BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema zoezi la kuwahamisha wakazi hao kwa awamu ya kwanza litahusisha Kaya 23.
“Wananchi tumewaambia hatutagusa majengo yao, watabomoa wenyewe na tumetoa fursa, pamoja na fidia, mali wanazotaka kuzichukua wachukue, watapelekwa hadi Handeni bure.
Video zimeonesha wakazi wanaoishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari yao wenyewe wakianza kufungasha mizigo yao na kuvunja makazi yao ya hifadhini hapo tayari kuelekea Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni Mkoani Tanga.
Wafugaji hao wamesema wameridhia kuondoka katika maeneo hayo kwani wanafidiwa kila kitu ikiwamo kujengewa nyumba na huduma mbalimbali. Wamemshukuru Rais Samia kwa kuwasikiliza na kuwaandalia makazi mapya yaliyo bora yenye Umeme, Maji, Huduma za afya na sehemu ya kufugia mifugo na kulima pia
Wameongeza kuwa fursa hiyo waliyopewa ni bahati na upendeleo kwa wana-Ngorongoro kwani licha ya kupewa nyumba, mashamba na huduma nyingine lakini wamewezeshwa ili kuweza kuendana na kasi ya maendeleo.
“Kuna shule, hospitali nzuri, miundombinu ya maji vikiwepo visima ambapo katika mzunguko wa nyumba kuna ekari 3 mbali na mashamba yenye ekari 5,” amesema Beatrice Soka.