Moja ya dalili ya kijana kukosa maadili ya wazazi ni kuwafanya Wasanii wa muziki, drama na Filamu kuwa Role Model

For sure.
Yaani watoto wengi wamelelewa na movie pamoja na muziki huku wazazi wao wakiwa busy
 
Mimi Nakubali Hoja Zako Kwa Kujiangalia Mimi Mwenyewe Na Wale Wanaonizunguka.

Wakati Ninakua Nilikuwa Mpenzi Wa Music Sana Kitu Ambacho Kilinifanya Baadae Nipate Tabu Maishani Kwani Nilipoteza Wazazi Angali Mdogo Sana Na Kutokana Na Familia Nyingi Za Kiafrika Nililazimika Kuanza Kujitegemea
Hapa Ndo Changamoto Zilipoanza Na Nililelewa Kiuwana Muziki Huku Nikiamini Ipo Siku Mziki Utanitoa Kitu Ambacho Kilifanya Niwe Mvivu Na Kushindwa Kuwa Mchakalikaji Nilikuja Kubadilika Baadae Sana Baada Ya Kupigwa Sana Na Maisha.

Ni Stori Ndefu Ngoja Niishie Hapa .

Next Time .
 
Huja yako ungeweka specifically kwa Tanzania
 
Ikiwa ni Tanzania pekee ,tatizo nini ushamba wa wazazi wapya na vizazi vyao?!!
Nchi nyingine za Afrika wamewezaje kuukwepa ushamba huo wa kimaisha?!!
Nimesema hivyo kwasababu binafsi nina experience mbovu na wasanii wa Tz..
Hivi mfano binti yangu nitajihisi furaha nikimuona ni role model wa msanii wa filamu?!
 
Nimesema hivyo kwasababu binafsi nina experience mbovu na wasanii wa Tz..
Hivi mfano binti yangu nitajihisi furaha nikimuona ni role model wa msanii wa filamu?!
Ni ngumu kujihisi furaha mkuu wangu......

Je tujenge "novelty centers" nyingi ambazo zitakuwa "programmed" kwa mitazamo yetu ya kukiokoa hiki kizazi cha "malimbukeni"?!!
 
Nililelewa katika nyumba ambayo mtoto chini ya miaka 18 hakuruhusiwa kuangalia televisheni zaidi ya vipindi vya watoto na taarifa ya habari tena wikiendi tu.....

Leo nikimzuia mwenzangu asivipe simu janja watoto naonekana "mkoloni" eti hizo simu wanawekewa "game za watoto" ilihali watoto wanaperuze hata wasipotakiwa "kwenda".....
 
Baelezee Batanzani

Huezi ukaepuka hali hio unaeza limit tu muda ya kuwaangalia, unawatafutia vitu ya kufanya. You have to be there for your kids bazee.

Kwa maendeleo ya Ulaya na Marekani, ya tech unakutana na katoto miaka 3 anayo simu janja, ana TicToC, Instar, netflix na apps nyingi tu zingine za mitandao ya jamii.

banakutana na basanii mastaa banaonekana kama wamefanikiwa sana mapedeshe, mundani batoto banaoneshwa maisha na mafanikio kuwafanya kuwa mifano ya kuiga.
Nyumba wanayoishi inafanana na banda la Kuku Kenya. Wanaita Trailer park cjiu nn Watoto hawana maadili, wazazi hawana maadili unamkuta mzazi amevaa singlendi cku nzima ti wanaita wife beater, unategemea watoto wawe na role model hapo? Bac wanaingia kwenye cmu janja kuangalia tictoc. kutafuta rolemodel wake iwe ni msanii, drama n.k apate kuescape na mateso ya kuangalia bazazi wanalewa cku nzima.

Kwa mutechnology ya leo, huezi ukaepuka

Nikupe mfano Juzi nilikuwa natizama fainali za NFL footbal, wakati kocha wa Eagles akihojiwa familia yake ikaja kumlaki na kumpongeza, kilichonishtua ni pale mwanae wa miaka ka 2 tatu hivi akabebwa na babake, mkononi kana simu ya iPhone. Unafikiri atakuwa anafanyia nn cmu hio?

Balinishangaza pia kuwaona batoto bya miaka 9,10,13,15 vinazimia ety kwasababu wamemuona Taylor Swift. Nilisikitika sana banajiita Swiftiz

tusiwache batoto bawe kwa mutelefonee cku nzima. Tunaeza epuka kuporomoka kwa maadili ya batoto yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…