Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

magufuli aweza kuwa na lengo zuri kwenye hiyo bomoa bomoa yake, lakini ufatiliaji na uthibiti wa kile anachokiboa ndio kina utata

ikithibitika kwamba amelitia taifa hasara ya bilioni 15 (serikali ikikaa rufaa na kushindwa) basi hana buni bali kuwajibika kwa kujiuzulu na kutokuwa waziri tena maishani mwake.

kwa vile tunazungumza kuhusu tanzania hapa, serikali inaweza kulipia pesa hizo na magufuli akaendeleze libeneke ya bomoa bomoa kama kawaida.

hakuna kisichowezekana Tanzania
 
kama sikosei ubomoaji wa ile stesheni ulifanywa chini ya ulinzi wa polisi, nahisi hapa kulikuwa na something behind the scene, inawezekana issue yake ikawa inafanana na unga wa Bakhresa uliochomwa na serikali.
am sure tunaweza pia tusipate feedback ya kitakachoendelea tena.
na kujiuzuru magufuli? labda JK amtose, la sivyo huu si utamaduni wetu.
 
Hakuna uwajibikaji ktk serikali ya Tanzania ya sasa.

huo ni msamiati ambao inabidi twende Ngurdoto kuufanyia semina ili ieleweke!
 
Kwanini ajiuzuru? Eti kwa kuwa ameshindwa kesi ya Mahakama hizi hizi ambazo kila siku humu tunazilalamikia!! Magufuli si mkurupukaji na hasa kwenye issue iliyokuwa moto kama hii naamini kuna something wrong somewhere. Hizi ndo sehemu ambazo wajanja wa CCM wanazitumia kutuibia pesa.
 
Hivi nani atailazimisha serikali kulipa kama haitaki kulipa licha ya hukumu zote mahakamani?
 
Sidhani kama magufuli anatakiwa kujiuzulu maana ni mmoja wa viongozi makini angalau saa nyingine hutokea anafanya makosa just like bin wa adamu yoyote yule ! so in my opinion, he's OK !
 
Naikumbuka sana hii kashehshe pale Mwanza....................kwa kifupi kama kuna mahali MAGUFULI ALIBOA basi na pale mwanza.................yes alikuwa na kila sababu ya kutaka kile kituo kivunjwe..................and yes akiwa na ushawishi mkubwa kwa Rais wakati huo alikuwa na uwezo wa kufuata taratibu za ku-revoke kile kiwanja (niliambiwa hakufanya hivyo)......akidai huwezi kushindana na serikali......................pale mwanza kulikuwa na seke seke patashika nguo chanika.................na hata ilibidi Injinia mmoja aondolewe kwa sababu ya Magufuli...............well wakati huo akiwa kwenye chat nani angezuia maamuzi yake!!

Ohhh no..........now we are paying for somebody's nonsense
 
Hivi hawa jamaa (Magufuli and his associates)mpaka wanafikia uamuzi wa kuvunja hicho kituo hawakuwa na washauri??? Ina maana hawakujua hili linaweza kutokea???

Hivi huyo chenge ni mwanasheria kweli???
 
na Agnes Yamo, Bagamoyo

WENYEVITI wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya wametakiwa kuchukua maamuzi magumu katika kutafuta suluhu ya migogoro ya ardhi.

Mbali ya hilo wenyeviti wa mabaraza hayo wametakiwa kufanya maamuzi hayo kwa haki na pasipo kuiogopa wala kuipendelea serikali.

Wito huo wa kwanza wa aina yake, ulitolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wenyeviti wa mabaraza hayo kutoka wilaya zote za Tanzania Bara.

Alisema suala la kutoa maamuzi katika migogoro ya ardhi huwa ni gumu, lakini aliwaambia wenyeviti hao kuwa wanapaswa kuwa imara kwa kutenda haki, ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya utatuzi wa mashauri yanayowafikia.

