Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Kazi ndio kipimo cha Utu,

Magufuli sasa anazungumza nje ya sheria kabisa kuwa mtu akipewa kibali kujenga katikati ya barabara basi imetoka na ndio maana hawa hawa waliuza hata bustani ya mnazi mmoja. Kitu muhimu hapa sio authority to occupy land toka kwa Commissioner ambaye katoa hata uamuzi wa kugeuza mipaka ya mawe kutoa nafasi ambayo bado kesi yake ilikuwa ikifuatiliwa. Kukubali mpango wa vibali ni sawa na kukubali mikataba feki kwa sababu tu kuna vibali. hao akina Sinclair, Richond, IPTL n.k.

Wote wanapinga mikabata hii huonekana hawana tofauti na hawa madiwani kwani hatupendi kumwangusha mtu fulani kwa sababu zetu binafsi.

Magufuli hazungumzi kabisa kuhusu madai ya ZEK kuomba kibali kisitolewe! hazungumzii kabisa uamuzi wa uliotangulia kibali hicho kuhusu kiwanja hicho ila anang'ang'ania kibali ambacho TZ kinatoka kwa njia ya simu tu toka juu.

Magufuli mfanyakazi hodari lakini bob ana kitu UUNGU ktk uongozi wake. Anapenda sana kushindana ktk maswala ambayo hayana hata sababu ya ushindani.

Nakumbuka sii miaka aliwakatalia jamaa kusafirisha boti zao kwenda Mwanza ati zitaharibu barabara zetu hali jamaa wale walikuwa na kibali, watu wakashangilia sana lakini jamaa akatumia njia ya Kenya na boti zikatinga Mwanza leo zinafanya kazi na hakuna barabara ya Kenya iliyoharibika. Kichekesho ni kwamba barabara hiyo leo hii ni mbaya na mbovu kuliko barabara kuu zote za Tanzania.

He is wrong on this bob!
 
Kazi ndio kipimo cha Utu,


Nakumbuka sii miaka aliwakatalia jamaa kusafirisha boti zao kwenda Mwanza ati zitaharibu barabara zetu hali jamaa wale walikuwa na kibali, watu wakashangilia sana lakini jamaa akatumia njia ya Kenya na boti zikatinga Mwanza leo zinafanya kazi na hakuna barabara ya Kenya iliyoharibika. Kichekesho ni kwamba barabara hiyo leo hii ni mbaya na mbovu kuliko barabara kuu zote za Tanzania.

He is wrong on this bob!

Kwa taarifa tu mbona boti zilichemsha hata miezi miwili haikupita? Mara zizimike ziwani, mara moshi kibao...mwishowe jamaa wa SUMATRA wakazipiga top kwamba mpaka zitengenezwe. Wadosi wakasema wataleta mafundi toka Sauzi, mpaka jana kama si leo ikawa hadithi ya alfu lela u lela!
 
Mimi bado simhukumu kwani sijapata udhibitisho juu ya hilo naona watu wanaandika tu akiwa hayupo akiwepo hawaulizi.Nafikiri meya amekuja na point nzuri tu ya uamuzi wa halmashauri kwamba upo pale pale na watabomoa hilo ndiyo ninalitaka mimi lifanyike na sitisha toto,wakifanya hilo nitajua Kuna ukweli wa hoja zao!
 
magufuli anakwambia yeye kama waziri ana protection ya kubadilisha cheti chochote "kama waziri", mhm, here he goes ! sasa now we know inakuwaje akina richmonduli wanapata ulaji eehh, je huyo pm si ndio atatumia mamlaka yake yoooote ahakikishe anakula ulaji ! mheshimiwa magufuli angalia unachosema, utatoa siri zako bure bila ya kukusudia mwenyewe, duh halafu huyu braza 'gufuli nasikia aliwafukuza wafanyakazi wa wizara yake kwa tuhuma kwamba wanatoa siri za wizara yake juu ya RG !!
 
Magufuli awekwa kikaangoni tena
na Mwandishi Wetu

MGOGORO wa kiwanja ilipojengwa baa maarufu ya Rose Garden jijini Dar es Salaam, umeanza kubadilika na kuchukua sura inayoonyesha jitihada za baadhi ya wakubwa serikalini kuutumia kumkaanga Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli.

