Moja ya kumbukumbu mbaya machimboni nchini Msumbiji. Lakini maisha lazima yaendelee

Moja ya kumbukumbu mbaya machimboni nchini Msumbiji. Lakini maisha lazima yaendelee

Asante. Bado una utoto mwingi sana. Angalia umri ulionao halafu unang'ang'ania mtu akuandikie story usome kwa lazima.
Unanitukana unanijua? Utakuja uumie kwa ujinga wako. Hii dunia ni pana sana kijana

Asante. Bado una utoto mwingi sana. Angalia umri ulionao halafu unang'ang'ania mtu akuandikie story usome kwa lazima.
Unanitukana unanijua? Utakuja uumie kwa ujinga wako. Hii dunia ni pana sana kijana
Sorry Mkuu
 
Story la ki hustler!respect bro!ila ni jimbo gani hilo?sio cabo de lgado kwa wazee wa takbiiir..
 
Story la ki hustler!respect bro!ila ni jimbo gani hilo?sio cabo de lgado kwa wazee wa takbiiir..
Kuna jamaa humu anaitwa Kitoabu alituhadithia habari za #Lupaso na mambo mengineyo ya huko cabo...

Naye ni mchimbaji kutoka pande hizohizo!! Hakika stori za huko zinanoga sana!!
 
kule nilibaki Mimi,, nikabaki nasimamia (karasha) mashine ya kusaga mawe Ila sasa ushuru ukawa changamoto unafatana Sana mashine ndio Ivo aitulii kuharibika kila muda.
Tukawa na madeni mengi tunadaiwa tukikopa pesa labda kuweka Mambo fresh ndio Kwanza tunaongeza madeni inakua ngumu Sana kulipa hili likawa janga kubwa

Tuendelee 04
Baada ya Mimi kubaki kule na kuendelea na kazi Ila sasa sikua nikinunua tena dhahabu zaidi ni Mimi na msagaji wa mawe tulikua tunapiga kazi tunakusanya pesa mdogo mdogo tunalipa ushuru na sie tunatoa pesa ya kula hapo hapo.

Wakati huo pia madeni baadhi nilikua nikikusanya ambao walilipa ikawa Sawa ambao walikimbia ikawa basi tunakutana njiani lakini akuna jipya zaidi ni kusema Tu subiri,, tuangalie kesho kuna siku nikapanda mlimani kwenda kupiga simu njiani nikapishana na Mzee mmoja hivi wakati napandisha nikakuta pesa elfu 40 zimeangushwa.

Nikaziokota na kutia mfukoni alafu nipo katika kipindi cha uhitaji Sana wa pesa, nikatulia kule juu mtandaoni nikajiunga bando la msumbiji nikaanza peruzi mtandaoni nikaanza angalia humu thread za watu ambao walishafanya biashara ya samaki sababu nilisikiaga samaki wanatoa faida nusu kwa nusu kulingana na mtaji sasa kipindi hicho niliwaza labda ule muda niweze kukusanya vimadeni then nikirudi tz niingie mtera kwenye samaki.

Kipindi nipo tz kuna teacher mmoja alikua anafundisha beroya secondary, bahati mbaya alifukuzwa, baada ya kufukuzwa akaingia kwenye hii biashara sio haba ilikua ikimlipa alifanikiwa kununua pikikpi 5 kupitia hii biashara na nilikua na namba yake nikamcheki watsap kweli alirespond Ila aliniambia kwa sasa aliacha sijui kulikua na changamoto gani huko mtera nahisi walifunga lile bwawa kitu ka icho.

Basi nikaendelea kuperuzi kidogo akaja yule Mzee niliepishana nae akaniambia kaangusha pesa elfu 50 kama nimeiyona na iyo pesa katoka kuuza dhahabu wakati huo Mimi nimeokota elfu 40 nikamwambia sijaona pesa Mzee nikaanza msaidia kuitafuta kama sio Mimi vile baadae akasema basi ishapotea akaondoka nilimuonea huruma Ila wakati huo na Mimi Nina shida Sana ya pesa mungu anisamehe.

Nilipomaliza kule mtandaoni kuperuzi nikarudi mpaka pale kijiweni kwetu kiwandani nafika pale kaja kiongozi flani na karatasi lile karatasi Lina majina ya wote wenye viwanda na wanunuzi wa madini hawa wanaitwa LUPILICHI hawa huwa na kawaida ya kupita kila baada ya miezi 6.
Walikua wanahitaji pesa ambayo ndio inalipwa kila baada ya miezi 6 shilingi laki4

Hapa ndio nikaona hawa wanacheza na hukata tulio nao huu laki nne inatoaka wapi nikamwambia yule kiongozi ngoja tujichange alafu tutaileta akasema lini nikamwambia itakapotimia akasema wale hawana muda wanaondoka nikamwambia wakiondoka basi sasa tufanyeje Sisi kama pesa aipo wakati huo na Mimi nimevurugwa sitaki ujinga.

Jamaa akasepa Sisi tukaendelea na kazi baadae akaja mwingine uyu ni wa msumbiji kabisa lakini Kiswahili anaongea vizuri Tu na ni kiongozi pale akasema tusimame kazi mpaka tutakapo lipa pesa,, nikamwambia tuna mizigo pale nafikiri ikiisha tutakua tushatimiza iyo pesa so tupe muda tunakuja kulipa akasema Sawa ila tusichenge.

