Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Nelson...Niumie nini wakati sisi ndio watawala!!!Anaumia mzee saidi na marafiki zake wa hizbu kaka
Wazee wetu ndiyo waliounda TANU.
Abdul Sykes na Dossa Aziz ndiyo waliomjulisha Nyerere kwa Karume.
Wazee wetu wote wakiunga mkono ASP.
Abbas Sykes ndiye akipeleka fedha kwa Karume Zanzibar akipanda majahazi kuweka usiri.
Karume akija Dar es Salaam anafikia nyumbani kwa Regional Commissioner Abbas Sykes Mtaa wa Shaban Robert.
Hii baada ya Tanganyika kupata uhuru.
Na inaaminika siku ya kupindua alikuwa kwa Abbas Sykes.
Si ya kuhadithiwa haya baadhi ya ndugu zetu wameyaona kwa macho yao.
Wewe nini ulichokuwanacho katika historia hii unikejeli mimi kwa ati marafiki zangu Hizbu.
Hao Hizbu ni umri wa kunizaa mimi si marafiki zangu na tunaunganishwa na udugu wetu wa Kiislam.
Narudia tena huna moja ulijualo katika historia yetu.
Ati unatawala unawacheka Wazanzibari kwa kutawala ingawa umeshindwa katika sanduku la kura mara sita?