Iko hivii, kwanini pepsi inapendwa sana siku hizi kuliko vinywaji vingine vya cocacola kama zamani zilivyokua zinapendwa. Tatizo lilianzia kwenye bei, kuna kipindi soda za coca zilipandisha bei mpaka miasita 600, na pepsi pia,,, lakini pepsi akaona fursa kwa watu baada ya kuona hawakupendezwa na ile bei, Pepsi akashusha bei soda zake zote iwe 500,, kwa maana ukiwa na 1000, unapata soda 2 sio moja tena,, huku coca aliyejitengenezea soko akakomaa na 600,, Watu wakachangamkia sana pepsi za jero hata kwa wasiozipenda ikawalazimu wanywe tu ili kwenda sawa na bajeti,, watu wakajikuta wamezipenda na kuzizoea sana pepsi na mirinda,, huku soko la coca likishuka,,, Cocacola kuja kustuka tayari wameachwa pakubwa saaaana, nao wakapunguza bei,, lakini wakiwa washachelewa, watu washauonja utamu wa pepsi na mirinda na kuwanogea,,,Ndo maana mpaka sasa Pepsi inaongoza kwa mauzo sana kuliko coca.. kuna pepsi big pia kumbuka[emoji16] nao wataiga tu.