Basi tukaendelea, siku ya pili asubuhi Tu mashine ikabuma kumsaka fundi akaja tengeneza Ila vinahitajika vifaa kukamilisha ufundi wa Ile mashine piga hesabu pesa nyingi inahitajika yote tulioingiza inabidi tuingize kwenye ufundi na ya kumlipa fundi.

Mhmm ni Mambo juu ya Mambo nikampigia mshikaji simu akasema we komaa Tu mwanangu utakua unanipa mrejesho kila kinachotokea. Mashine ilipona tuaka endelea na kazi nikakusanya kama laki moja ivi jama hawa hapa wale wa LUPILICHI nikawaambia sina pesa mashine iliharibika mtuvumilie awataki nika waambia basi fanyeni mnachoweza Sisi atuna la zaidi kama mnakataa ujue Amna kitu hapa, wakasema zima mashine na akuna kuwasha mpaka pesa iletwe ofisini.

Mizigo iliyokuepo ikahamishwa wachimbaji wakaenda saga sehemu nyingne mfukoni Nina laki kama na 25 ukiacha pesa kidogo nilimuachia msagaji ya matumizi maana sasa niliona kila mtu afie kwake akuna la zaidi ukizingatia wametupiga stop no job.

Nikabaki pale msumbiji nikiendelea kukusanya vimadeni mpaka vikafika laki na elfu 10 hii ikawa yangu sasa na hii pesa niliyo kusanya madeni na kufika kiasi hicho kuna siku nilikua geto akaja mchimbaji kuniuzia dhahabu nikamwambia sina pesa akasema ngoja basi nipime Tu kuipima ni gram moja na point moja Sawa na laki moja na elfu 10 nikamwambia kama iyo ninayo nikampa Ile pesa nikabaki na dhahabu pamoja na pesa iliyotoka mashineni Ile laki na elfu 25.

Usiku mida kama ya saa tatu nikaona niende baa ku refresh ubongo kidogo kupoteza mawazo na kujichanganya na Wana nimefika nikaagiza soda na kuanza kunywa taratibu na story za hapa na pale mule ndani kuna warembo alafu kuna kademu nilikua nakafatilia Sana wakati kafika Tu sasa hawa mademu wakija pale mwanzo watu huwa wanawashobokea Sana kwaiyo kuna watu wanahonga Sana kumpata hapo mtihani Ila akishakaa Miez 2 ivi watu wamekula na kusepa anapitia ukata hapo ukimfata ni kiulaini unaenda kula mzigo.

Sasa kwa vile nae analijua Hilo nilisha mfataga Sana akachomoa akaanza kujisogeza kwangu nikaona ndio muda huu nikamnunulia bia moja nikampanga aje geto na geto analifahamu so ikawa fresh nimepiga soda taratibu mpaka saa sita usiku nikaondoka kuelekea geto yeye akasema anakuja.
Nimefika geto bana nikatoa pesa iliyobaki mfukoni na Nina kumbuka nilikua na dhahabu zile dhahabu sikuziona tafuta wapi angalia mule ndani akuna sachi mifukoni Amna nikakumbuka inawezekana muda niliokua nalipa pesa mfuko niliotoa ndio Ile dhahabu ilikuepo nimeiviriga kwenye karatasi la sigara lile la ndani ZIGI so nikaona kabisa muda ule niliangusha pale kwenye baa.

Nikarudi kwenda kucheki sikuambulia kitu yawezekana wahuni walishaokota da niliona huu mkosi gram moja na point moja Sawa na laki na 10 zimepotea nilijilaumu Sana Sana sijui kwann sikupata wazo la kuacha geto
Nikarudi geto kinyonge Sana mawazo kibao aisee nikatulia kitandani nimewaza Sana akuna jipya zaidi ya mawazo. Yule demu akaja bana akagonga mlango sikuamka aligonga mwisho akasepa niliona kiwingu tu
Nikalala zangu mpaka asubuhi hapo akuna kufanya kazi wala nini sababu tulisha simamishwa.

Ikawa ni kuzurula Tu mshikaji nikawasiliana nae akasema kama vipi mwanangu we sepa tukane tz uko inabidi tujipange tena nikamwambia poa Aina noma Ila sasa hapo Nina Ile pesa iliyobaki ya mashine ukiacha Ile ya dhahabu iliyopotea so na zingine nikawa napata ambazo ndio nilikua nakula.

Nikawa nina mawazo Sana sababu nageuka tz naenda Anza maisha upya nimekaa mwaka mmoja na miezi mitano msumbiji toka nitoke tz narudi sina pesa ya maana alafu ni muda mrefu Sana je home watakuonaje unawaambia nini wife nae namwambia nini lakini nikajipa moyo japo Pana changamoto zimetokea lakini mshikaji hawezi kuniachia ivi ivi lazima Tu atanitoa.

Usiku wake baada ya Jana kupita ule usiku mbaya ambao nimepoteza dhahabu nikaenda tena kwenye Ile bar nikaagiza soda yule demu akaja akaniambia alifika Ila aligonga Sana nikamwambia ulichelewa nilipitiwa na usingizi akasema basi baadae nakuja nikamwambia poa nikanywa soda Ile nikalipa nikasepa geto.
Yule demu alikuja uyu demu alikua kama Ka tomboy flani Ila kapo vizuri ki ukweli basi kaja muda umefika wa kupelekeana moto.