Mpango huo ambao tayari unaonekana kuanza kuiva umemfanya waziri huyo kujiandaa kukabiliana na kile ambacho watu wake wa karibu wanakielezea kuwa ni mashambulizi ya wazi wazi dhidi ya mwanasiasa huyo aliyepata umaarufu mkubwa enzi za Serikali ya Awamu ya Tatu. Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Manispaa ya Kinondoni vimeieleza Tanzania Daima kwamba, Magufuli anawekwa katika wakati mgumu kwa sababu ya uamuzi wake wa kumlinda mmiliki wa baa hiyo.

Wakati tayari Manispaa ya Kinondoni inalitaja eneo hilo la Rose Garden kuwa la hifadhi ya barabara, Wizara ya Ardhi inaliona vinginevyo. Kauli aliyoitoa Magufuli mwanzoni mwa wiki hii, wakati akizungumza na waandishi wa habari akimtetea mmiliki wa baa hiyo, akisema ana hati halali iliyotolewa na Kamishna wa Ardhi, tayari imepokewa kwa hisia tofauti na watu mbalimbali walio na masilahi yanayokinzana juu ya umiliki wa kiwanja hicho.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima unaonyesha kuwa, Magufuli alitoa kauli hiyo akitumia kumbukumbu zilizopo wizarani hapo ambazo zinaonyesha kuwa kiwanja hicho hakipo katika hifadhi ya barabara. Dokezo linalohusu eneo hilo ilipo Rose Garden lililosainiwa na Kamishna wa Ardhi, Albert Msangi, ambalo Tanzania Daima imepata nakala yake linaonyesha kuwa barabara inayopita hapo iko katika kundi la Barabara za Mikoa (Primary Distributor Road) na si Barabara Kuu za Kitaifa.

Kwa mujibu wa dokezo hilo, ambalo linazingatia Mpango Kabambe wa Jiji la Dar es Salaam wa mwaka 1979, upana wa barabara za mikoa unapaswa kuwa wa kati ya mita 30 hadi 40 na ‘carriage’ ya kati ya mita saba hadi 10, viwango ambavyo vinakidhiwa na Rose Garden, na hivyo kuifanya kuwa nje ya eneo la hifadhi ya barabara.

“Kulingana na viwango hivyo, upana wa barabara ambayo upo sambamba na ‘Rose Garden’, inayounga Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Barabara ya Mikocheni, unatakiwa kuwa kati ya mita 30 hadi mita 40 kwa kuwa ni ‘Primary Distributor Road’. “…Kwa mantiki hiyo, upana wa barabara iliyopo kwenye eneo hilo la Rose Garden unakidhi viwango hivyo vya mita 30 kwa ‘carriage way’, inatakiwa iwe kati ya mita saba hadi 10, kwa maelezo hayo eneo la Rose Garden halipo katika ‘road reserve’ kama inavyodhaniwa (angalia kiambatanisho kinachoonyesha upana wa barabara kulingana na G.N 157 ya mwaka 1997 ), eneo husika limegawiwa kwa matumizi ya cafes and restaurants,” linasema dokezo hilo.

Mbali ya dokezo hilo, Tanzania Daima pia imebaini kuwapo kwa mawasiliano ya barua kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Waziri Magufuli kuhusu suala hilo la Rose Garden. Moja ya barua ambayo gazeti hili limeiona, imeandikwa na Waziri Magufuli kwenda kwa waziri mkuu ikitoa ufafanuzi wa uhalali wa umiliki wa kiwanja hicho. Barua hiyo ya Agosti 14, 2006, yenye kumbukumbu namba LD 247419 iliyosainiwa na Magufuli mwenyewe, inasisitiza kuwa eneo hilo limegawiwa kwa matumizi ya migahawa.

Sehemu ya barua hiyo ambayo ni majibu ya barua aliyoandikiwa Magufuli na Katibu wa Waziri Mkuu, B. Olekuyan, ya Agosti 4, 2006, yenye kumbukumbu namba PM/P/1/567/38, inasomeka: “Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa mujibu wa sheria Na. 167 ya mwaka 1967 inayohusu hifadhi ya barabara, tangazo la serikali G.N 157 la mwaka 1997 likisomwa kwa pamoja na kifungu cha 78 cha sheria ya mipango miji na vijiji.

“…..Sura 378 (The Town and Country Planning (Town Planning Space Standards) Regulation, 1997) na kwa kuzingatia mchoro wa mipango miji na. 1/518/369 wa eneo la Mikocheni ilipo barabara ambayo iko sambamba na Rose Garden inayoungana na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi. “…..Inaonyesha eneo la Rose Garden halipo katika hifadhi ya barabara (Road Reserve) kama ilivyodhaniwa. Hali kadhalika, eneo hilo limegawiwa kwa matumizi ya cafes and restaurants.”

