabu na Afrika ya Mashariki, biashara ya watumwa haikutiliwa matumaini na Wafaransa. Kwa mujibu wa tarakimu rasimi, zaidi ya watumwa 1,000 walikuwa wanasafirishwa kila mwaka. Wafaransa, wakifanya magendo kwa ajili ya kukwepa kodi ambazo zilitozwa Msumbiji, labda waliongeza idadi na kufika angalau 1,500. Inawezekana ni idadi ile ile ilichukuliwa kutoka Ibo wakati wa muongo huu. Kwa hiyo Wareno kule Msumbiji na Ibo (na baadaye Quelimane, karibu na mdomo wa mto Zambezi unapoingilia baharini) walijishughulisha na sera ya biashara ya watumwa na hawakurudi nyuma, wakaendelea nayo hadi kukomeshwa kwake.

Biashara ya watumwa ilizidi kupamba moto mnamo miaka ya themanini, hasa zaidi baada ya kumalizika vita ya uhuru wan chi ya Amerika.

Katika miaka ya sabini, wafanya biashara ya utumwa wachache wa Kifaransa walichukua mizigo kutoka Msumbiji kwenda visiwa vya West-Indies, kwa sababu waliiona hasara ilikuwa inaongezeka katika wakati wa kutafuta bidhaa zao zinazohamashika kwenye pwani ya Guinea. Sasa, wakati wa amani, kwa mashindano makubwa zaidi ya kutafuta watumwa katika Afrika ya Magharibi, ilifunguliwa njia kwa ajili ya upanuzi mkubwa wa biashara ya watumwa ya Waamerika kutoka Afrika ya Mashariki.
 
Nani aliyemweka Nyerere madarakani baada ya kupinduliwa na wanajeshi waafrika? Au nao walikuwa walowezi wa kiarabu?Unafikiri Mzungu hukufanyia Bure tu ?
Tuweke kumbukumbu sawa. Nyerere hajawahi kupinduliwa ila kulikuwa na majaribio kadhaa ya kumpindua.
 
Tuweke kumbukumbu sawa. Nyerere hajawahi kupinduliwa ila kulikuwa na majaribio kadhaa ya kumpindua.

USIKU wa kuamkia Januari 21, 1964, Jeshi la Tanganyika liliasi na kushikilia serikali kwa muda, tukio ambalo , Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alilielezea kuwa ni “siku ya aibu sana kwa Taifa” .

Wakati jeshi hilo likiasi; siku hiyo hiyo, na saa hiyo hiyo, majeshi ya Kenya na Uganda nayo yaliasi kwa staili hiyo hiyo.

Maasi yote ya nchi tatu hizo yalizimwa na majeshi ya Uingereza siku moja na wakati huo huo.
 
@ kmbwembwe


Wakati huo huo meli za Wareno pia zilianza sehemu ya kufaa (ingawa ilikuwa bado ni ya kufuata) katika biashara ya watumwa kwenda kisiwa cha Mascarene. Tarakimu rasimi kutoka Msumbiji peke yake zinaonyesha kwamba tangu 1781 hadi 1794 jumla ya watumwa 46,461 walipakiwa kwenye meli za Kireno na za kigeni, ambazo karibu zote zilikuwa za Wafaransa. Ikijumlishwa na idadi ndogo ya magendo, angalau watumwa 4,000 lazima walikuwa wanaondoka Msumbiji wakati wa kipindi hiki kila mwaka.”


Ilikuwa katika hali hii ambayo Waarabu walipanua msaada wao kuwasaidia hawa wafanyabiashara ya utumwa wa Kikristo. Mwandishi huyo huyo anasema: “Baada ya Waarabu wa Oman kuitika wito wa baadhi ya watawala wa Kiswahili wa miji ya pwani na kwa msaada wao waliwatoa Wareno kutoka Mombasa mnamo 1698 na sehemu zingine muhimu za mbali, wao wenyewe walikuwa wanyonge sana kushughulika na jambo lingine zaidi ya kuwasumbua na kuwaibia watu hao hao waliowaomba msaada wao;
.


“Hata hivyo, hakuna takwimu sahihi zozote zile zenye kuonyesha kuhusu ukubwa wa biashara ya utumwa iliyofanywa na Waarabu katika karne ya kumi na nane.

Dalili ya kwanza iliopo inatoka kwa mfanya biashara ya watumwa wa Kifaransa aitwaye Jean Vincent Morice, ambaye alifanya biashara Zanzibar na Kilwa, ambayo ilikuwa bandari muhimu ya watumwa katika pwani, mnamo miaka ya 1770.

Mnamo tarehe 14, September, 1776, Morice alifanya mkataba na Sultani wa Kilwa kwa ununuzi wa angalau watumwa
1,000 kwa mwaka.

Katika misafara mitatu kabla ya kuutia sahihi mkataba huu, Morice alikwisha nunua watumwa 2325 kwa ajili ya kuwasafirisha nje.

Morice hatuambii Waarabu walikuwa wakiwachukua watumwa wangapi kutoka pwani kila mwaka, lakini kwa wazi aliona kuwa ilikuwa biashara kubwa kwa viwango vya Kifaransa.


Inaonekana ni sawa kusema kwamba angalau watumwa 2000 walikuwa wanachukuliwa kwa mwaka katika kipindi hicho.

Kwa hiyo, licha ya kwamba Wafaransa hawakutawala biashara ya watumwa hapa kama walivyofanya Msumbiji, walikuwa kichocheo kwa mahitaji ya soko la watumwa katika kipindi ambacho biashara ya Waarabu ilikuwa bado ndiyo inakua katika uchanga wake.

Juhudi za Ufaransa ziliendelea hadi miaka ya 1780, lakini mnamo mwishoni mwa karne hiyo, juhudi hizi zilionyesha zilikwisha pungua sana umuhimu wake kuliko biashara ya Waarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…