Alisema wenyeviti hao wanapaswa kutenda haki hata kama serikali ndiyo imeshitakiwa hawapaswi kuiogopa kwa kuipendelea.

Magufuli, mmoja wa mawaziri maarufu zama za Serikali ya Awamu ya Tatu, akiwa Waziri wa Ujenzi, alisema aliamua kutoa kauli hiyo kutokana na kuwapo kwa taarifa kutoka maeneo mengi nchini zinazoeleza kuwa wananchi wengi wamenyang’anywa ardhi bila kulipwa fidia.

“Najua wakati mwingine kutoa maamuzi ni matatizo, lakini msiogope kutoa maamuzi, lakini pia muwe imara wakati wa kutoa uamuzi, kwa kuhakikisha haki za wanyonge zinapatikana na speed ya utatuzi wa migogoro inakuwa kubwa, ili kumaliza mashauri 7,228 yaliyopo,” alisema.

Aliagiza kufanyika haraka kwa utatuzi wa migogoro ya ardhi iliyoko katika mabaraza hayo, kwa kuwa ipo inayochelewa kusikilizwa kwa kuwapo kwa mazingira ya rushwa.

Aliwataka wenyeviti hao kuhakikisha kuwa wanaitumia vizuri sheria namba 4 na namba 5 kifungu (3 (g)), ili kutoa maamuzi sahihi.

“Sheria namba 4 na 5 lazima zizingatiwe, ili kama shamba lolote la mwananchi linapochukuliwa kwa ajili ya matumizi yoyote ya serikali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa sekondari, mwananchi huyo ni lazima afidiwe,” alisema.

Waziri Magufuli pia aliziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaunda mabaraza ya ardhi na nyumba katika ngazi ya kata na vijiji kwa lengo la kuharakisha utatuzi wa migogoro katika ngazi ya wilaya.

Naye Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, Bahati Mlole, alisema ukosekanaji wa fedha unachangia ucheleweshwaji wa mashauri, kwa kuwa utendaji wa mabaraza ni vikao na kuwa posho kwa wajumbe limekuwa ni tatizo.

Mkutano huo wa wenyeviti ni wa kwanza tangu kuanzishwa kwa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Oktoba mosi, 2003 na kuwakutanisha wenyeviti wa mabaraza kutoka katika wilaya zote za Tanzania Bara, majaji na wasajili ili kujadili kwa pamoja mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na njia bora ya utatuzi wa migogoro.
 
Ana wasiwasi na kibarua kuota majani katika mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri litakalofanyika mwaka 2010....🙂. Huyu ni mmoja wa mawaziri ambao kwa maoni yangu anastahili kuondolewa.
 
Ana wasiwasi na kibarua kuota majani katika mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri litakalofanyika mwaka 2010....🙂. Huyu ni mmoja wa mawaziri ambao kwa maoni yangu anastahili kuondolewa.

labda ana perform to the audience and judges na matokeo yake ndio haya:

6kgavyg.gif
 
Ana wasiwasi na kibarua kuota majani katika mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri litakalofanyika mwaka 2010....🙂. Huyu ni mmoja wa mawaziri ambao kwa maoni yangu anastahili kuondolewa.
Ni dhahiri kuwa ardhi sasa imekuwa ndio wimbo wa taifa lakini kwanini uhusianishe harakti za mh.waziri na na hofu ya kuondolewa uwaziri; kwani wewe bubu ushakuwa waziri nini??

JK anafahamu walio wake na kama haumo basi ni wazi kuwa wewe siye wake.

Acha chuki binafsi kwa huyo bwana Magufuri,mwacheni achape kazi,the way alivyoingia ndivyo atakavyotoka.

Nimekushauri tu Bubu
 
...yaani hayo mabaraza ndio mwanzo wa ubabaishaji,rushwa na upotevu wa muda na pesa kwa posho na vikao visivyoisha,hao wabunge tunaowalipa mabilioni kuwaweka Dodoma ina maana hawawezi kuja na kitu fair na kinachoeleweka kuliko huo upuuzi wa mabaraza...kazi ipo kweli kweli na shida nyingine ni za kujitakia tuu.
 