Nimevaa condom nikaanza kupiga shimo piga mzigo piga wakati tupo Kati Kati ya gemu akasema nichomoe condom kwani asikii utamu na condom mhm aikuwezekana Kwanza niliwaza inaonekana uyu kote anakopita ni mwendo wa kavu kavu sasa hapa magonjwa ni kujichotea Tu mi nikapiga mpaka nilipoona hapa nimetosheka fresh Ila ndom sikuweza vua.
Demu aliondoka asubuhi nikampa elfu 10 akasepa zake.

Iyo asubuhi mi nikajiandaa zangu nikaweka kila kitu fresh beg langu la nguo na kila kitu kwa safari pale sikupanda pikipiki kwanza kabla nilitanguliza beg langu mbele,, nikaliacha sehemu ilikua asubuhi Sana alafu nikarudi nikamuaga yule msagaji na watu wachache na kusepa zangu nikampanga boda flani anikute mbele namsubiri kumbe kapata abiria mwingine nimekaa mpaka
saa tano asubuhi sina uhakika wa kuondoka nikaona ujinga hapa siwezi ludi nyuma.

Nikaanza kuuchapa kwa mguu ili pkpki itakayonikuta mbele inibebe ukizingatia kule kuna machimbo nyingi tofauti so nikajua kabisa njiani ntapata boda but siludi nyuma.

wakuu kesho tukutane .....

Poleni kwa uandishi wangu
 
Story la ki hustler!respect bro!ila ni jimbo gani hilo?sio cabo de lgado kwa wazee wa takbiiir..
Hapana pale ni Jimbo la niassa lugha nyepes (Nyasa) but sio Nyasa kwenye dagaa.
 
Nikaanza kuuchapa kwa mguu ili pkpki itakayonikuta mbele inibebe ukizingatia kule kuna machimbo nyingi tofauti so nikajua kabisa njiani ntapata boda but siludi nyuma.

Tuendelee 05
Nikakanyaga kwa mguu begi kubwa mgongoni Nina bonge la koti la kaki, chini kiatu converse kubwa black leza
alafu jua lilikua Kali siku Ile nakumbuka
pori Kwa pori msitu Kwa msitu pikipki zinakuja zipo full nafasi Amna ikabidi nizidi kusonga taratibu sehemu penye mtandao nampiga mshikaji simu namuelekeza nilipo anachoniambia ni yah kaza mtoto wa kiume ndio safari za kiume izo.

Nilipiga mwendo mpaka getini ambapo hapo ndio unaacha mpaka wa msumbiji na unaitafuta Tz pale getini wakaniuliza Tu maswali flani na nikalipa elfu 5 na hata kule nako nililipa elfu 5 wakati natoka nakumbuka nilimkuta Askari bonge ivi akaniambia mwanangu subiri Tu hapa pikipiki utapata usiwe na pressure na alikua anaongea Kiswahili fresh Tu.
Kweli nikasubiri pale kuna pikipiki ilitoka boda inampeleka abiria kule pori akasema sio muda anarudi niandae elfu kumi nikamsumbiri pale saa nzima mpaka alivyorudi nikapanda chuma ndefu saa nzima tupo njian mpaka boda kivukoni.

Pale tukapanda mtumbwi mpaka ng'ambo mishale inasoma saa7 iyo nikashuka pale na kusubiri bus ambayo hua inaingia pale saa 8 inashusha na inaanza safari ya kurudi songea aikua chukua muda ikawadia tukapanda pale palikua na abiria wengine na safari ya kuitafuta songea kuanza.
Wakuu hapo sasa nakaribia home naiyona home hii hapa mawazo ndio Kwanza yanaanza aisee acheni Tu, akuna kitu nilikula zaidi ya pale boda kula mua Tu na baadae kunywa maji basi.

Tulisonga mpaka mida ya saa moja jioni hatimae tunaingia songea stend mshikaji nilimkuta ananisubiri pale nimeshuka salamu za siku kitambo kidogo kilipita toka tuachane tukapiga stor nyingi sikua na mood ki ukweli Ila tuliongea Sana mpaka saa mbili ivi akaniuliza pesa niliyobaki nayo nikamwambia ipo laki na elfu 6 niliamini hii ataniachia ya kuanza maisha mapya after one year and five month's akasema basi nipe elfu 40 mwanangu nyingine Baki nayo nikampatia tukaagana mi nikatoka mpaka saloon flani ivi nikanyoa nywele zangu.

Kisha nikatoka mpaka kijiwe cha boda saa tatu usiku iyo sasa kabla sijachukua boda simu yangu iliita alikua ni demu flani nilikua natoka nae kule msumbiji nae wa songea Ila tulijuana kule,, na tulijuana wakati huo yupo mwishoni kumaliza mkataba wake ivyo aliondoka mi nikamwambia sina mda mrefu ntakua huko alikua akituma Sana watu nikampigie wakati Niko msumbiji
uyu demu alinikubali Sana Mimi pia........ na kipindi chote icho ata akija geto akuwai niomba pesa mpaka nimpelekee nisipo mpa ndio basi kuna muda yeye mpaka chakula alininunulia,

kuna soda nilikua naipenda Sana kwajili ya kifua daily ilikua lazima aniletee geto kuna siku nimeenda baan kwao nikaagiza iyo soda alinhudumia mdada mwingine wakati ananiletea aliiyona Ile soda alitoa macho kwenye Ile soda akamtazama yule mdada akageuka nilipo Mimi kunichek mi nikachengesha macho Ka simuoni ivi kumbe napiga jicho kinyonga, uyu ilikua ata nikimkuta yupo na wenzake anapiga stor Kwa sauti akiniona anashtuka na anapoteza kabisa kujiamini hasa iyo Hali niliijua so nikawa napita nimevimba Ka dume la nyani ivi....

