Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Hili eneo mara la barabara limegaiwa visivyohalali mara ZEK Group wamelinunua sasa kama wamelinunua au kumilikiswa na hao jiji sasa inakuwaje wanapewa eneo amabalo ni la barabara.Hapa kuna kitu mbaya ngoja waendelee kutoana jasho na sisi tutaupata ukweli!
 
Eneo walilonunua ZK sio eneo la barabara,ni kiwanja kikubwa tu kilicho nyuma ya RG.

Mfano wewe leo ukawa na kiwanja chako,then mtu aje kufungua baa mbele ya uzio wako.Nina uhakika hutakubali.Hilo eneo kisheria sio lako,ni mali ya mamlaka inayoshugulika na barabara,lakini halina matumizi yeyote zaidi ya barabara,na wewe as mwenye kiwanja unaweza kuliendeleza bila kuweka permanent structure,labda ukapanda maua,au miti nk.

Kwani RG si ilianza kama butani ya maua,walikuwa wanauza maua na baadae kuanza kuuza na pombe pia.

Cha kushangaza ni kwamba huyu mwenye ZK alikuwa ni mteja mkubwa wa RG,sasa sijui walikorofishana wapi hawa
 
Zanaki,
Sasa nimeshaona mbali kabisa kuhusiana na hili sakata.

Ni kweli kwamba ZEK, wapo pale kihalali, na RG ipo mbele yao.
But, ZEK walipata miliki ya kiwanja hicho lini????? Sababu wamejenga pale juzijuzi tu. Wakati RG ilishakuwepo hapo kwa miaka mingi.

Je ZEK walikuwa tayari na hati, toka 90's kweusi wakati RG ilipoanza kuoperate???

Kama ZEK haikupata kibali hiki wakati huo, kwa nini basi aliyekuwepo mwanzo ambaye RG hakupewa kiwanja hicho kwa vigezo vya uzawa na uwepo wake tayari katika eneo husika.

Banandugu, we need to be very careful here. Hii issue inanuka uozo ile mbaya....

Kazi ndiyo kipimo cha utu,
Usitake kabisa kujadili wanahabari wa bongo hapa sababu utaishia ku-upset watu bure. At least hicho ndicho ninachofanya.

Wanahabari wengi bongo hawajui kutafuta habari, mara nyingi wanategemea mwenye issue awape habari ya kuandika, kadiri atakavyo mwenye habari

Bongo, Press conference inamaana ya wanahabari wanakaa kitako kusikiliza walichoitiwa, nothing more nothing less. Hakuna cha maswali wali wala nini, na yakiwepo haya kichwa wala miguu sababu hawana tabia ya kufanya research ya issues zitakazozungumziwa kwenye hiyo mikutano wanayohudhuria.
 
zinduka,maneno ya kweli kabisa,bongo ni fitina juu ya fitina tu.kwa hilo nawapa 100%.waliniacha hoi pale waliposema lile jengo lililoanguka pale changombe halina mwenyewe . kwa kifupi hatuna viongozi.bongo ukijua kuongea tu,mtaji tayari .
 
Jamani kama sikosei huko nyuma imeelezwa kwamba ZEK walinunua kiwanja toka simu ambao ndio walimpa nafasi RG kuweka bistani ya maua na hadi kujenga RG lakini chini ya masharti isiwe nyumba ya kudumu.
Kwa hiyo ZEK waliponunua kuna mkataba kati yao na simu ambao unawapa milki ya eneo hili. RG ni lazima afuate maagizo ya ZEK kwani ndiye mmiliki wa eneo hilo. Matatizo ni pale Magufuli kutoa kibali kwa RG kumiliki sehemu ndani ya hifadhi ya barabara ktk uwanja unaomilikiwa na ZEK.
Hivyo ndivyo nilivyoelewa mimi.
 
Kama ni ZEK kununua au kupewa eneo hilo kutoka kwa SIMU (2000) basi itakuwa kuanzia 2000 na si kabla ya hapo. Hata hivyo RG ilikuwepo kabla ya 2000.

