Moja ya kinywaji laini (soft drinks) kinachopendwa Bongo Pepsi inaongoza

Moja ya kinywaji laini (soft drinks) kinachopendwa Bongo Pepsi inaongoza

Iko hivii, kwanini pepsi inapendwa sana siku hizi kuliko vinywaji vingine vya cocacola kama zamani zilivyokua zinapendwa. Tatizo lilianzia kwenye bei, kuna kipindi soda za coca zilipandisha bei mpaka miasita 600, na pepsi pia,,, lakini pepsi akaona fursa kwa watu baada ya kuona hawakupendezwa na ile bei, Pepsi akashusha bei soda zake zote iwe 500,, kwa maana ukiwa na 1000, unapata soda 2 sio moja tena,, huku coca aliyejitengenezea soko akakomaa na 600,, Watu wakachangamkia sana pepsi za jero hata kwa wasiozipenda ikawalazimu wanywe tu ili kwenda sawa na bajeti,, watu wakajikuta wamezipenda na kuzizoea sana pepsi na mirinda,, huku soko la coca likishuka,,, Cocacola kuja kustuka tayari wameachwa pakubwa saaaana, nao wakapunguza bei,, lakini wakiwa washachelewa, watu washauonja utamu wa pepsi na mirinda na kuwanogea,,,Ndo maana mpaka sasa Pepsi inaongoza kwa mauzo sana kuliko coca.. kuna pepsi big pia kumbuka[emoji16] nao wataiga tu.
Umeongea ukweli mkuu, Pricing strategy walioadopt Pepsi iliwarudisha kwenye ramani maana walipoteaga kabisa enzi zile wanatumia creti za mbao 😂😂😂
 
Mi soda yangu pendwa ilikuwa VIMTO. Sijui hata ilipotelea wapi hii kitu jamani. Nilikuwa napiga chupa hadi 3 kwa mpigo.
 
Mi nimeacha rasmi mwaka jana baada ya kuwa teja la pepsi. Nilkuwa nikiamka naiwaza kumbe wanatia coccaine unakuwa na arosto. Watu hawajashtuka. Bas tu binadam huwa tu ajiua taratib had tukilazwa hudhan tumeanza siku hiyo. Siamin mimi kuacha peps na aina zote za soda na vinywaj vya aina hiyo.
Hongera mkuu soda siyo kabisa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Naona Pepsi inazidi kupendwa sana na wabongo, sijui kwanini juzi kati nilikuwa Dar kama unavyojua Dar jua kali sana sehemu za vinywaji laini wengi walikuwa wanaagiza pepsi na maji.

Sasa hivi mkoa niliopo kulikuwa na sherehe mahali nami nikawepo hapo kulikuwa hamna pombe bali ni aina zote za soda lakini wengi walikuwa wanaagiza waletewe pepsi.

Hata ukicheki mida ya mchana ile time watu hawanywi pombe wakiwa bar au wap wengi huagiza pepsi tu.

Hongereni pepsi maana hata hapa nilipo kaa sasa hivi napata pepsi yangu ya baridi.
Pepsi ipo vizuri sana
 
Dah! Huu utafiti wako aisee unachekesha... anyway huku nilipo vinywaji vya energy vinatumiwa sana na vinapendwa mpaka na waliokatazwa kuvitumia
Wote mturushie picha tuone kinywaji gani ni pendwa zaidi Kati ya hivyo.
 
Kuna kipindi nilikuwa mteja wa Mirinda nyeusi sana mpaka ikafikia stage nikawa nikinywa nahisi mwili una badilika. Nahisi kizungu zungu dah nikaacha aisee.
Ile kitu ni hatari sana mkuu,kuna mtu namfahamu vzr alikua hanywi pombe kabisa lkn daily ilikua lazima anywe hio kitu.

Sa hivi anasumbuliwa na kisukari hatari.
 
Ni kweli hata maji kifungashio Cha maji ya afya kilikuwa Cha kuvutia soko lao likapanda na uhai ikapoteza soko lakini uhai imerudi kwa kasi sana lita 1.6 ni mia tano wakati afya lita 1.5 ni mia sita na lita1 ndiyo mia tano
 
Yap,hasa ukikutana na lile pepsi big,unahangaika nalo wee mpaka nafsi inasuhuzika.

pepsi[emoji818]
peps[emoji777]
Hivi faiza fox siku hizi Yuko wapi? Alikuwa anapenda Sana kurekebisha makosa kwenye kiswahili.natamani aendeleze kazi yake.
 
Back
Top Bottom