Basi Ile simu kupokea Tu akatulia sekunde kazaa kisha akasema usiniambie upo msumbiji nasikia kelele za pikipiki na honi za magari, miziki kule mlimani Amna ivyo niambie upo wapi ibu nimekumiss Sana tafazali niambie ahaa kidume nikasema nilipo nikasikia yeeeeebo akasema soon nakuja.
Nimetulia kama dakika 5 simu inaita yeye akauliza nilipo nikamwambia akaja mgongoni kwangu akanikumbatia mwanana tukapiga stor Sana pale alafu alikua kanenepa umbo limezidi kuchongeka msambwanda sasa mhm

Tukatoka mpaka kwenye mgahawa flani tukaagiza wali maziwa izo siku zote msumbiji maziwa ya ng'ombe nilikunywa siku moja Tu Lita 2500 tukagonga msosi tukiendelea na stor tukasepa pale njiani story nyingi Sana mpaka saa 5 usiku akapigiwa simu bwana na mama mwenye nyumba wake akamuuliza upo wapi tunataka kufunga mlango akanigeukia Mimi akaniuliza vipi narudi ib? nikamwambia nenda J tuonane kesho si unaona nimechoka wacha nikapumzike hom akasema Sawa sikumwambia kama Nina mke tukaagana akasepa.

Mimi uyo mpaka home pale home yupo shangaz yangu na wife Ile nimefika wife yupo chohoni nikagonga wife akauliza Nani sikujibu shangaz akasema mbona sijasikia mtu akigonga wife akaenda chumbani nikagonga ya pili shangaz ndio akajua panagongwa akaamka kunifungulia shangazi akashangaa ehee shangazi usiku wote huu karibu jamani karibu Sana nikakaribia mpaka ndani nikasalimiana na shangazi pale then uyo chumbani kwangu.

Mlango wife aliacha wazi kumbuka Pana dakika 5 takribani toka atoke toilet nimeingia nimeshusha begi nime change nguo wife ananiona ajaamka nimeenda jikoni nimechukua maji mpaka bafun kuoga nimerudi ajaamka nimejiweka fresh toka alivyo mute mpaka nalala na ninajua kabisa yupo macho toka alivyo kauka na Mimi nikaona nikaushe sio ishu maana mapokezi niliyo tarajia ni tofaut Bora ningeenda kutwanga yule mchepuko nilimwambia nimechoka Kwa kujua home yupo Nani.

Ila ajabu nikayakuta Ayo piga mbonji mpaka asubuhi yeye aliwahi amka kitandani pale nikabaki Mimi na mtoto wangu wa kiume uyu ni second born niliondoka yupo mdogo ndio anaanza kutembea Tu kuongea bado bado Ila hapo nilikua naiyona njemba aisee mpaka mwenyewe nacheka dogo akashtuka nae akanicheki akatamka Baba rudi sikumjibu akashuka kitandani akaenda jikoni Kwa mama ake nikamsikia anasema mama alafu mama ake anaitika kisha anamwambia Baba ndani kule mam ake ajibu aliongea ivyo zaidi ya mara tatu.

Wife ana vibiashara vyake lakini sikuacha mtumia pesa wakati nipo ng'ambo ilikua kila tarehe 1 natuma si chini ya 50 alafu tarehe 15 natuma tena na tarehe 1 au 30 natuma pesa kama kawaida kuna vitu nilikuta kanunua ambavyo wife namjua pesa yake sio easy kununua kitu kwajili ya familia nikajua kabisa pesa nilizokua natuma kajiongeza nikamuuliza ivi vitu vya nani akasema vya kwangu nikamuuliza vya kwako akasema ndio nimenunua Mimi nikajibu Oho Sawa nikaona ubinafsi ule ndio huu chake chake na changu cha wote.

Nikachukulia easy Tu kamaliza shughuli zake neno alilo niambia ni hili utaacha pesa Kwa shangaz mhmm nikamjibu Sawa ntaacha hii pesa hua anaacha kwajili ya shangazi anabaki na madogo pale home ili ndio neno alilonipa wakuu kumbuka toka nimefika hata salamu Amna kunijulia Hali nilikotoka akuna labda za safari akuna na je umerudi tunaanzaje maisha mume akuna labda mume kaondoka muda mrefu Leo naghairi ata kwenye biashara siendi akuna ni akuna Tu akasepa zake.

Jioni aliwai Rudi akafanya mishe zake mi badae nimetoka kuchek mechi narudi nikamkuta anacheki series za kihindi akaanda Tu msosi basi nikala nikaanzisha stor nikaona kabisa anajibu Kwa kujilazimisha mhm Mzee mzima nikavuta shuka nikalala iyo Hali ilidumu mpaka siku tatu.
Siku iyo anaaga anaondoka nikamuuliza mama J mbona sikuelewi yani toka nimerudi upo busy ivi huo ubusy wa namna gani hata kukaa na Mimi akuna nikueleweje?! Akasema ivi wewe unayofanya uyaoni nikamwambia yapi Ayo akajibu sijui mwenyewe ahaaa hapa tuliongea na kubishana Sana mwisho nikasema ok watoto si hawa wamekua mwingine yupo darasa la pili mwingine ndio uyo akipiga chai basi Yuko na mishe zake kitaa basi Sawa tulee watoto ambae yatamshinda atanyosha mikono full stop.