Kingine kinachosemwa mtaani ni kuwa hawa jamaa Zadock na Mlatie (bosi wa RG) walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa sababu moja au nyingine wakakorofishana na hivyo kuanza kutunishiana misuli.

Lakini suala zima linaelekea kuwa ni vita ya vigogo serikalini na madiwani nao wameingizwa tu kwenye mkumbo. Naibu wa Pombe ni Rita. Pombe alimuumbua mwenzake bungeni kuwa kahodhi viwanja, mwenyewe akaviruka. Kumbuka bi mkubwa naye ni diwani wa manispaa ya Kinondoni kwa ubunge wake wa Kawe! Lakini mengi yatatoka nje kadri muda unavyokwenda.

Kitu kingine kinachonikera (hapa ni mahala pa kutolea kero!) ni tabia ya "wawekezaji" kutetea hoja zao kwa madai ya kutengeneza ajira nyingi wakati mara nyingi huishia kutokuwa kweli. Sasa huyo naye anadai atatoa ajira 5,000! Barrick wenyewe kwa uwekezaji wao wa mgodi mmoja mkubwa hapa Tanzania hata idadi hiyo hawana!
 
Kama ni ZEK kununua au kupewa eneo hilo kutoka kwa SIMU (2000) basi itakuwa kuanzia 2000 na si kabla ya hapo. Hata hivyo RG ilikuwepo kabla ya 2000.

Kingine kinachosemwa mtaani ni kuwa hawa jamaa Zadock na Mlatie (bosi wa RG) walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa sababu moja au nyingine wakakorofishana na hivyo kuanza kutunishiana misuli.

Lakini suala zima linaelekea kuwa ni vita ya vigogo serikalini na madiwani nao wameingizwa tu kwenye mkumbo. Naibu wa Pombe ni Rita. Pombe alimuumbua mwenzake bungeni kuwa kahodhi viwanja, mwenyewe akaviruka. Kumbuka bi mkubwa naye ni diwani wa manispaa ya Kinondoni kwa ubunge wake wa Kawe! Lakini mengi yatatoka nje kadri muda unavyokwenda.

Kitu kingine kinachonikera (hapa ni mahala pa kutolea kero!) ni tabia ya "wawekezaji" kutetea hoja zao kwa madai ya kutengeneza ajira nyingi wakati mara nyingi huishia kutokuwa kweli. Sasa huyo naye anadai atatoa ajira 5,000! Barrick wenyewe kwa uwekezaji wao wa mgodi mmoja mkubwa hapa Tanzania hata idadi hiyo hawana!

Mwanagenzi, hawa ni waosha sufuria; wauza mikate, soda, bia n.k. 1000 (5000?) inawezekana.
 
Bandugu hili suala la RG ni ugomvi binafsi kati ya ZK.

Kimsingi kumlaumu Magufuli sio halali, ukweli ni kuwa mwaka 1998 mmiliki wa Rose Garden alikuwa akiuza maua na vinywaji pale pembezoni mwa ukuta wa posta na simu, eneo lote hilo lina viwanja kama vinne vya wazi. Baada ya kuona eneo lipo wazi kina RG waliamua kuandika barua Manispaa ya Kinondoni kuomba ofa pamoja na wale majirani zake wanne. Manispaa ya Kinondoni ilimpa ruhusa ya muda wakati taratibu zikiendelea kwa masahrti kwamba wasijenge BAR bali ni kwa ajili ya maua au makazi.

Mwaka 2004 baada ya ZK kununua eneo la simu2000, ndipo kasheshe lilopoanza ambapo aliyekuwa mkuu wa mkoa Mhe. Makamba alipelekewa malalamiko ya eneo la Rose Garden kutumika kwenye matumizi ambayo hayapo kwenye mipango miji.