Magufuli hajafanya mapya hadi sasa....ARDHI bado tatizo? Leo viwanja kigamboni imekuwa DEAL kubwa...lkn hata hivyo bado PLAN za JIJI ni FINYU ktk hizi ENEO JIPYA>>>>>
 
Magufuli atoa mpya

na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, amezijia juu halmashauri nchini na kuzitaka kuacha mara moja kuvunja nyumba za wananchi zilizojengwa katika maeneo ya makazi ambayo hayajapimwa.

Alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam jana, alipokabidhi barua ya toleo kwa wakazi wa eneo la Hananasif katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya zamani vya Shule ya Msingi Hananasif.

“Hakuna sababu ya kuwabomolea (waliojenga maeneo yasiyopimwa), kinachotakiwa ni kuwatambua na kuwapa huduma muhimu… wananchi kuishi maeneo holela si tatizo lao, ni tatizo letu, kwani wananchi walivamia maeneo hayo kwa sababu serikali haikuwa na utaratibu wa kuwatengea maeneo maalumu ya kujenga tangu awali,” alisema Magufuli.

Alisema Sheria namba 4 na 5 ya Ardhi ya mwaka 1999 katika kifungu cha 3 (G) inawatambua wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyopimwa na kuwa endapo maeneo yao yanatakiwa yabomolewe, wanatakiwa walipwe fidia kwanza.

Aliwaonya wakurugenzi wa manispaa zote na kusema kuwa sheria hiyo inawalinda wanaokaa katika makazi yasiyopimwa na kuwataka wananchi kuwachukulia sheria wakurugenzi watakaowabolea nyumba zao kwa kuwashitaki katika mabaraza ya ardhi na vyombo vingine vya sheria.

Magufuli aliwatahadharisha wakurugenzi watakaokaidi agizo hilo na kuendelea kuwabomolea wakazi wa maeneo yasiyopimwa na kueleza kuwa watakaokaidi agizo hilo watajifunza kwa kuwekwa ndani.

Aidha, aliwataka wakurugenzi hao kuacha kumpelekea barua za mapendekezo ya kubadilisha matumizi ya ardhi ya maeneo ya wazi na kudai kwamba watakaofanya hivyo, atazituma barua zao moja kwa moja kwa Rais Jakaya Kikwete na kusisitiza kuwa hatobadilisha hati hizo kama wanavyotaka.

Hata hivyo, alitoa wito kwa halmashauri zote nchini kuwa na mkakati wa kujenga makazi bora badala ya kubomoa na kutambua makazi yaliyojengwa holela kwa kutoa huduma muhimu.

“Kutokana na Sheria ya Ardhi namba 4 na 5 ya mwaka 1999, ardhi ina thamani, ila iliyopimwa ina thamani zaidi na ni mtaji unaoweza kutumika kuwapunguzia wananchi umaskini kwa kuitumia kama dhamana ya kuombea mikopo katika taasisi za fedha.

“Nawasihi wakazi wa Hananasif ambao hamjakamilisha malipo ya barua zenu za toleo mkamilishe, ili mpate barua za toleo,” alisema.

Aliwaagiza wakurugenzi wa wizara wanaohusika na upimaji, ambao waliambatana naye, pamoja na maofisa wa Manispaa ya Kinondoni, kuanza mchakato wa kutoa hatimiliki kwa wananchi watakaopata barua za toleo, ambao idadi yao ni 1,423 na kati ya hao waliokamilisha taratibu za malipo ni 250.

Alisema shughuli za urasimishaji maeneo umeanza katika maeneo ya Isamilo jijini Mwanza na Mailimoja mjini Dodoma na kuwa huo ni ushahidi kuwa serikali inatambua maeneo yaliyojengwa holela, na kwa sasa serikali imeanzisha mradi wa kuzikopesha halmashauri 19, ili ziweze kuwapimia wananchi maeneo yao.

Akizungumzia mafanikio ya mradi wa urasimishaji wa maeneo uliofanyika Hananasif, mkazi wa eneo hilo, Hamisi Kaniki, alisema kuwa mwanzoni ilikuwa vigumu kwa wakazi wa eneo hilo kujua faida za kurasimisha maeneo, lakini sasa wengi wametambua hilo.

Kaniki alimuomba Waziri Magufuli awasaidie kutatua tatizo la kuvamiwa au kuchukuliwa kwa maeneo ya wazi ya eneo hilo, jambo linalosababisha watoto wao waende kucheza katika viwanja vya Biafra Kinondoni ambako nako alidai kuwa wamezuiliwa.

Akijibu, Magufuli alisema serikali tayari imeshatoa agizo la watu wote waliojenga maeneo ya wazi kuyaachia na kuwa wajiandae kuyabomoa hata kama ni taasisi za serikali, haziruhusiwi kujenga au kuchukua maeneo ya wazi.


Source: Tanzania Daima

Mya take: Jk keshapelekewa mangapi na kachukuwa hatua gani kwa wahusika?

Enewei komaa nao Magufuli.
 
Ana wasiwasi na kibarua kuota majani katika mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri litakalofanyika mwaka 2010....🙂. Huyu ni mmoja wa mawaziri ambao kwa maoni yangu anastahili kuondolewa.


Kama kweli magufuli ataachwa kwenye baraza la mawaziri Tanzania, ina maana hakuna waziri wa sasa hata mmoja anayetakiwa kubakia.

Mimi namwona kama Mchapakazi na mpenda ukweli ukimlinganisha na mawaziri wenzie
 
Aidha, aliwataka wakurugenzi hao kuacha kumpelekea barua za mapendekezo ya kubadilisha matumizi ya ardhi ya maeneo ya wazi na kudai kwamba watakaofanya hivyo, atazituma barua zao moja kwa moja kwa Rais Jakaya Kikwete na kusisitiza kuwa hatobadilisha hati hizo kama wanavyotaka.

Duh! Mheshimiwa Magufuli kwa kuwasemelea wenzake kwa Rais!

Yaani hataki barua za mapendekezo yoyote kuhusu mabadiliko ya matumizi ya ardhi, yaani akishaamua ameamua au labda sijamuelewa!?

Na vilevile hao wakurugenzi nao wakiamua kutuma barua za mapendekezo moja kwa moja kwa raisi badala ya kwa waziri wa wizara husika si itakuwa vioja...
 
Yule Waziri anayependa misifa Bwana John wa Pombe leo amejitokeza Kibamba na kusitisha zoezi la wananchi kuhamishwa na kulipwa fidia. Aidha Bwana Pombe ametoa kwa polisi majina ya wote waliotajwa kutoa hundi za kughushi na kudai rushwa ili wachunguzwe. Bwana Magufuli anajifanya kufungua hili kufuli hivi sasa wakati barua za malalamiko ya wakazi hao zilishafika mezani kwake siku nyingi sana lakini hakuchukua hatua zozote. Habari zaidi, soma magazeti ya kesho.

PM
 
magazeti gani? mimi sielewi unachopinga. unadhani kutoa uamuzi ni hivi hivi kama usemavyo, au initaji tafakuri. utaaminiji aliyeandika kama sio watu janjajanja.

pia utafanyaje kazi kama kila barua inayokufikia unaitolea hukumu bila kujua kitu gani na nani kaandika physically. kama muungwana kakalia majina anyopelekewa, iweje huyu awe kimbelembele. any way we might have a different views but I am clear to my best of my knowledge.
 
Mushobozi unapoteza muda wako na huyi Gwandumi ? Pole sana kama hujagundua hilo
 
Back
Top Bottom