Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MOMBA: HALITETE, SHULE SHIKIZI MAZINDE; MBUNGE CONDESTER APIGWA BUTWAA
MBUNGE wa Momba Mhe. Condester Sichalwe ameshangazwa kuona shule shikizi Mazinde iliyopo kijiji cha Masanyita kata ya Mpapa Halmashauri ya Momba iliyojengwa mwaka wa fedha 2022-2023 kwa gharama ya shilingi milioni 40 kujaa nyufa kila sehemu ya kuta hali ambayo inahatarisha usalama kwa wanafunzi.
Shule shikizi Mazinde iliyopo umbali wa zaidi ya kilometa tatu kutoka shule mama ya Masanyita ilianzaishwa na wananchi mwaka 2021, kwa lengo la kusogeza huduma ya elimu karibu na wakazi wa eneo hilo.
Licha ya jengo la shule hiyo kuwa na mwaka mmoja tu tangu ujenzi wake kukamilika, imeanza kutoa nyufa ambazo zinaashiria ubovu, hali ambayo imemfanya mbunge huyo kutoamini kama kweli majengo hayo yana mwaka mmoja.
“Haya mambo yanakatisha tamaa, Rais ametupa fedha milioni 40 ili kutusaidia, lakini chakushangaza jengo limeanza kuchoka hata miaka miwili haijaisha, najiuliza hili jengo limesimamiwa na wataalam wa halmashauri kweli” Sichalwe.
Wakizungumzia changamoto hiyo diwani wa Kata ya Mpapa Mhe. George Kasonso na mtendaji wa Kta hiyo Stanslaus Sinsungwe wamesema tatizo la nyufa kwenye shule hiyo zimesababishwa na ardhi mbaya mahali shule hiyo ilipojengwa.
“Kabla ya ujenzi tuliwashilikisha wananchi wa eneo hili kwamba sehemu hii haifai kujenga shule maana udongo wake ni chepechepe na unatuamisha maji, tukaomba watubadilishie sehemu nyingine yenye mchanga lakini walikataa, kwahiyo kwa ushauri wa Mhandis wa Halmashauri tukaamua kuanza kujenga hivyohivyo” Sinsungwe.
Mwisho
Attachments
-
WhatsApp Video 2023-09-19 at 10.10.34.mp439.5 MB
-
WhatsApp Image 2023-09-19 at 10.11.07(2).jpeg62.7 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2023-09-19 at 10.11.09(1).jpeg32.7 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2023-09-19 at 10.11.09.jpeg63.6 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2023-09-19 at 10.11.07.jpeg90 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2023-09-19 at 10.11.06.jpeg38.6 KB · Views: 1 -
WhatsApp Image 2023-09-19 at 10.11.10(1).jpeg90.8 KB · Views: 1