Mh Makamba ndipo alipoagiza Manispaa ya Kinondoni wachukue hatua. Mkurugenzi wa Kinondoni akamshauri waziri wa ardhi kupitia kwa kamishna wa ardhi asitoe hati (kumbuka wakati haya yanafanyika waziri pale alikuwa Mh. Gideon Cheyo) baada ya mkurugenzi kumshauri kamishna hatua iliyofuata ni kusimamisha taratibu za kupatia hati watu wanne walio karibu na ukuta wa ZK

Hapo RG wakaenda mahakamani. Baaada ya kesi kunguruma kwa kipindi RG waliachana na kesi na waliomba upya miliki kupitia sasa kamishna wa aridhi. Kamishana alifanya utafiti na kugundua hakuna ubaya kutoa miliki kwa maeneo yale kwa matumizi ya makazi.

Wakati hayo yakiendelea Mkurugenzi wa Kinondoni mwaka 2004 aliandika tena barua kwa Kamishna kumshauri asitishe kusudio la kuondoa watu eneo lile kwa kuwa aligundua wapo kihalali na kama wangewaondoa kwa nguvu ingesababisha serikali kulipa fidia kubwa. Baada ya hapo ndipo Kamishna alipokubali maombi ya hati ya RG na wenzake [viwanja vinne] na kuwamilikisha kwa matumizi ya makazi.

So, mtagundua hapa kisheria kosa la RG ni kufungua bar eneo lisiloruhusiwa kimipango miji, eneo ni lake kihalali. Manispaa kama wangekuwa na akili wangechukua hatua ya kufungia baa na si kumuondoa na RG wakiamua kubadili matumizi ya eneo wakajenga nyumba ya kuishi au office apartments itakuwa sawa.

Mtagundua hapa hoja ya kusema Magufuli ajiuzulu haina nguvu kwa sababu haya mambo yalifanyiaka kipindi cha GIDEON CHEYO hadi hapa yalipo! Nadhani yameibuka sasa kwa sababu za kisiasa tu na hao Manispaa ya Kinondoni si wakarudishe kwanza viwanja vya shule walivyouza kule kawe kama kweli wana uchungu?

Au wakambane yule mwekezaji wa Tanganyika Pakers aliyebadili eneo la kiwanda cha TANGANIKA PACKERS kutaka kujenga apertments wakati lilitengwa kwa viwanda wanabomoa kiwanda wanajenga nyumba za kuishi na mashine za nyama wameziuza.. Tukaajiriwe wapi?
 
Au wakambane yule mwekezaji wa Tanganyika Pakers aliyebadili eneo la kiwanda cha TANGANIKA PACKERS kutaka kujenga apertments wakati lilitengwa kwa viwanda wanabomoa kiwanda wanajenga nyumba za kuishi na mashine za nyama wameziuza.. Tukaajiriwe wapi?

Wataweza kumuuliza aliyekuwa Waziri wa Nyama wakati ule?? Si unajua sisi Wamasai tunavyopenda nyama!!
 
Wanabodi,
labda nikurudisheni nyuma kutazama kilichosemwa kabla hatujaendelea zaidi. Rudieni kosma ukurasa wa sita mengi yamezungumzwa kiasi kwamba nashindwa kabisa kumtetea Magufuli.
Kuna kipande hiki kinachotangulia yote:-
Kulingana na mlolongo wa nyaraka zilizoko, mmiliki wa baa ya Rose Garden, Damas Assey, aliomba kibali kutoka Kampuni ya Simu Tanzania, ofisi ya Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam Kaskazini, kutumia eneo iliko baa hiyo mwaka 1995. Ofisi hiyo kwa barua ya Novemba 2, 1995 ilimruhusu Assey kuendesha shughuli kwenye eneo hilo likiwa ni mbele ya viwanja namba 717/5 na 717/4 ambako kiwanda cha uchapaji cha TTCL kilikuwako wakati huo, lakini ikamkataza kujenga jengo la kudumu. Wakati huo alikuwa akifanya biashara ya kuuza maua.
Sasa hadi hapa tunaelewa kuwa ni kampouni ya simu iliyompa kibali cha kuuza maua na hata kufikia kujenga RG. Kisha tunaelewa kuwa simu 2000 ltd ndio waliokuwa na jukumu la kuuza sehemu hiyo na kulingana na report waliwauzia ZEK.