Maisha yaka endelea kila mtu Yuko bize na Mimi nipo na stress zangu hapa Kati yapo mengi mengi Tu ok
Back Kwa mshikaji alikua na dhahabu kidogo alienda dar akauza dhahabu akarudi siku iyo akanicheki yupo pub flani ivi nikaenda kuanzia mida ya saa 3 tukapiga stor Sana akaniambia na faida iliopatikana akasema Kwa sasa anatulia Kwanza mjini hapa akawa anaagiza safari baridi anapiga sinywi pombe nikaagiza soda na chips za kutosha nikala piga Sana story mpaka saa Saba ivi Ile pub wkaanza kufunga tukahamia kwingine.

Pale akaanza tena agiza castle mi nikachukua juis,,,,,,,story na mziki taratibu vinaendelea mpaka saa8 usiku akapita demu flani alikua msumbiji mi ndie niliemuona tukamwita jamaa akaanza ongea nae akampanga akale mbususu na ndio kasha zoea maisha ya kule pori chap cha fasta wakaondoka kwenda kusaka gest muda mfupi wakarudi jamaa akasema gest zote zimefungwa akapiga mafundo kazaa ya bia akamchukua demu tena wakaondoka na tayar Alisha mnunulia bia kazaa hapo.

Wakasepa mi nipo zangu alone na Mimi sio muongeaji Sana nipo kimya Tu pale na simu yangu na play games baadae wakarudi jamaa akaniambia amepiga mbususu mpenyoni amemuinamisha Tu amepiga kimoko kiroho akampa elfu 5 demu akulizika na Ile pesa kaja kafula kanuna mbaya ahaa si tukampotezea Tu .

Pale tulikaa mpaka mida ya saa kumi na moja alfajiri mke wa jamaa anapiga simu sio mchezo jamaa akasema mwanangu saiz tusepe inaenda asubuhi hii akazama mfukoni akatoa pesa akaicheki akanipa mwana ya pikipiki iyo ilikua ni shilingi elfu moja nakazia buku dah pale sikuonesha mshtuko Ila Tu lilibaki moyoni na kukesha kwenye ma pub ni kama nilikua namsapoti yeye ananipa buku kudadeki tukaagana kiroho akasepa aisee niliwaza Sana nilijua hii ndio golden day ya kunipa mzigo baada ya kutoka Dar angalau nianze maisha kivingine mjini hapa du buku sikupanda pikipiki nikatembea mdogo mdogo na sikuiz njiani wameweka taa basi mpaka home.

Nikachukua funguo wanapoweka sababu nilibaki nje Mimi nikaingia ndani kulala wife anashtuka ananiambia saizi ndio umeamua kurudi asubuhi nikamwambia ina maana mpaka useme saizi Nimeamua kwani kuna Jambo gani limetokea na kupelekea mi kujiamlia kurudi asubuhi? mpaka useme ivyo je nilikua kazini unajuaje akasema niwekee pesa mezani pale si ulikua kazini nikamwambia je nafanya kazi ya ulinzi mshahara mwisho wa mwezi iyo pesa ya usiku Nimepata wapi we si utaki ata kuniuliza michakato yangu utajuaje?.

Akakaa kimya nikapiga mbonji asubuhi kumekucha akaanza kuongea Mambo yake ya ajabu ajabu kuna kipindi hapa mwishoni baada ya Mambo kuyumba kabla sijarudi ulipita mwez sikutuma pesa akaongelea iyo ishu dahaa nikamwambia siku zote natuma pesa mwishoni Mambo yangu ayakua vizuri nikashindwa kabisa kutuma pesa sasa iyo ndio unaongea ivi Nani ambae Mambo yake muda wote yatakaa Sawa Tu nikamwambia tena si upo bize utajuaje Mambo yangu huwezi elewa ujui nini kimenikuta wakati huo kale Ka pesa nilikobaki nako baada ya kurudi kalishaisha hapo ilikua mwendo wa kuunga ungaa Tu kitaa.

Uyo Mzee nikaingia na mizunguko yangu yule demu aliefika kunifata stend siku iyo akanicheki tukapiga story akasema kamiss gemu nikaona Yaha wife mwenyewe ananizingua Tu akaja mpaka lodge akalipa kila kitu nikachakaza mbususu demu alinimisi Sana alikua na mizuka balaa.
Toka saa kumi tukaja achana saa mbili usiku ivi nikampeleka mpaka kwake nikageuka zangu.

Nimerudi home bado kichwa akijatulia nawaza naingilia wapi na mishe taiti Sana nafanyaje wife akaanza vimaneno vyake na katika kubishana bishana akaja akatoa kauli hii hapo ulipo hata kitu chochote ujawai ni nunulia we mwanaume vipi akaropoka kishenzi nikamwambia unasemaje wewe nilijizuia Sana nilitaka nimchalaze makofi Ila nikaamua kuacha nikamtazama Kwa ghadhabu Sana nikamuuliza hapa juzi vitenge vimetoka msumbiji vya wewe na shangazi je ulinipa ela yako ni nunue?

