Asante ila kabla nijue ni Dengue doctor alikua ananipa matibabu ya Malaria, ndio mshikaji fulani akshauri nicheck Dengue, tatizo vituo vyenye vifaa vya kupima ni vichache, nilizunguka sana, hatimaye nikabahatika kufaulu pale Kisutu kuna kituo cha mhindi kinaitwa Ibrahim Haji centre, hapo ndio nilipatikana na Dengue.
Ngoma ikawa kwamba Dengue haina dawa, yaani kunywa maji mengi meza panadol basi, wiki imeisha napitia mtihani wa kijehanamu, pressure ikashuka noma, ila nimepona lakini hiyo homa hapo hatari halafu imezagaa Dar, kwanza maeneo ya Magomeni.