Kisha kuna kipande kingine kinasema:-
Hata hivyo, baada ya Simu 2000 Ltd kutaka kuuza eneo hilo na kuiomba Manispaa ya Kinondoni kuondoa vibanda vyote vilivyokuwa mbele ya viwanja hivyo kwa sababu wawekezaji walikuwa wakisita kuvinunua, Assey alifungua kesi mahakamani kuzuia kuvunjwa kwa baa hiyo.
.

Wawekeshaji walisita kuvinunua! Mhhhn Je, ZEK walinunua viwanja hivyo hali wakijua kuna utata wa kesi ya Assey mahakamani?...if yes why did they?

Mmoja wa watu ambao wamejikuta wakiathirika na uamuzi wa Magufuli wa kubariki viwanja namba 948 hadi 951, ni Kampuni ya ZEK Group ambayo ilinunua viwanja namba 717/5 na 717/4 kutoka Simu 2000 Ltd kwa ajili ya kuwekeza mradi mkubwa wa mabilioni ya shilingi. Akizungumzia suala hilo jana, Mwenyekiti Mtendaji wa ZEK Group, Zadock Koola, alisema pamoja na kumweleza Waziri Magufuli juu ya mkanganyiko uliokuwako juu ya kubuniwa kwa viwanja hivyo, ameamua kuvitambua bila hata kujibu barua waliyomwandikia mwaka jana, wakimuomba kuingilia kati mgogoro huo.
.

Hukumu yenu waungwana!.. kesi ubaoni.
 
Mkandara,
This makes it hard. My emotion was with the Minister, but if these are the facts then my head says justice must be done.
 
Zinduka!
sikutaka kujadili waandishi wa habari hapa bali nimesema wanatuopotosha kwani nafasi ya kumuuliza magufuli walikuwa nayo kulikoni waache halafu waje kuandika vitu vya upande mwengine yaani Halmashauri na wengine vya Magufuli.Kuhusu swala la kwamba waliitwa tu na hawakupewa nafasi ya maswali halina ukweli kwani tuliona hata kwenye picha Magufuli akijibu maswali yao swala la msingi ni kwamba maswali aliyoulizwa hayakulingana na vingezo ambavyo tayari walikuwa navyo kama FACT ya swala zima, kwanini wasiulize na haya ambayo wametuandikia hapa na kuacha maswali mengi kwetu wasomaji kuliko majibu.Wakati haya maswali wangeweza kumuuliza Magufuli na tukapata majibu na kama walikuwa na uhakika na walichokiandika wangemueleza magufuli ni wapi amepotosha umma wa Watanzania.Hii inatuweka katika hali ngumu ya kufikiri sisi ambao ni third part ya kupokea habari.
 
Mkandara!

Bado kuna ugumu wa kutoa hukumu kwa hili swala mpaka ukweli wote utakapokuwa wazi.Kumbuka wewe umechukua Habari iliyokuwa inamueleza magufuli tu na ilitoka kwenye gazeti la mwananchi Lakini Habari ambazo zilitoka kwenye magazeti mengine ambazo Magufuli alijibu maswali alisema kwanini yeye hauhusiki na akatoa mpaka changa moto kwa MADIWANI Kwamba kibali kilitolewa na kamishina ya Ardhi na huyo RG anamiliki kihalali hiyo sehemu sasa kama Halmashauri wanaitaka hiyo sehemu wapatane na mmiliki.

Hapa palikuwa na swali ambalo walistahili kuuliza kibali kilitolewa lini?

Lakini hao waandishi ambao walikuja baadae wakaeleza FACTS Zingine baada ya Press Conference yao na waziri kwanini hawakutumia hizo FACTS kama walivyotuandikia tukasoma kuzijengea maswali na kumuuliza Magufuli?Sasa wanapotuandikia wasomaji na wakati nafasi ya kuuliza na kujibiwa na Mhusika ilikuwepo wanataka sisi tuelewe vipi?Halafu si waandishi wote waliondika habari sawa bali waliowengi walioandika yale magufuli aliyosema kujibu hoja husika na maswali aliyoulizwa kutokana na hoja hizo.