Akakaa kimya alafu akasema si ndio ivyo Tu.
Nikamwambia ayo madela pesa alitoa Nani Ayo magauni pesa alikupa nan umesahau hizi sendo zilizo humu ndani za msumbiji pesa katoa Nani Ayo makoti
nilimuolozeshea vitu kibao japo aistahili akaona kaingia cha kiume akavuta shuka na kujifunika gubi gubi alinikera sana nikakaa kimya nikavuta shuka na kulala zangu.

Maisha yalisonga jamaa yangu nikimcheki angalau aniwezeshe kauli ni moja subiri Kwanza mwanangu ndio kauli yake ehee nikaona poa Ila wakati huu niliwaza sasa hapa niludi msumbiji kuna washikaji nilishwapanga Mambo yakienda ovyo ntarudi tujumuike tuchimbe waliniambia nisijali we mwanetu njoo Tu tutaungana kutafuta chochote, nikamuelekeza jamaa yangu kama vipi anikopeshe nauli ya kurudi msumbiji hii mesag nilituma ilikua kitu Ka saa 8 usiku nilikua sijalala nawaza kesho yangu.

Asubuhi jamaa alinicheki akasema sikilizia mwanangu usiwe na hofu naweka Mambo fresh tutarudi kupiga mishe tulia Tu sio muda nikamwambia mi nitangulie hapa town mishe Amna akasema Aina haja ya kuwai.
Aha dadadeki mi nahuwawa na maisha nimebanwa unipi sapoti yeyote alafu unasema nitulie Tu nikaona mwanangu ana masihara Sana na nikahisi kama anitakii mema ivi kutokana na ivyo visa.

Nikaendelea kuunga kitaa nikasonga kibishi nikiokoa nanunua mahitaji napeleka home siku zinakwenda na nikipata vijisent vya kutosha kwenye madili huko na nunua mahitaji ya kutosha home.
Kuna jamaa yangu akanipa mchongo nae anapitia life gumu na alishawai fanya kazi pub moja mjini na alikua anachukua pesa nzur na yeye na wife wake kimenyata tena yeye ndio balaha sababu ana mfatilia mno muda wote anahisi kuibiwa Tu kuna siku nilimwambia yanayo endelea kwangu akasema mi mkatili nikamwambia ukiwaza Sana mwanamke utaacha kufanya vitu vya msingi waza mwanao kesho anaishiji we mwenyew utaishi wapi nyumba unayokaa ya Mzee je inakuaje ?! Jamaa atajibu Sawa kesho nasikia nimekuta wife anakunywa pombe nyumbani akumbuki kurudi na wakati huo uyu wife wake alimpatia uko pub.

Basi ule mchongo akanidokeza tukasepa wote siku ya kusepa nika muaga wife naenda sehemu flani kuna Ka job na huko tunasafiri alichojibu yeye ni haya akuuliza kazi gani, na ninakaa muda gani mpaka kurudi au chochote kile juu ya iyo kazi hili nalo lilikua jipya kwangu
sitataja kazi gani ila ni kazi halali,,. kwenda kule Ile tumefika mashine zimeharibika baada ya kama siku tatu ivi zikapona tukaingia mzigoni ng'ombe wa masikini hazai nikaumia mkono huu mkono niliwai vunjika kwenye mpira Aya mandondo nilifunga P.O.P mwezi mzima.

wakati huo napiga center half moja matata Sana Acha ukiniweka kiungo mkabaji
namba 6 pia kiungo mchezeshaji namba 8 pia wingi ya kushoto namba 11

wapo wachezaji niliocheza nao kitaa wapo ligi kuu sasa,,. polisi tz wapo wawili mmoja wao juzi mechi ya (polis vs prison) alipiga kros iliyozaa bao akitokea wingi ya kushoto ,

Kwa wanaofatilia NBC ligi wanamjua alafu ihefu yupo mmoja,,, ruvu shooting wawili,,, jkt ruvu ya daraja la Kwanza mmoja, namungo yupo mmoja,, mbeya city mmoja Ila uyu nilicheza nae prymary na alinizidi madarasa.

Tuendelee mkono kwa muda huu aukuvunjika ni kama Tu ulishtuka lakini ulikua na maumivu Sana nikaugulia pale labda nivute muda wapi auponi ikanilazimu kurudi home siku narudi home nikamwambia wife nimeumia mkono so sijafanya kazi kabisa narudi ivyo niambie funguo utaweka wapi ukitoka maana yule shangazi aliondoka.

Akajibu utaikuta sehemu flani swala la Mimi kuhumia akuulizia labda kimenikuta nini na hata kufatilia kujua wapi akuna.
Nimerudi home nikafunga clip bandage sio ile ngumu p.o.p hapana sio iyo basi nikasonga na mishe zingine.
Asubuhi yake bana baada ya kufika home toka nihumie wife aliniamsha alafu akaniambia naomba hela,,,, nikamwambia yani wewe mtu wa ajabu Sana yawezekana unatamani nife unaulizia pesa
Na sio afya kwanza
ivi Mimi bila afya njema nitatoa wapi pesa?
Ata kunijulia Hali Hali kweli? Alikaa kimya akaondoka sijui aliona kakosea au aibu tu

Basi Nikamcheki yule jamaa yangu kumueleza Hali iliyonikuta akasema Tu pole mwanangu ndio uhanaume huo nikaona hapa nimekutana na chuma chikoli Moto nikapanga mishe zangu alafu kuna jamaa wa kule msumbiji alinicheki kwenye simu tulipangana ntarudi alinicheki nikamwambia naweka ishu fresh nakuja soon Ila saiz niliumia mkono jamaa akunitupa alinitumia pesa flani si haba ambayo ilikimbiza siku

Ilibidi nimalize stor sema nimeugua Sana tumbo na hata kuandika nimejikaza sana
Tukutane kesho.....

Uandishi tuvumiliane

N.B
>>>Wakuu hapo juu machache nimejaribu kueleza japo ayapo kule niliko toka nimeona niguse kidogo sio mbayaMsije sema nimeenda nje ya mada hapana.
 
Nakumbuka enzi hizo unakichafua pale zimani moto na majimaji fc we unaua centafu,iddi kipagwile wa polisi Tz anapiga winga teleza mi nipo kati ya dimba nasambaza upendo...
pole sana masta
 
Nakumbuka enzi hizo unakichafua pale zimani moto na majimaji fc we unaua centafu,iddi kipagwile wa polisi Tz anapiga winga teleza mi nipo kati ya dimba nasambaza upendo...
pole sana masta
Dah Mzee umejitaid Sana kuunga dot ni kweli hapo ziman Moto tumekipiga Sana yoso kipindi icho na Kwa vipaji vile wale makocha ingekua sasa wangetoa vipaji San na kupiga hela idi nilicheza nae aisee timu moja yoso mpaka kwenye mandondo humu Ila maji maji sijachezea...
 
Nikamcheki yule jamaa yangu kumueleza Hali iliyonikuta akasema Tu pole mwanangu ndio uhanaume huo nikaona hapa nimekutana na chuma chikoli Moto nikapanga mishe zangu alafu kuna jamaa wa kule msumbiji alinicheki kwenye simu tulipangana ntarudi alinicheki nikamwambia naweka ishu fresh nakuja soon Ila saiz niliumia mkono jamaa akunitupa alinitumia pesa flani si haba ambayo ilikimbiza siku

TUMALIZE
Siku zikasonga muda ausimami maisha yanaenda hata iweje usiku utafika Tu lakini pia asubuhi itafika tu,,, wakati naendelea na kuuguza mkono [emoji113] nikivuta siku baadae nikapata dili jamaa flani aliniunganisha ilo dili ilinilazimu niende japo bado mkono aukua poa tulipiga kazi na mshikaji takribani wiki hivi tukamaliza mkono uliniuma sana.

Lakini kazi ilishaisha tukalipwa na kutawanyika kuna siku mshikaji nilimsalimu Tu kwa mesej akapiga akasema mwanangu mida ntakua town tukutane nikamwambia poa,.
Mida ilipofika direct nikapanda town nikakutana na mshikaji yupo na dogo mmoja ambae tulikua nae kule msumbiji tuliingia bar flani tukatulia pale stor nyingi jamaa akaagiza Safar na yule dogo Serengeti lite mi nikaagiza Tu azam energy tukawa tunacheki mechi pale na stor kibao.

Ile tumekaa akaja muhudumu wa pale mdada alikua kule msumbiji Alisema katoka huko sio muda na pale yupo na wenzake nao aikuchukua muda walifika jumla walikua wa tatu tukawa na stor baadae wakajichanganya na wateja wengine, jamaa aliniulizia mishe zangu hapa town nikamwambia mi naunga Tu mwanangu na juzi kuna mishe nimetoka kuimaliza saiz nauguza mikono Kwanza.

Tuliendelea na stor kuna muda yule dogo alienda toilet tukabaki na mshikaji jamaa akawa analaumu dogo anaagiza bia nyingi pesa ananitegemea Mimi nikamuuliza makubaliano yenu yalikua vipi akasema tulipanga tuje tunywe sasa bia nalipa peke angu na saiz anaagizia mpaka mademu alafu nalipa pesa yangu Tu
sikumsapoti Sana nikaacha Tu alalamike mpaka dogo aliporudi.

Baadae jamaa alitoka pale tukabaki Mimi na yule dogo,, dogo akaniuliza bro vipi,,, brother anamtaja jina alishakuwezesha kidogo au ndio Amna kabisa nikamwambia bado Ila Kuna kipindi nilimwambia akasema nisubiri
atafanya Jambo kwangu,
dogo akasema mi nikwambie kitu, brother nilimuuliza kuhusu swala lako na ukizingatia wewe umekaa muda mrefu sana kule ila alicho nijibu ni hiki

>>>kwamba wewe kule kuna kipindi ulipata shoti na hata Mimi ulishaniambia nafahamu kwaiyo kutokana na swala lile akaniambia je wewe akupe pesa ya nini? ndivyo Alisema kwaiyo hapo anakuzungusha tu akwambii ukweli dogo akaendelea lakini hata ivyo ajafanya poa angalau angekupa kiasi sio Kwamba siku zote alipata shoti zipo faida kapata na alinunua aset tunajua kupitia kaz ambayo alikupa wewe shot na faida,. Faida ipo juu kapata zaidi kuliko shoti Ila kaamua tu
Ndivyo aliniambia yule dogo nikaona hewa sasa nime ujua ukweli za kuhambiwa changanya na zako basi baadae jamaa nae akarudi tukajumuhika pale mi niliwaza Sana Ila mwisho nikaona poa sio kesi ndio mapito hayo sikukaa Sana nikaaga jamaa akaniuliza wapi sasa mbona mapema nikamwambia nawai home nimejisahau
funguo nimeondok nayo sasa wife akirudi funguo nnayo Mimi itakua tatizo akasema poa basi tuta wasiliana nikamjibu poa.