Barua hii inadhihirisha kuwa msimamo wa Waziri Magufuli kuhusu mgogoro wa Rose Garden hauwezi kubadilika, na kwa sababu mmiliki wake analindwa na sheria ambazo Magufuli alizitumia kujibu barua aliyoandikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Katika kuthibitisha kuwa Magufuli amekwishatambua mpango wa watu wanaotaka kummaliza kwa kutumia sakata la mgogoro wa umiliki wa kiwanja cha Rose Garden, hivi karibuni, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake alisema haogopi matokea ya uamuzi wake.

Magufuli, ambaye mara kadhaa amekumbana na misukosuko, ikiwamo kuokotwa bunduki nyumbani kwake, anaonekana kuzidi kuandamwa baada ya hivi karubini kuzushiwa kuwa amefariki dunia akiwa nchini Ujerumani ambako alikuwa akitibiwa.
 
KadaMpinzani
Maneno ya waziri Magufuli ni haya hapa:

`Namshangaa mmliki wa mgahawa wa Rose Garden kwa kutowashtaki mahakamani watu wanaomkwaza kufanya kazi zake? Hata akienda mahakamani, mimi na Kamishna wa Ardhi ni mashahidi wake,`alisisitiza.

Pia Waziri Magufuli alisema ni Wizara pekee iliyopewa mamlaka kisheria ya kuidhinisha matumizi ya ardhi nchini kote.

`Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999, inampa Waziri wa Ardhi mamlaka ya kuidhinisha au kubadili matumizi ya ardhi katika vijiji na miji yote nchini, hivyo hata kama ningefanya hivyo, bado ningefanya kwa mujibu wa sheria hiyo,` alisema.

sasa angalia wewe unavyosema

magufuli anakwambia yeye kama waziri ana protection ya kubadilisha cheti chochote "kama waziri", mhm, here he goes ! sasa now we know inakuwaje akina richmonduli wanapata ulaji eehh, je huyo pm si ndio atatumia mamlaka yake yoooote ahakikishe anakula ulaji ! mheshimiwa magufuli angalia unachosema, utatoa siri zako bure bila ya kukusudia mwenyewe, duh halafu huyu braza 'gufuli nasikia aliwafukuza wafanyakazi wa wizara yake kwa tuhuma kwamba wanatoa siri za wizara yake juu ya RG !!

Vipi unausongo na Magufuli?
 
hivi ritta MLAKI na magufuli wanaonbea lugha moja?imekuwaje kasheshe na kuzusha kuanzie kinondoni ambako huyo mrembo pia ni diwani? ameshindwa nini kumtetea bosi wake hukohuko [you know collective decision],kabla mambo hayajaenda press..tena hata kama alishindwa kutetea kwa nini hakuomba waijadili hiyo hoja mara bosi wake atakapotoka hosipitali?

kuna walakini kama kweli hawa ,wanaongea lugha moja!
 
Mimi toka awali nimejua Magufuli si mwendawazimu asimamie kitu ambacho anaona kitamtia matatani katika kipindi hiki kigumu kwake cha kuwa ndani ya team ambayo inamuona ni Adui,Kitendo cha Muandishi wa mwananchi kuwepo kwenye Press Conference Ambayo alikuwa na uhuru wa kumuuliza swali lolote na hakufanya hivyo na kuja kuandika nakala kuonyesha Magufuli alitoa kibali bila hata ya kutaja kibali kilitolewa lini? Hili nalo lilinitia mashaka kushiindwa kumhukumu Magufuli,pili kitendo cha mwandishi huyo kutofautina na waandishi wa magazeti matatu tofauti yaliyonukuu majibu ya magufuli nacho kiliniongezea wasiwasi. Hata sijafikia tamati nasubiri Habari zaidi Kabla sijafikia uamuzi juu ya swala hili.Tusubiri Habari zaidi zitajitokeza!
 
hivi ritta MLAKI na magufuli wanaonbea lugha moja?imekuwaje kasheshe na kuzusha kuanzie kinondoni ambako huyo mrembo pia ni diwani? ameshindwa nini kumtetea bosi wake hukohuko [you know collective decision],kabla mambo hayajaenda press..tena hata kama alishindwa kutetea kwa nini hakuomba waijadili hiyo hoja mara bosi wake atakapotoka hosipitali?

kuna walakini kama kweli hawa ,wanaongea lugha moja!

Hawa hawaongei Lugha moja kwani katika viwanja ambavyo vimewekwa katika Orodha ya kumilikishwa upya katika jimbo la Mlaki kwa kushindwa kuviendeleza na yeye Mlaki ana vyake na Bossi Amelala navyo mbele na vitapewa wamiliki wapya.
 
Nasubiri KadaMpinzani afafanue maneno yake hapo juu.
 
KadaMpinzani,
Usikubali kutishika, yakhe! Under surveillance, so what?
Tuendelee kukata issues.
 
Nani anatoa vitisho? Hakuna vitisho hapa, sema hao wanaokutisha ni kina nani?
 
KadaMpinzani

Asikutishe mtu hapa JF ni kumwaga mavitus tu, endelea kushusha mavitus
 
asanteni na shukrani kwa kunipa moyo ! now i feel am free at last ! sasa chizi kakabiziwa rungu !!
 
Nipende kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya humu JF na pia nipende kuwapa pole wale wote ambao kwa njia moja ama nyingine wamekuwa wakitishiwa kwa kuweka ukweli hadharani.

pili ni lazima huyu magufuli aonyeshe njia za uwajibikaji pale anapojikuta kuwa amechemsha na hilo alionyeshe kwa vitendo ili basi aweze kuendelea kujiwekea sifa alizowahi kupewa na wakubwa wenzake na hata kupewa ulinzi ,ila pia LONDA na madiwani wake hawana budi pia kujiuzulu na haswa meya londa mwenyewe kwani nafikiri mliweza kulifuatilia sakata la shule ya sekondari kawe kwa kiwanja cha walalahoi kuuzwa kwa MWEKEZAJI so to say?eti alikuwa na lengo la kuendeleza kiasi kwamba hadi muda huu wa leo hakuna hata sehemu ya kujenga majengo ya kidato cha tatu na nne eneo hilo .

hapa hakuna aliyejitokeza kumtaka londa ajiuzulu ama hawa madiwani hawakupewa chochote kwenye mgawo wa rose gadern?

niwatake waungwana waweze kuliangalia pia na hili kwa undani ama ndio mbio za 2015 ndio zimeanza kwa kasi hiyo kwani wale wale waliommaliza DRSalim na wenzake bado wangali wapo hai na wanamalengo ambayo bado hawajayafikia .

kumbukeni kisa cha Sundi mwalomo kupewa nyumba ubungo na hilo likawa ni sakata kwa magufuli peke yake na sio kwa wale wote walioshiriki kuhakikisha kuwa nyumba hizo zinauzwa hata kama ni kwa bei ya kutupwa.

tuangalie pande zote za shililngi.
 
Huyu Magufuli ni mtoto yatima katika familia ya JK. Ni ubishi na kukosa ujasiri kinachomfanya abaki katika serikali ya JK na CCM. Ingekuwa katika nchi zingine kama Kenya, Senegal, Ghana, n.k., huyu mtu angekwisha kujiunga na CHADEMA tangu Julai 2006. Zile makala kwenye gazeti la Rai zilitosha kumuonesha jinsi asivyotakiwa. Katika CCM kuchapa kazi na kusisimamia sheria kama zilivyo ni tatizo. Kwa CCM sheria na taratibu ni kwa walala hoi tu, kitu ambacho Magufuli haelewi. JK alimpa uwaziri kwa sababu za kisiasa, kwani jamii isingemuelewa. Kinachofanyika sasa ni kujaribu kumtoa Magufuli katika nyoa za watanzania ili watakamtema akose wa kumtetea. Na tayari Magufuli polepole ameshaanza kutoka katika nyoa za Watanzania kama tunavyoona humu katika forum. Sasa kwa kukosa ujasiri atasubiri hadi wamtose na aishe kisiasa. Wakimhurumia sana watamuacha hadi kura za maoni za 2010, na hapo inafanyika namna ashindwe. Ndipo atakapoanza kupaparika na kukimbilia katika vyama vya upinzani kama alivyofanya Njelu, but it will be too late, na ataonekana hakubali kushindwa. Katika kundi hili yumo pia Mwandosya. Namhurumia sana Magufuli, maana nathamini utendaji kazi wake.
 
Back
Top Bottom