Ni mwananchi pekee ndiyo aliandika tofauti na wengine, Lakini katika huo utofauti hakuna sehemu waliyosema mwaandishi alimuuliza maswali Magufuli na Majibu yake yalikuwa ya aina gani kutokana na hicho walichokiandika. Sasa siwezi kumuhukumu mtu kwa ushahidi wa upande mmoja kwani upande wa pili nao unahaki wa kujibu hoja zilizoelekezwa kwake na hi ni katika hali ya kuwapa MAJAJI (amabo ni JF KAMA ULIVYOOMBA) Kuamua yupi mkweli.

Hadi hapo tutakapopata habari za ziada kuhusu hili swala ndiyo tutaweza kufiKia hukumu isiyo tata.Natumaini hao waandishi watamfuata tena magufuli na wajenge maswali yao kwa hizo facts zao walizotuwekea hapo halafu KUTOKANA NA MAJIBU YA MAGUFULI tutapata muelekeo mwengine.

Au kama kuna mtu anafanya kazi ofisi ya kamishina wa ardhi na analielewa hili swala atupatie ufafanuzi wakina kwa kuliweka hapa ili tuchambue mbivu na mbichi.
 
Kazi ndio kipimo cha Utu,

Nimesoma baadhi ya madai ya Magufuli ambayo mwanzoni niliyaamini kwa sababu hapakuwepo na ukweli huu toka upande wa pili.

Magufuli alidai kuwa Assey yaani mwenye RG alikuwepo katika maeneo hayo toka zamani na hata yeye Magufuli alimkuta tayari akiwa pale...Jibu lake tumelipata kuwa RG walipewa nafasi na simu kwa masharti ya kutojenga nyumba ya kudumu. Ilikuwa hisani ya simu ama makubaliano nje ya taratibu na sheria za uuzaji kiwanja.

Kisha kabla na baada ya sehemu hiyo kuuzwa na simu 2000, RG na wengine wote waliaombwa kuondoa vibanda vyao kwa sababu eneo hilo linauzwa... RG hakukubali (hapo kakiuka mkataba) nakala ya barua imetolewa hapa...

Mwisho tunaona kuwa RG alipinda na kupewa kibali, hali Magufuli huyu huyu miaka yake alivunja vibanda kibao kwa sababu vilikuwa ktk maeneo ya hifadhi ya barabara. Leo ilipofikia swala la RG kasema mbona kuna vibanda kibao sehemu nyingi Kinondoni ambazo ni hifadhi za barabara na bado viko..kama vile anauliza what is so special?

Well, mimi namuuliza yeye!... Ulipokuwa ukivunja vibanda vya watu sehemu nyingine hukuviona hivyo vya Kinondoni!.. Kulikoni?

Na kama uliviacha wewe chini ya usimamizi wako why question watu waliofuata kabla ikiwa wewe hujatueleza sababu zilizokufanya usivivunje vibanda hivyo wakati ukitekeleza mkakati wako wa upanuzi wa mabarabara?...

Beside guys, huyu mwenye ZEK kasema waliandika barua kwa Magufuli kuomba aingilie swala hili lakini bado kibali kilitolewa mwaka baada ya bila hukumu ama majibu kwao.. Na kikubwa zaidi mmiliki wa kiwanja hicho ni ZEK ambaye alikinunua kihalali toka simu. RG ni sehemu ndani ya mkataba wa simu na ZEK..ZEK wana kila haki ya kuchagua kitu gani kiwepo pale.

Mwisho, haiwezekani hata kidogo ktk eneo lile kibali cha kiwanja kitoke baada ya 2000.. eneo hilo ni hot cake, hiki kibali lazima kiwe cha kughushi ama ukiukaji wa sheria fulani kuwazima ZEK ambao wamenunua eneo hilo kihalali na sijui wamekipanua vipi nje ya hifadhi hadi kubadilisha mawe ya zamani, Bandugu haiwezekani kupata kibali cha haki kujenga ktk eneo ambalo ni hifadhi ya barabara. Hata kama kibali kilitolewa na waziri wa ardhi, kwani wizara hiyo haiwezi kufanya kosa?