Akazama mfukoni akajisachi pale akatoa pesa ambayo ilikua shilingi Mia sita ni sarafu moja ya 500 na shilingi 100 akanipa nikapokea Ila nayo ilinishangaza yaani unapiga pombe za kutosha na kununulia mademu alafu mi ndio unanipa 600 kama ningekua nakunywa basi ningekunywa zingelipwa lakini sinywi ndio Aya nilijisemea

basi mi uyo nikasepa zangu hapa sasa nikaona akuna kutegemea tena labda kesho atanipa na wakat kila kitu nishakijua ivyo nikufanya mishe zangu Tu mungu akijalia mbeleni no new.

Kuna siku yule demu ambae nipo nae kitaa alietoka kule msumbiji na akanifata stendi siku nimerudi alinipigia simu akaniambia flani kanipigia ndio uyo jamaa yangu nikamuuliza kasemaje,.

Akasema tumeongea kidogo akaniuliza kuhusu wewe Kwamba upo hapa hapa nikamwambia mbona upo akasema ahaaa sijawasiliana nae muda mrefu rafiki angu uyu ngoja nimpigie vipi alipiga nikamwambia ajapiga na mpaka akuulize wewe mbona namba yangu anayo si angenipigia na kujua kama nipo hapa au sipo akasema hata mi nimeshangaa ndio ivyo tukaishia hapo.

siku ya pili yule dogo alienipa mchapo akapanda chuma kwenda msumbiji baada ya kufika alinipigia na tukaongea mengi Tu kubwa zaidi kuhusu Mimi sababu nilikua najipanga niweke Mambo yangu fresh then niingiie msumbiji kuchimba kumbuka sijawai fanya hii kazi ni ngumu Kwa kiasi chake Ila ukipambana na malengo yako na kuweka pesa zako hata ndogo ndogo unatoboa.

Na hilo ndio likawa wazo langu la mwisho kurejea tena msumbiji Ila Kuna vitu viwili ndani ya nafsi yangu ni kama vinashindana kimoja kinanipa go ahead ya kurudi msumbiji na kingine ni kama kina kataa nipo katikati.

Yote Kwa yote kuteleza sio kuanguka nimepoteza muda mrefu Sana akuna kitu cha malengo ambacho nimeambulia ukiacha pesa ya kula ambayo nilikua natuma home hii pesa nilipata vipi ilikua ikitokea labda dhahabu zimezidi ndio inakua ya kwangu,,,

dhahabu zinazidi vipi? mfano umepewa milioni 5 ina maana hapo ni dhahabu gram 50 sasa unakusanya dhahabu viwango tofauti tofauti labda uyu kaleta point 5 mwingine gram moja mwingine point 2 yule gram 3 pesa ikiisha iyo M5 inamaana hapo Una dhahabu gram 50
sasa unazijumlisha zote na kupima labda unakuta mzigo umezidi badala ya kua gram 50 unakuta ipo labda gram 50.6 Sawa na milioni tano na elfu 60 hii elfu 60 imezidi so inakua yangu ndio nabaki nayo.

Jamaa yangu ndio kaniacha ivyo na Kwa sasa hata simu yeye kunipigia ni mara chache Sana nahisi labda anafikiri ntaomba pesa kumbe wala mi nilisha jivua na kupambana na Hali yangu coz akipiga simu kwangu ata niulizia vipi Una hali gani mwanangu na maisha? Mi hapa Kwa sasa hivi namjibu Tu
mungu anasaidia Mambo yanaenda poa si haba atauliza tena mishe gani mbona atuambiani ni kama ziaka Tu mi namwambia Tu mjini hapa ndugu yangu si unajua kazi za saidia fundi kujenga zinatoa Kwa siku ef 5 Sana Tu
Kumbe hata sifanyi iyo nipo na Mambo yangu mengine tu.

Wazo langu kuu ni kurudi msumbiji nikaanze safari yangu nyingine ya ahadi na hapa sitokua nakaa Sana labda miezi 2 narudi tz
Bi mkubwa wangu nilimueleza hali halisi na
ana elewa kila kitu alichoniambia nikirudi kule na uyu rafiki angu akirudi tukiwa wote cha msingi Mimi nifanye shughuli zangu Ila nisiwe na tofauti yoyote au kinyongo kwake sababu Aya ni mapito Tu ambayo binamu sie hupitia kwaiyo ona kawaida Tu.

Mimi pia siwezi kumkunjia mshikaji wala kua na kinyongo nae ukiacha haya yaliyotokea uko nyuma alishanipaga sapoti nachukulia kawaida kikubwa silali njaa na muda ausimami na aitakiwi kukata tamaa nguvu ninazo uwezo wa kupambana ninao
Siludi nyuma mapambano Yana endelea.

Ayo machache nimeyaleta kwenu japo sikuweza andika yote mengine niliyasahau
Vijana wenzangu tupambane
wakuu_____MWISHO [emoji113][emoji113]

Mbarikiwe
IMG_20230222_030221.jpg
 
Back
Top Bottom