Wakubali makosa na irekebishwe ila tu kama RG itavunjwa basi maeneo yote ya hifadhi ya barabara za Kinondoni zivunjwe kwa kufuata plan ambayo tayari imekwisha pitishwa na serikali na fedha zimekwisha tengwa ktk upanuzi wa maeneo hayo...Zisiwe hadithi tupu kwani na sisi waswahili kwa kikorosho hatujambo!
 
Wanabodi,

Kama eneo la RG liko ndani ya hifadhi ya barabara itakuwaje ZEK adai ni lake? Ina maana SIMU (2000) walimuuzia na hifadhi ya barabara?
 
Mwanagenzi,

Ukitazama viwanja vyote kuna nafasi kati ya barabara na nyumba tukiacha hizo nyumba za Harlem (Kariakoo). Hiyo nafasi wengi hutumia kama bustani na upo uwezekano ikaingiliana na hifadhi ya barabara ikiwa ramani na sehemu hiyo ina mpango wa muda mrefu kupanuliwa.
Sasa hata kama iwe chini ya manispaa bado picha nzima inatuonyesha kuwa RG aliomba kibali toka simu na sio wizara ya ardhi ama manispaa. Tumeona haya ktk ujenzi mbalimbali ambapo mwenye duka huwaruhusu wenye maduka ya dharura - container wakiweka mbele ya nyumba zao.

Hapa kinachonipa taabu ni kwamba, Madiwani kusema kweli ni wawakilishi wa wananchi, na tunapowapiga vita inaonyesha wazi kwamba mfumo wa serikali kuu kuchukua madaraka kutangulia wawakilishi wetu ndio unakubalika, hali mimi nafikiria Manispaa inatakiwa kuwa mbele ya wizara ktk maendeleo ya sehemu husika.

Na hii ni moja ya hatari kubwa tunapofikiria hata mipango ya majimbo ama kuwapa madaraka wajumbe waliochaguliwa kushika uongozi. Haiwezekani kabisa wizara kutoa maamuzi wakitengua yale ya wilaya na kata bila mawasialiano ama makubaliano ya kimsingi kati yao.

Na hapo hapo sote tunaelewa jinsi wizara yetu ya ardhi inavyoboronga wakitoa vibali viwili kwa kiwanja kimoja kiasi kwamba ufumbuzi wake ni mgumu sana hata kortini imekuwa ngoma.
Niliwahi kuwa na kiwanja Mikocheni ambacho Mshikaji Freeman alikinunua miaka hiyo ya 1980's, mara ikaja onekana kuna watu kama watatu hivi wenye kiwanja kicho hicho pamoja na kwamba niliwatangulia na hizo hati zao zilikuwa za mazabe. Naambiwa Freeman alinyang'anywa kiwanja hicho hali kila record za serikali zinaonyesha mmiliki halali ni nani.

Tanzania mshikaji hakuna sheria mwenye nacho ama address ndiye mmiliki halali hata kama umetangulia.

waswahili wanasema Kutangulia sio kufika! siku hizi wameongezea - wala Kufika sio Kupata!... what counts ni yule aliyepata.
 
However, Magufuli told journalists yesterday that the owner of Rose Garden had not trespassed because he was authorized by the Commissioner for L lands to occupy the area. The councilors claim that Rose Garden, a famous bar in Kijitonyama suburb, has been built on a road reserve and want it pulled down. Magufuli said if the Kinondoni Municipal authority wants to demolish the structures, it will have to compensate the owner since he followed all the laid down procedures to secure the plot.
Need I say more? Mwenye shida aende mahakamani na hapo ndio tutafahamu nani mkweli na uongo utajitenga. Authority imetoka kwa Commissioner for Lands.
 
Mkandara,
Hili swala bado ni tata. huu unaouita ukweli na hata magufuli wake anauona ni ukweli,sasa kinachonistajabisha mimi hawa mwananchi kwanini hawakuraise hilo kwenye kikao cha wanahabari na magufuli wakati walikuwa na nafasi hiyo?Hapo ndiyo panaponipa mashaka mimi. Unajua kuna ka mchezo Bongo inapotokea swala la mfutano kama hili baadhi ya wahusika wanawanunua waandishi na hata baadhi ya vyombo vya habari kuwakilisha yale wanayoyataka na hiki kinanipa wasiwasi mimi ya kudemand maelezo zaidi kabla sijafikia maamuzi juu ya swala hili.Nafikiri kama kuna anayeona amekosa haki kuna mhimili unaoshughulika na hilo,Huko tutayasikia yote yaliyofichika kwa hivi sasa.
 
Meya Kinondoni azidi kusuguana na Magufuli

2007-02-23 09:20:54
Na Simon Mhina


Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mstahiki Salum Londa, amesisitiza kwamba uamuzi wa Baraza la Madiwani kuhusu kubomoa mgahawa maarufu wa Rose Garden upo palepale.

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Bw. Londa alisema binafsi anamheshimu sana Waziri John Magufuli.

Hata hivyo, alisisitiza kwamba kama ambavyo yeye (Waziri) yupo kwa mujibu wa sheria, pia kikao cha madiwani kilichobatilisha umiliki huo, nacho kimewekwa kwa mujibu wa sheria.

`Unajua Sheria ya Ardhi imetungwa na Bunge ninachotaka kukisema hapa jamani, tufanye kazi zetu kwa mujibu wa sheria... Utawala bora maana yake ni kila mtu afuate sheria, kwa hiyo msimamo wetu upo pale,` alisema Bw. Londa.

Meya huyo alisema hataki kuingia kwa undani juu ya sakata hilo, wala kulitolea maamuzi binafsi kwa vile uamuzi wa awali, haukuwa wa kwake binafsi kama Londa, bali ni uamuzi wa Baraza la Madiwani.

Jana Waziri Magufuli alikaririwa na vyombo vya habari akinukuu vifungu kadhaa vya Sheria ya Ardhi, vinavyompa mamlaka ya kubadili matumizi ya ardhi husika.

`Wizara ya ardhi ndiyo inayosimamia masuala ya ardhi nchi nzima, na sheria zilizopo zinampa waziri mamlaka kubadilisha matumizi ya ardhi hata kama ni ya maeneo ya wazi, na mimi kama waziri nikaamua nibadilishe matumizi ya ardhi ile,` alisema Waziri Magufuli alipozungumza na waandishi juzi.

Alikaririwa akiwataka madiwani hao, kuacha mpango wa kubomoa mgahawa huo, vinginevyo wanaweza kujikuta wakimlipa fidia kwa uharibifu wowote, kwa vile anamiliki eneo hilo kwa mujibu wa sheria. Magufuli alisema atakuwa shahidi wa mmiliki wa mgahawa huo kama atalifikisha sakata hilo mahakamani.

Hata hivyo, Bw. Londa alisisitiza kwamba anavyojua yeye, hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria, anayeweza kujiamulia mambo kwa matakwa yake binafsi.

`Magufuli ni waziri, mimi ni meya. Ukitulinganisha ni sawa na bahari na mto, yeye mwenzangu ni bahari mimi ni mto. Mto unaweza kukauka lakini bahari ikaendelea kuwepo, lakini ni lazima niseme kwamba tufuate utawala wa sheria kwa vile japo mito inaonekana midogo na maji machache, lakini ndiyo inayojaza bahari,` alisema.

Alisema madiwani watakutana kujadili kauli ya waziri, lakini akasisitiza kwamba msimamo wa Manispaa haujatenguliwa.

Mapema mwezi uliopita, madiwani wa Manispaa ya Kinondoni, chini ya Meya Londa, walitoa tamko la kutaka mgahawa wa Rose Garden ubomolewe kwa vile hauko kwenye eneo la biashara wala makazi, bali kwenye hifadhi ya barabara.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom